Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Majibu ya Maswali: Kuhusu Ardhi Mfu na Kharaji kwa Dhimmia

September 15, 2013
3963

(Sfululizo wa majibu ya mwanachuoni Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, Ameer wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook)

Majibu ya Maswali Kuhusu Ardhi Mfu na Kharaji kwa Dhimmia

Kwa: Zaman Al-Ghurba

Swali:

Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh

Kuna swali lenye sehemu mbili linalonijia akilini na limenifanya nitafakari sana katika kitabu cha Nidhamu ya Kiuchumi (Al-Nidham al-Iqtisadi) kuhusu ardhi mfu katika ardhi ya Kharaji, na mada hii imejirudia katika kitabu cha Amwal (Al-Amwal) kwa mtindo ule ule; nayo ni kwamba ardhi mfu iliyomo ndani ya ardhi ya Kharaji inachukuliwa kama ardhi ya Ushri kwa Muislamu, hivyo anaruhusiwa kuimiliki na hakuna Kharaji juu yake, bali Ushri pekee. Lakini kwa Dhimmia, haruhusiwi kuimiliki na hulipa Kharaji juu yake. Swali: Kwa nini haimiliki wakati imechukuliwa kama ardhi ya Ushri, na yeye anaruhusiwa kuimiliki katika ardhi ya Ushri? Hivyo msingi ni kwamba achukuliwe kama ardhi ya Ushri kama alivyochukuliwa Muislamu, hii ni kwa upande wa kwanza.

Ama swali la pili: Kwa nini tunasema kwamba Dhimmia anapaswa kulipa Kharaji kwenye ardhi ya Ushri, ilhali Kharaji haiko kwenye ardhi ya Ushri? Asili ni kwamba achukuliwe kulingana na asili na tusiseme Kharaji; kwa sababu lina dhana ya kisheria (mafhum shar'i), na hapa tumekhalifu ufafanuzi kwa kuuita mali inayochukuliwa kutoka kwa Dhimmia kwenye ardhi ya Ushri kama "Kharaji". Kwa nini kusiwe na ijtihadi katika kuipa jina mali hii? Jazakallahu Khairan.

Jibu:

Wa Alaikum Salam wa Rahmatullahi wa Barakatuh

1- Ardhi mfu ima iwe katika ardhi ya Ushri au katika ardhi ya Kharaji;

a- Ama ardhi ya Ushri, kuhuisha ardhi mfu ndani yake kunaifanya ibaki kuwa ya Ushri. Ikiwa Muislamu ataihuisha, anamiliki asili yake (raqabah) na manufaa yake, na hulipia Ushri kama zaka. Ikiwa kafiri Dhimmia ataihuisha, inabaki kuwa ya Ushri, anamiliki asili yake na manufaa yake, lakini hulipia Kharaji na siyo Ushri, kwa sababu Ushri ni zaka, na zaka haitolewi na kafiri... Na kwa sababu ardhi ya kilimo ima ilipiwe Ushri kulingana na hukumu za kisheria, au ilipiwe Kharaji. Na kwa sababu Ushri hautolewi na kafiri, basi hulipa Kharaji.

b- Ama ardhi mfu ya Kharaji, iko aina mbili:

  • Ardhi ya Kharaji ambayo tayari ilishawahi kuwekewa Kharaji hapo awali, kisha ikawa mfu. Hii ikiwa itahuishwa na Muislamu au kafiri, sifa yake haibadiliki, bali inabaki kuwa ardhi ya Kharaji ambapo Muislamu na kafiri wote hulipa Kharaji juu yake.

  • Aina ya pili ni ardhi ya Kharaji ambayo haikuwahi kuwekewa Kharaji hapo awali. Hii ikiwa itahuishwa na Muislamu, inakuwa ardhi ya Ushri na hulipa Ushri. Lakini ikiwa itahuishwa na kafiri Dhimmia, sifa yake haibadiliki bali inabaki kuwa ardhi ya Kharaji ambayo hulipiwa Kharaji.

c- Ama kuhusu kwa nini tunasema Dhimmia anapaswa kulipa Kharaji kwenye ardhi ya Ushri ikiwa ataimiliki, hiyo ni kwa sababu ardhi haikosi kuwa na wajibu wa kifedha (wadhaifa). Ni ardhi ya Ushri ambapo Muislamu hulipa Ushri kama zaka, na kwa sababu zaka haitolewi na Dhimmia, na ardhi ya kilimo haikosi kuwa na wajibu kulingana na hukumu za Sharia, basi Dhimmia hulipa Kharaji ikiwa ataimiliki.

