Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: Matibabu kwa Kutumia Nishati (Bioenergy)

February 18, 2016
7138

(Silsila ya Majibu ya Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa Maswali ya Wafuasi wa Ukurasa Wake wa Facebook "Fiqhi")
Jibu la Swali
Matibabu kwa Kutumia Nishati (Bioenergy)
Kwa: Iman Thawabteh

Swali:

Assalamu Alaykum,

Mimi ni mwanafunzi wa uuguzi ninayesoma katika Chuo Kikuu cha Hebron. Profesa anayetufundisha alianza kuchukua kozi katika nyanja ya matibabu kwa kutumia nishati (energy healing) na anataka kuendelea na Shahada ya Uzamili (Masters) katika fani hiyo.

Lakini mwenzetu mmoja amefanya utafiti juu ya mada hii na anasema kuwa ni haramu kisheria. Hata hivyo, profesa huyo alimtaka atoe dalili ya kisheria ya mkato kuhusu uharamu wake kwa sababu anataka kukamilisha masomo yake katika fani hiyo, lakini mwanafunzi huyo hakuweza kuleta dalili ya wazi kutoka kwenye Qur'an na Sunnah za Mtume kuhusu mada hii. Je, unaweza kunisaidia kwa kutoa maoni yako na dalili kuhusu mada hii, tafadhali?

Jibu:

Si wazi kutokana na swali nini kinachokusudiwa na matibabu ya nishati, na ingekuwa bora zaidi kama muulizaji angefafanua maana ya matibabu ya nishati ili tumjibu kulingana na swali lake...

Hata hivyo, kuingizwa kwa suala la uharamu katika mada hii kunanifanya nitarajie kwamba haulizi kuhusu nishati ya kifizikia inayohisika kama vile nishati ya mionzi na matibabu ya leza (laser) kwa mfano, au matibabu ya mionzi (radiotherapy) kwa ajili ya kutibu saratani ambapo mionzi yenye nishati ya juu hutumiwa, au picha za Magnetic resonance imaging (MRI) au mfano wa hayo; kwani mambo haya na mengineyo kama haya hayana tatizo katika kuyatumia kama matibabu... Bali natarajia kuwa muulizaji anaulizia kuhusu nishati iitwayo nishati ya uhai (Bioenergy)... Ikiwa nishati hii ndiyo inayouliziwa kuhusu matibabu yake, basi nasema na kwa Allah ndiyo taufiki:

Kulingana na taarifa tulizozipata kuhusu mada ya matibabu ya nishati ya uhai (Bioenergy), imebainika kuwa ni aina ya matibabu yanayojengwa juu ya misingi ya kifalsafa ya Kibudha. Wafuasi wake wanadai kuwa "ni matibabu ya kisaikolojia, kimwili, na kiroho yanayozingatia uelewa wa athari za ghaibu kwa mwanadamu zilizogunduliwa na watu wa kale wa Mashariki, ambapo muhimu zaidi ni kuwepo kwa nguvu inayoenea katika ulimwengu iitwayo Ki, au Chi, au Prana. Mwanadamu anaweza kuivuta na kuifanya itiririke katika miili yake isiyoonekana ili kufikia kinga dhidi ya magonjwa ya kimwili yasiyotibika, na kujikinga na matatizo ya kisaikolojia na sonona. Isitoshe, inadaiwa kumpa uwezo wa kisaikolojia wenye ushawishi unaomwezesha kufikia mafanikio, kubadilisha watu, na kutibu miili na nafsi zao kwa kiasi kikubwa..." Na kwamba ni matibabu yanayochanganya baadhi ya mazoezi na udanganyifu pamoja na ushirikina...

Bila shaka matibabu kama haya ni haramu kwa sababu yanategemea misingi ya kifalsafa ya Kibudha inayopingana na Uislamu, na kwa sababu ni aina ya ushirikina na udanganyifu...

Wala haihitaji kuwepo kwa nass (maandiko) kutoka katika Kitabu (Qur’an) au Sunnah yanayozungumzia matibabu kwa jina la "nishati ya uhai" (Bioenergy) ili kusema kuwa ni haramu, bali inatosha kubainika kuwa matibabu haya yanarejea kwenye misingi ya kifalsafa ya kipagani ya Kibudha na kwamba yanachanganywa na baadhi ya mazoezi ya udanganyifu na ushirikina...

Ikiwa hili ndilo lililokusudiwa katika swali, basi jibu lake ni hili lililotajwa hapo juu, na ikiwa ni aina nyingine basi itajwe kwa uwazi ili tuijibu Inshallah.

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Amir: ![facebook](https://domainnomeaning.com/ar/images/icons/site_logo/facebook.png)

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Google Plus wa Amir: ![Googleplus](https://domainnomeaning.com/ar/images/icons/site_logo/Googleplus.png)

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Twitter wa Amir: ![Twitter](https://domainnomeaning.com/ar/images/icons/site_logo/Twitter.png)

Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir

Share Article

Share this article with your network