Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Majibu ya Maswali: Kuhusu Mavazi ya Kisheria ya Mwanamke katika Maisha ya Umma na Maisha ya Faragha

January 15, 2015
9603

(Silsila ya majibu ya mwanachuoni Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi")

Kwa: Nessrine Boudhafri - Buluughaka Marami - Mosa Za

Maswali:

Nessrine Boudhafri: Barakallahu fikum Amir wetu na Allah akunusuruni kupitia nyinyi.. lakini swali katika muktadha huu, mlisema katika jibu lenu "kwa hivyo hairuhusiwi kuvaa wigi kwa namna inayodhihirika katika maisha ya umma hata kama amevaa jilbab, isipokuwa akivaa juu ya wigi hilo khimar inayolifunika kikamilifu na kutoacha athari yoyote kwa anayetazama". Inafahamika kutokana na hili kwamba inaruhusiwa kuvaa wigi chini ya khimar au nyumbani kwa mfano, kisha je, wigi halichukui hukumu ya kuunga nywele (wasl)?

Buluughaka Marami: Je, wigi au nywele za bandia hazichukuliwi kuwa ni miongoni mwa kuunga nywele kulikokatazwa katika hadithi ya (mwenye kuunga na mwenye kuungwa)? Na jazakumullahu khayra.

Mosa Za: Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh. Ndugu yangu mpendwa - kuna jambo ambalo limeenea sana kwetu nalo ni kuvaa jilbab juu ya suruali ambalo linafika magotini, je, hili linaruhusiwa?

Jibu:

Wa Alaikum Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh,

Hakika maswali yenu yana mada zinazoshabihiana, na kwa hivyo nitayajumuisha majibu yake pamoja:

A- Hairuhusiwi kwa mwanamke kutoka kwenda katika maisha ya umma isipokuwa kwa vazi la kisheria ambalo ndani yake yanatimia mambo matatu: kusitiri uchi (awrah), kuvaa Jilbab na Khimar, na kutofanya Tabarruj;

  • Kuhusu Jilbab, ni vazi pana lenye kusitiri ambalo hufunika nguo za ndani, na huteremshwa chini ili kufunika miguu, kwani Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لِأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِنْ جَلَابِيبِهِنَّ

"Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie shuka zao (Jilbab)." (QS. Al-Ahzab [33]: 59)

Maana yake ni kuteremsha juu yao nguo zao wanazozivaa juu ya nguo nyingine wanapotoka, kama vile mula’a na milhafa ambazo huziteremsha hadi chini. Kwa hiyo, sharti ya Jilbab ni kuwa imeteremshwa chini hadi ifunike miguu, kwa sababu Mwenyezi Mungu anasema katika aya: ﴿يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِنْ جَلَابِيبِهِنَّ﴾. Hapa ﴿مِنْ﴾ si ya tab'idh (kuonyesha sehemu ya kitu) bali ni ya bayan (ubainifu), yaani kuteremsha mula'a na milhafa hadi chini ili isitiri miguu. Ikiwa miguu imesitiriwa kwa soksi au viatu, basi hilo halitoshelezi badala ya kuteremsha vazi hilo chini kwa namna inayoonyesha kuwepo kwa mteremko huo (irkha’). Si lazima ifunike miguu (nyayo) ikiwa tayari imesitiriwa, lakini ni lazima ifike kwenye miguu ili kuwe na irkha’ (mteremko), yaani Jilbab iwe imeshuka chini kwa namna iliyo wazi ambayo kwayo itajulikana kuwa ni vazi la maisha ya umma ambalo mwanamke anapaswa kuvaa, na ndani yake udhihirike mteremko (irkha’). Hili linamaanisha kufika ardhini ikiwa miguu iko wazi, na inatosha kufika kwenye miguu ikiwa miguu imesitiriwa kwa viatu na soksi, lakini si chini ya kufika kwenye miguu ili kutimiza maana ya neno "wajiteremshie" (yerkhina).

Kwa mujibu wa hili, hairuhusiwi kwa mwanamke katika maisha ya umma kutoka akiwa amevaa suruali na juu yake kuna koti refu linalofika magotini mwake pekee bila kufika kwenye miguu yake iliyositiriwa kwa soksi, kwani hili haliendani na maana ya kisheria ya Jilbab. Hairuhusiwi kwa mwanamke kutoka kwenda katika maisha ya umma isipokuwa kwa Jilbab linalofunika nguo zake za ndani na kuteremshwa chini hadi miguuni kwake. Na ikiwa hapati, basi asitoke au aazime Jilbab kwa jirani yake kutokana na hadithi iliyopokelewa na Muslim katika Sahih yake kutoka kwa Umm Atiyyah, amesema:

أَمَرَنَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنْ نُخْرِجَهُنَّ فِي الْفِطْرِ وَالْأَضْحَى، الْعَوَاتِقَ، وَالْحُيَّضَ، وَذَوَاتِ الْخُدُورِ، فَأَمَّا الْحُيَّضُ فَيَعْتَزِلْنَ الصَّلَاةَ، وَيَشْهَدْنَ الْخَيْرَ، وَدَعْوَةَ الْمُسْلِمِينَ

"Mtume wa Allah (saw) alituamrisha tuwatoe katika (sherehe za) Al-Fitr na Al-Adh'ha; wanawake waliovunja ungo, wenye hedhi na waliofaraghani. Ama wenye hedhi, watajitenga na sehemu ya kuswalia, lakini washuhudie kheri na dua za Waislamu."