  • Ili kufafanua jambo hili, yaani jinsi gani ardhi ya kilimo haikosi kuwa na wajibu, tunasema:

Dalili za hukumu za ardhi ya kilimo hazikufanya kuwe na ardhi yoyote isipokuwa iwe ya Ushri au Kharaji.

Na kuhusu jinsi gani ilivyo hivyo, huu hapa ni ufafanuzi:

Dalili za hukumu za ardhi ya kilimo zilizokuja katika Sharia ni:

• Dalili za jumla kuhusu kila ardhi, ambazo zinawajibisha zaka ya Ushri au nusu ya Ushri kulingana na hukumu za kisheria...

فِيمَا سَقَتْ الأَنْهَارُ وَالْغَيْمُ الْعُشُورُ، وَفِيمَا سُقِيَ بِالسَّانِيَةِ نِصْفُ الْعُشْرِ

"Katika kile kinachonyeshewa na mito na mawingu ni Ushri (fungu la kumi), na katika kile kinachonyeshewa kwa kutumia ngamia ni nusu ya Ushri." na nyinginezo.

• Baada ya ushindi (futuh), lilitokea tatizo jipya kwenye ardhi ambazo zilitolewa kwenye andiko la jumla na kuwekewa Kharaji. Abu Ubayd amesema: Yazid bin Harun ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Abi Dhi’b, kutoka kwa Az-Zuhri, amesema: Mtume wa Allah (saw) alikubali Jizya kutoka kwa Majusi wa Bahrain. Az-Zuhri amesema: Yeyote aliyesilimu miongoni mwao, Uislamu wake ulikubaliwa, na Uislamu wake ukahifadhi nafsi yake na mali yake isipokuwa ardhi, kwani hiyo ni fay’ kwa Waislamu, kwa sababu hakusilimu mara ya kwanza akiwa katika nguvu (kabla ya kushindwa). Na hivi ndivyo alivyohukumu Umar (ra) katika ardhi ya As-Sawad kwa kusema kwake: "Nimeona nizuie ardhi hizi pamoja na wakulima wake, na niweke Kharaji juu yake...", na nyinginezo.

• Kwa hiyo, kila ardhi ya kilimo katika Dar al-Islam ina zaka kulingana na hukumu za kisheria, isipokuwa aina maalum ambayo ina Kharaji.

• Hukumu ya jumla inabaki katika ujumla wake "kila ardhi ya kilimo katika Dar al-Islam ina zaka" kulingana na hukumu za kisheria, na hakuna kinachotoka humo isipokuwa kile kilichohusishwa kwa andiko lingine "Ardhi ya Kharaji".

2- Hii ndiyo hukumu ya ardhi ya kilimo, nayo ni: ima iwe ya Ushri au ya Kharaji. Huu ndio mgawanyo wa ardhi ya kilimo, hivyo haikosi kuwa na wajibu, yaani hakuna ardhi ya kilimo isiyoitwa ya Ushri au ya Kharaji.

3- Ama kauli yako kwamba Kharaji ina dhana ya kisheria (mafhum shar'i), hivyo ikiwa Dhimmia atalipa Kharaji kwenye ardhi ya Ushri tutakuwa tumekhalifu dhana ya kisheria ya Kharaji, kauli hii si sahihi kwa sababu ardhi ya Kharaji haina sababu ya sifa inayofafanua uhalisia wa ardhi kati ya kuwa ya Ushri au ya Kharaji. Ardhi ni ardhi tu, yaani ni tamko gumu (lafdh jamid). Hii ni ardhi ya Ushri, na inaweza kuwa karibu nayo kuna ardhi ya Kharaji, na hakuna tofauti kati yake si katika udongo wala katika mazao... Hivyo neno Kharaji si sifa inayofafanua inayofungamana na hukumu... Kwa hiyo, Dhimmia kulipa Kharaji kwa ardhi ya Ushri anayoimiliki haina ndani yake ukhulifu wa dhana ya Kharaji.

Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Ameer kwenye Facebook

Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Ameer

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Ameer kwenye Google Plus

Share Article

Share this article with your network