Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Majibu ya Maswali: Kuhusu Kuzungumza Juu ya Ndoto (Ruya), na Sheria ya Udhamini wa Kijamii.

September 11, 2013
4185

** (Sfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Ata bin Khalil Abu al-Rashta, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa Maswali ya Wageni Kwenye Ukurasa Wake wa Facebook)**

Kwa Sham al-Izz

Swali:

Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh

Barakallahu fikum na Mwenyezi Mungu ayaongoze hatua zenu kwenye njia ya haki.

1- Je, inaruhusiwa kuzungumza kuhusu ndoto (ruya) kwenye ukurasa wangu binafsi, au huku ni kuonyesha (riya)... ni ndoto binafsi na muhimu sana.

2- Ninafanya kazi kama mfamasia na tumewekewa sheria ya udhamini wa kijamii (takaful) ambayo ni ya lazima; hakuna leseni ya kazi bila kulipa ada... wanachukua kiasi fulani kutoka kwetu na kukiwekeza benki, hivi ndivyo ilivyoandikwa kwenye kipengele hicho, na mfamasia mwenzetu anapofariki, mfuko wa udhamini wa kijamii huwapa watu wa familia yake dinari za Jordan 25,000. Swali: Je, jambo hili linajuzu?

Je, nini niwausie familia yangu kuhusu pesa hizi? Je, inafaa wachukue kiasi nilicholipa na kutoa sadaka kilichobaki, au zirudishwe kwenye chama, au wafanye nini nazo? Mwenyezi Mungu awalipe kheri.

Jibu:

Wa Alaykum Assalam Warahmatullahi Wabarakatuh

1- Kuhusu kuzungumzia ndoto, Al-Bukhari amepokea kutoka kwa Abu Sa’id al-Khudri, kwamba alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akisema:

إِذَا رَأَى أَحَدُكُمُ الرُّؤْيَا يُحِبُّهَا، فَإِنَّهَا مِنَ اللَّهِ، فَلْيَحْمَدِ اللَّهَ عَلَيْهَا وَلْيُحَدِّثْ بِهَا، وَإِذَا رَأَى غَيْرَ ذَلِكَ مِمَّا يَكْرَهُ، فَإِنَّمَا هِيَ مِنَ الشَّيْطَانِ، فَلْيَسْتَعِذْ مِنْ شَرِّهَا، وَلاَ يَذْكُرْهَا لِأَحَدٍ، فَإِنَّهَا لَنْ تَضُرَّهُ

"Mmoja wenu anapoona ndoto anayoipenda, basi hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu, basi na amhimidi Mwenyezi Mungu kwayo na aisimulie. Na akiona kinyume na hivyo miongoni mwa anayoyachukia, basi hiyo inatoka kwa shetani, basi na ajikinge na shari yake na asiitaje kwa yeyote, kwani haitamdhuru." (Sahih al-Bukhari)

Kuhusu suala la kama kuzungumza juu ya ndoto fulani ni riya au si riya, hilo unaliamua wewe mwenyewe. Mwenyezi Mungu (swt) akuwafikishe na akusaidie katika kila kheri.

2- Ama kuhusu sheria ya udhamini wa kijamii, maana zake ni tofauti... Ikiwa inafanana na sheria ya kustaafu katika vyama vya taaluma, yaani chama cha wafamasia kinakulazimisha kujiunga na sheria ya kustaafu na kulipa ada fulani, na huruhusiwi kufanya kazi kama mfamasia bila kujiunga, yaani hupati leseni ya kufanya kazi ya ufamasia bila kujiunga na kulipa ada... kisha baada ya umri fulani wanakupa mshahara wa kustaafu na/au kiasi fulani cha pesa wakati wa kifo... Ikiwa hali ni hiyo, na kujiunga huku ni kwa lazima la sivyo huruhusiwi kufanya kazi kama mfamasia, basi inaruhusiwa kujiunga kwa sababu hii ni sawa na kuchukua leseni ya kazi ya mubah na hili linajuzu. Na wakati ambapo kujiunga na kulipa ada kutakuwa ni jambo la hiari, na hakuathiri leseni ya kazi, basi haijuzu kujiunga.

Ama kuhusu kuwekeza fedha za chama katika riba, ikiwa jambo hili linategemea ridhaa yako, yaani ikiwa utakubali kuwekeza ada unayolipa katika riba itafanyika hivyo, na usipokubali haitafanyika, basi hapo haijuzu kwako kukubali uwekezaji wa riba. Lakini ikiwa uwekezaji unafanyika bila ridhaa yako, yaani si kwa hiari yako, basi huna kosa, maadamu kujiunga kwako na kulipa ada hakuvuki mpaka wa kupata leseni ya kazi.

Ama kuhusu kile ambacho mfuko huwapa watu wa familia yako wakati wa kifo katika hali hii, yaani katika hali ya kujiunga kwako tu na kile kinacholazimu kwa ajili ya kupata leseni ya kazi, basi inajuzu kwao kukuchukua, na warithi wanastahili kiasi hicho... Na ningependa uwausie kutoa sehemu ya pesa hizo kwa mafukara na masikini, kwani hilo ni bora zaidi na safi zaidi. Mwenyezi Mungu akurefushie umri katika kutenda mema.

Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu al-Rashta

Link ya jibu kutoka kwa ukurasa wa Amir kwenye Facebook

Link ya jibu kutoka kwa tovuti ya Amir

Link ya jibu kutoka kwa ukurasa wa Amir kwenye Google Plus

Share Article

Share this article with your network