Nikasema: "Ewe Mtume wa Allah, mmoja wetu anaweza kuwa hana Jilbab." Akasema:

لِتُلْبِسْهَا أُخْتُهَا مِنْ جَلَابِيبِهَا

"Dada yake amvalishe miongoni mwa majilbab yake." (HR. Muslim)

  • Kuhusu Khimar, ni kifuniko cha kichwa ambacho hufunika nywele, shingo, na uwazi wa shati (kifuani), Allah (swt) anasema:

وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَى جُيُوبِهِنَّ

"Na waangushe vifuniko vyao (vya kichwa) mpaka vifuani mwao." (QS. An-Nur [24]: 31)

Maana yake ni wazungushe vifuniko vya vichwa vyao juu ya shingo zao na vifua vyao, ili kuficha kile kinachodhihirika katika kola ya shati na kola ya vazi kutokana na shingo na kifua.

  • Kuhusu Tabarruj, inamaanisha mapambo yanayovutia macho. Kuvaa suruali kunasitiri uchi, lakini ni miongoni mwa tabarruj ikiwa hakuna Jilbab juu yake. Na wigi ni miongoni mwa tabarruj kwa sababu linavutia macho. Kwa hivyo, hairuhusiwi kuvaa wigi kwa namna inayodhihirika katika maisha ya umma hata kama amevaa Jilbab, isipokuwa akivaa juu ya wigi hilo khimar inayolifunika kikamilifu na kutoacha athari yoyote kwa anayetazama. Kwa sababu pambo hata likiwa limesitiriwa, likivutia macho linakuwa ni tabarruj, kama Alivyosema Mwenyezi Mungu (swt) kuhusu uharamu wa kudhihirisha sauti ya kitalimbwasere (khal-khal) kinachovaliwa mguuni chini ya vazi la mwanamke; akipiga chini mguu wake na kitalimbwasere kikatoa sauti inayokijulisha, basi huku ni tabarruj hata kama kimesitiriwa kwa sababu kwa kutoa sauti yake kimekuwa ni chenye kuvutia macho:

وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِنْ زِينَتِهِنَّ

"Wala wasipige miguu yao ili yajulikane yale wanayoyaficha katika mapambo yao." (QS. An-Nur [24]: 31)

B- Ama kuhusu ikiwa wigi linachukua hukumu ya kuunga nywele (wasl), sivyo hivyo. Wigi si kuunga nywele, bali mwenye kuunga (waasila) na mwenye kuungwa (mustawsila) ni yule anayerefusha nywele kwa kufunga nywele nyingine nazo ili zionekane nzuri na ndefu. Imeelezwa katika vyanzo vya lugha kuhusu maana ya Waasila: Katika Lisan al-Arab "...na al-Waasila miongoni mwa wanawake ni: Yule anayeunga nywele zake na nywele za mwanamke mwingine." Na hili ni haramu katika sehemu yoyote alipo mwanamke, hata nyumbani kwake kulingana na hadithi iliyopokelewa na Bukhari kutoka kwa Abu Hurairah (ra), kutoka kwa Mtume (saw) amesema:

لَعَنَ اللَّهُ الوَاصِلَةَ وَالمُسْتَوْصِلَةَ

"Allah amemlaani mwenye kuunga nywele na mwenye kuungwa." (HR. Bukhari)

Ama wigi, ni nywele zinazovaliwa juu ya nywele asilia. Nalo ni miongoni mwa tabarruj ambayo hairuhusiwi kwa mwanamke kuivaa katika maisha ya umma, kama vile kutofaa kuvaa suruali katika maisha ya umma bila Jilbab kwa sababu ni tabarruj, na tabarruj kama inavyojulikana ni haramu.

Kwa hivyo, inaruhusiwa kwa mwanamke kuvaa wigi kichwani mwake mbele ya mume wake kama pambo kwake katika maisha yake ya faragha, lakini hairuhusiwi kulivaa katika maisha ya umma bila ya kuwa na khimar juu yake inayolifunika kikamilifu, kwani kudhihirika nalo katika maisha ya umma ni tabarruj na ni haramu.

Ndugu yenu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

AF2

Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Google Plus

Share Article

Share this article with your network