Home About Articles Ask the Sheikh
null

JIBU LA SWALI

July 06, 2004
46

Swali: Imetajwa katika kitabu cha Mfumo wa Kijamii uk. 41:

إِذَا زَوَّجَ أَحَدُكُمْ خَادِمَهُ عَبْدَهُ أَوْ أَجِيرَهُ فَلَا يَنْظُرُ إِلَى مَا دُونَ السِّرَّةِ وَفَوْقَ الرُّكْبَةِ فَإِنَّهُ عَوْرَةٌ

"Mmoja wenu akimwozesha mtumishi wake (wa kike) kwa mtumwa wake au mwajiriwa wake, basi asitazame (sehemu iliyo) chini ya kitovu na juu ya magoti, kwani hiyo ni 'awrah."

Hadith hii imetajwa katika muktadha wa kutoa dalili ya kuruhusiwa kwa mwanamume kuangalia kile ambacho si 'awrah kwa mwanamke, na mwanamke kuangalia kile ambacho si 'awrah kwa mwanamume. Sasa, kuna tofauti gani kati ya kuangalia sehemu iliyo chini ya kitovu na juu ya goti kwa mtumishi wake kabla ya kumwozesha na baada ya kumwozesha?

Jibu: Inaonekana kuna mkanganyiko katika kuelewa swali hilo. Maana ya hadith ni: Mmoja wenu akimwozesha mtumishi wake, yaani mtumwa wake wa kike (amah), kwani neno (khadim) hutumika kwa mwanamume na mwanamke. Mtumwa wa kike kabla ya kuozeshwa na bwana wake kwa mtu mwingine, anakuwa ni halali kwake (milki ya mkono wa kulia) na inaruhusiwa kwake kuona 'awrah yake. Lakini akishaolewa, inakuwa haramu kwa bwana wake (yule aliyemwozesha) kuangalia 'awrah yake. Inaruhusiwa kwake kuangalia tu kile ambacho si 'awrah kwa mtumwa wa kike, yaani sehemu zilizo chini ya goti na juu ya kitovu, maadamu amebaki kuwa ni mtumwa wake na hajampa uhuru. Alichokifanya ni kumwozesha tu kwa mtumwa wake au mwajiriwa wake na amebaki kuwa mtumwa, yaani hajawa mwanamke huru; vinginevyo, ingekuwa haramu kwake kuangalia mwili wake wote isipokuwa uso na vitanga vya mikono pekee.

Kwa hivyo, matini ya hadith:

«إِذَا زَوَّجَ أَحَدُكُمْ خَادَمَهُ عَبْدَهُ أَوْ أَجِيرَهُ...»

Basi أحدكم ni fa'il, خادَمَه ni maf'ul bihi wa kwanza wa kitendo زوّج, na عبدَه au أجيره ni maf'ul bihi wa pili wa زوّج, na wala si atf bayan ya خادمه. Hadith hii ni dalili kwamba uhalali wa bwana kuangalia mtumwa wake wa kike mzima (kwa sababu ni milki ya mkono wa kulia), uhalali huu unafutwa katika kile ambacho ni 'awrah kwa mtumwa wake baada ya kuolewa, kwani anakuwa si halali tena kwake. Hivyo inakuwa haramu kwake kuangalia 'awrah yake, yaani sehemu iliyo chini ya kitovu na juu ya goti, kwa sababu yeye ni mtumwa ambaye amemwozesha na hakumwacha huru.

Kwa hivyo, manthuq (maana ya wazi) ya hadith hii inafaa kuwa dalili ya uharamu wa mwanamume kuangalia 'awrah ya mwanamke. Na mafhum (maana inayofahamika) ya manthuq haya ni kwamba inaruhusiwa kwa mwanamume kuangalia kile ambacho si 'awrah kwa mwanamke, iwe ni mwanamke huru au mtumwa. Na mwanamume na mwanamke ni sawa katika hili; mwanamume huangalia kile ambacho si 'awrah kwa mwanamke, na mwanamke huangalia kile ambacho si 'awrah kwa mwanamume.

19 Jamada al-Ula 1425 H 06/07/2004 M

Share Article

Share this article with your network