Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Majibu ya Maswali: Kuhusu Sheria za Fikra na Thariqah

January 02, 2015
4685

(S mfululizo wa majibu ya mwanachuoni Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook "Fikri")

Majibu ya Maswali Kuhusu Sheria za Fikra na Thariqah

Kwa Abdulnaser Fakhaydah - Ibrahim M Bader

Maswali:

Abdulnaser Fakhaydah:

Assalamu Alaikum, Mwenyezi Mungu akuhifadhi na akunusuru kwa ajili ya ushindi wa Uislamu. Swali langu ni: Je, inawezekana kwa nyenzo (wasail) kuingizwa ndani ya Fikra, kwa mujibu wa mgawanyo wa مبدأ (itikadi) kuwa ni Fikra na Thariqah? Mtoto wako na ndugu yako: Abdul Nasser Hamid Abu Ahmed.

Ibrahim M Bader:

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh... Baada ya hayo, nina maswali kuhusu Fikra na Thariqah:

a- Je, kuna hukumu katika Fikra ambazo hazina hukumu katika Thariqah? Ikiwa jibu ni ndiyo, je, hukumu zinazohitaji adhabu za kuta’zir (adhabu za hiari ya kadhi) zinachukuliwa kuwa hivyo; mfano wake ni kama ukiritimba, udanganyifu, riba na fikra kama hizo ambazo zimeachiwa ijtihadi ya Imamu, hivyo zinatofautiana hukumu zake kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine?

b- Je, kuna hukumu katika Thariqah zinazomhusu mtu binafsi, au zinahusu tu dola au kikundi? Ikiwa hakuna hukumu zinazomhusu mtu binafsi, basi nini kinaitwa kule kurekebishwa kwa mke mkaidi (nashiz) na mumewe, na nini kinaitwa kulinda mali na heshima na mtu binafsi, na jihadi ya mtu binafsi, na mzazi kumpiga mwanawe kwa ajili ya Swala baada ya umri wa miaka kumi...?

Barakallahu fika Sheikh wetu na akusaidie katika yale yenye kheri kwa Uislamu na Waislamu.

Jibu:

Wa Alaikum Salaam Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh.

Maswali haya mawili yana mfanano na uhusiano fulani, hivyo nitayajibu kwa pamoja:

  • Uislamu ni Fikra na Thariqah. Aqeedah na hukumu za kisheria zinazotatua matatizo ya mwanadamu ni Fikra, na hukumu za kisheria zinazobainisha namna ya kutekeleza masuluhisho hayo, kulinda Aqeedah, na kulingania Da’wah, ni Thariqah.

  • Nyenzo (Wasail) ni vitu vya kimaada ambavyo mwanadamu huvitumia anapotekeleza vitendo vyake, au kwa maneno mengine ni vifaa vya kimaada vinavyotumika kutekeleza vitendo (kama vile kompyuta). Na mitindo (Asalib) ni namna zisizo thabiti ambazo mwanadamu huziweka kwa ajili ya kutekeleza vitendo vyake, au kwa maneno mengine, mtindo ni namna maalumu ya kutekeleza tendo, na ni namna isiyo ya kudumu, kama (namna ya kugawa kipeperushi). Nyenzo na mitindo ni mambo ya kidunia yanayorejea kwenye makadirio ya mwanadamu, na maadamu huu ndio uhalisia wake, basi hayawezi kuingizwa chini ya istilahi ya Fikra wala chini ya istilahi ya Thariqah. Hii ni kwa sababu Fikra na Thariqah ni mambo thabiti yasiyobadilika, na hayachukuliwi isipokuwa kutoka katika Uislamu. Ama nyenzo na mitindo huchukuliwa kutoka kwa Mwislamu na kafiri na hubadilika na kugeuka kulingana na mahitaji; hivyo basi, hali yake ni sawa na sayansi za kidunia kama vile hisabati, fizikia, mbinu za ukuzaji wa matunda na miti, na viwanda vya silaha... Haya yote ni mambo ya kidunia ambayo Uislamu umewaachia watu, Mwislamu hujifunza kutoka kwa Mwislamu mwenzake au kwa kafiri kwa sababu hayafungamani na mtazamo wa maisha (point of view). Hivyo basi, mambo ya kidunia kama vile nyenzo, mitindo na sayansi za kidunia ambazo hazifungamani na mtazamo wa maisha, hayaingii chini ya istilahi ya Fikra na istilahi ya Thariqah. Hii ni kwa sababu Fikra na Thariqah kama tulivyotaja hapo awali ni "mambo thabiti yasiyobadilika, na hayachukuliwi isipokuwa kutoka katika Uislamu, ama nyenzo na mitindo huchukuliwa kutoka kwa Mwislamu na kafiri na hubadilika na kugeuka kulingana na mahitaji, hali yake ikiwa ni sawa na sayansi za kidunia...".

  • Hakuna katika Uislamu Fikra isiyo na Thariqah ya kuitekeleza:

  • Ama kuhusu adhabu za kuta’zir (uqubat ta'ziriyyah), nazo ni adhabu kwa maasi ambayo Sharia haikuweka adhabu thabiti bali imeachia uamuzi wa adhabu yake kwa Imamu au Kadhi... hizo ni miongoni mwa hukumu za Thariqah. Na ukweli kwamba Sharia haikuainisha adhabu haumaanishi kamwe kwamba haikuweka njia ya kutekeleza hukumu za kisheria ambazo imeadhibu kwa kutozingatiwa kwake kwa njia ya ta’zir, kwa sababu imeweka sheria ya ta’zir na ikabainisha maelezo ya hukumu zake na aina zake... na ikamwachia Imamu pekee kuchagua miongoni mwa aina za adhabu ambazo Sharia imezibainisha, na kwa kiwango ambacho anakiona kinafaa kwa uhalisia wa maasi na uhalisia wa muasi. Hii ina maana kwamba Sharia imebainisha namna ya kutekeleza hukumu hizi kwa kutaka kutekelezwa kwa adhabu kwa asiyezizingatia, lakini kiwango cha adhabu hii na aina yake... hiki ndicho Sharia imemwachia Imamu au naibu wake.

  • Hukumu za Thariqah kuna zinazohusu dola na nyingine zinazomhusu mtu binafsi; hivyo kumwadhibu mtoto, kumtia adabu mke wakati wa ukaidi (nashiz), na baadhi ya hukumu za Jihadi zinazohusiana na mtu binafsi kujilinda... ni miongoni mwa hukumu za Thariqah, nazo zinahusiana na mtu binafsi. Lakini mara nyingi hukumu za Thariqah huhusiana na dola kwa sababu dola yenyewe ni Thariqah ya kutekeleza hukumu za Uislamu.

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah

AF2

Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Google Plus

Share Article

Share this article with your network