Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni mtukufu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amiri wa Hizb ut Tahrir
kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi"
Jibu la Swali
Kujiunga na Kuhusika Katika Majeshi ya Tawala Zilizopo Katika Nchi za Kiislamu
Kwa Muhibuddin
Swali: Swali langu mkiniruhusu: Ni ipi hukumu ya kisheria kuhusu kujiunga na kuhusika katika majeshi ya tawala hizi, yaani je, inajuzu kwa kijana kufanya kazi katika majeshi ya tawala za sasa na kupanda vyeo katika nyadhifa zake...
Jibu: Waalaykum Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh
1- Tumeshatoa jibu hapo awali mnamo tarehe 08/06/2013 kuhusiana na kufanya kazi kama msimamizi ('arif) au polisi (shurti)... na ndani yake kulikuwemo:
[– Abu Ya’la ametoa katika Musnad yake na Ibn Hibban katika Sahih yake, na tamshi ni la Abu Ya’la: Kutoka kwa Abu Said na Abu Hurairah, walisema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ:
لَيَأْتِيَنَّ عَلَى النَّاسِ زَمَانٌ يَكُونُ عَلَيْكُمْ أُمَرَاءُ سُفَهَاءُ يُقَدِّمُونَ شِرَارَ النَّاسِ، وَيَظْهَرُونَ بِخِيَارِهِمْ، وَيُؤَخِّرُونَ الصَّلَاةَ عَنْ مَوَاقِيتِهَا، فَمَنْ أَدْرَكَ ذَلِكَ مِنْكُمْ، فَلَا يَكُونَنَّ عَرِيفاً وَلَا شُرْطِيّاً وَلَا جَابِياً وَلَا خَازِناً
“Hakika utawafikia watu wakati ambapo watakuwako kwenu viongozi wapumbavu wanaowatanguliza watu waovu na kuwakandamiza walio wema, na wanachelewesha swala baada ya wakati wake. Atakayewahi hayo miongoni mwenu, basi asiwe msimamizi ('arif), wala polisi (shurti), wala mkusanya kodi (jabiyan), wala mweka hazina (khazinan).” (Musnad ya Abu Ya'la na Sahih ya Ibn Hibban).
Hadithi hii, Mtume ﷺ anakataza mambo haya manne chini ya utawala wa viongozi wapumbavu kwa namna ya kiujumla (mutlaq).
- Lakini At-Tabarani ametoa katika Al-Saghir na Al-Awsat kutoka kwa Abu Hurairah upokezi ufuatao:
فَمَنْ أَدْرَكَ مِنْكُمْ ذَلِكَ الزَّمَانَ فَلَا يَكُونَنَّ لَهُمْ جَابِياً، وَلَا عَرِيفاً، وَلَا شُرْطِيّاً
Akasema: «فَلَا يَكُونَنَّ لَهُمْ», yaani ukatazaji huo umefungwa (muqayyad) kwa sababu herufi Lam ni kwa ajili ya uhusika (al-ikhtisas). Hii ina maana kwamba ukatazaji katika hadithi ya pili unahusiana na kufanya kazi kwa ajili ya watawala hao kama vile walinzi wao binafsi, idara za usalama zinazohusika na kuwalinda wao, na pia mweka hazina wa mali zao na idara nyinginezo za usalama zinazohusiana na watawala hao... Na kwa sababu kanuni za kimsingi za kifiqhi (qawa’id al-usuliyyah) zinaelekeza kubeba maana ya kiujumla (mutlaq) kulingana na maana iliyofungwa (muqayyad), basi ukatazaji unahusiana na kufanya kazi katika vyombo vya polisi vilivyotengwa kwa ajili ya ulinzi wa watawala na usalama wao... Ama vyombo vingine vya polisi vya kawaida, basi inajuzu. Na bila shaka, kujuzu huku hakumaanishi kuwadhulumu watu au kula haki zao, bali ni kutafuta haki katika kazi... 29 Rajab 1434 H - 08 Juni 2013 M]
- Na neno shurti lililotajwa katika hadithi ni kama ilivyokuja katika Lisan al-Arab cha Ibn Manzur:
[وأَشْرَط فلان نفسَه لكذا وكذا أَعْلَمها له وأَعَدَّها ومنه سمي الشُّرَطُ لأَنهم جعلوا لأَنفسهم علامة يُعْرَفُون بها الواحد شُرَطةٌ وشُرَطِيٌّ... Na al-shurtah katika mamlaka ni kutokana na alama na maandalizi, na mtu ni shurtiyyun na shuratiyyun akinasibishwa na al-shurtah na wingi wake ni shurat, waliitwa hivyo kwa sababu walijiandaa kwa ajili ya hilo na wakajitofautisha kwa alama ambazo wanajulikana kwayo, na inasemekana wao ni kikosi cha kwanza kinachoshuhudia vita...]
- Na imekuja katika Al-Qamus al-Muhit cha Al-Fayruzabadi:
[والشُّرْطَةُ، بالضم: kile ulichoshurutisha, inasemwa: خُذْ شُرْطَتَكَ, na mmoja wake ni al-shurat, kama surad, na wao ni kikosi cha kwanza kinachoshuhudia vita, na kujiandaa kwa kifo, na kundi miongoni mwa wasaidizi wa magavana, naye ni shurtiyyun, kama turkiyyun na juhaniyyun, waliitwa hivyo kwa sababu walijitambulisha kwa alama ambazo wanajulikana kwayo...]
Hivyo basi, kile kinachotumika kwa polisi (shurti) pia kinatumika kwa mwanajeshi (jundi) kwa upande wa kuruhusiwa na kutokuruhusiwa.
Hivyo basi, kufanya kazi katika jeshi katika nchi za Waislamu kunajuzu maadamu si nguvu maalum ya kumlinda mtawala asiyetawala kwa Uislamu, na kumkusanyia mali na kuilinda mali hiyo. Ikiwa yumo katika kikosi maalum cha kumlinda mtawala na mali zake, basi ni haramu. Ama ikiwa kazi yake katika jeshi ni kwa ajili ya mambo mengine, basi inajuzu. Na bila shaka, kujuzu huku hakumaanishi kuwadhulumu watu au kula haki zao, bali ni kutafuta haki katika kazi, na kuifanya vizuri kwa ufanisi.
Natumai hili linatosheleza, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi na Mwenye Hikima zaidi.
Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
17 Sha'ban 1445 H Sawa na 27/02/2024 M
Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amiri (Mwenyezi Mungu amuhifadhi) kwenye: Facebook