(Mfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Ata bin Khalil Abu al-Rashta, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa Maswali ya Wageni kwenye Ukurasa wake wa Facebook)
Kwa Sameh Raihan Abu Maysara
Swali:
Assalamu Alaykum, imeelezwa katika kitabu cha Nidham al-Islam kuwa Dola ya Kiislamu haipati vyanzo vya mapato isipokuwa kupitia njia za kisharia, na pia imeelezwa kuwa inachukua ushuru wa forodha (jamarik) kutokana na usimamizi wake juu ya biashara ya ndani na nje.
Je, hii inaendana vipi na kupinga kwenu sera ya ushuru wa forodha hivi leo kwa msingi wa hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): "Hataingia Peponi mtoza maks (ushuru dhulma)"? Na je, maana ya biashara ya ndani ni kwamba Dola inatoza ushuru wa forodha kwenye biashara kati ya majimbo (wilayat) ya Dola ya Kiislamu yenyewe?
Jibu:
Wa Alaykum Salam wa Rahmatullahi wa Barakatuh
- Hadithi ya al-Maks, ameitoa Al-Hakim katika Al-Mustadrak 'ala al-Sahihayn na akasema kuihusu: "Ni hadithi sahihi kwa sharti la Muslim na hawakuitoa (Bukhari na Muslim)", na matini yake ni:
عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم، يَقُولُ: «لَا يَدْخُلُ صَاحِبُ مَكْسٍ الْجَنَّةَ»
"Kutoka kwa Uqbah bin Amir, amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema: 'Hataingia Peponi mtoza ushuru usio wa kisharia (maks).'" (Al-Hakim katika Al-Mustadrak)
Hadithi hii inahusu raia wa Dola, Waislamu na Ahlu Dhimma. Hawa haijuzu kuchukua ushuru wa forodha kutoka kwao juu ya biashara zao; hivyo wanafanya biashara bila kutozwa ushuru, iwe ni kati ya majimbo ya Dola ya Kiislamu (biashara ya ndani) au kati ya Dola ya Kiislamu na nje (biashara ya nje). Kwa hivyo, wafanyabiashara wa Dola ya Kiislamu, Waislamu na Ahlu Dhimma, hawatozwi ushuru... Jambo hili linathibitishwa na yale aliyoyaweka wazi Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika barua zake kwa wale waliosilimu kwamba hawatozwi ushur (moja ya kumi), yaani hawachukuliwi ushuru wa forodha kwenye biashara:
- Ameeleza Abu Ahmad Humayd bin Makhlad bin Qutayba bin Abdullah al-Khurasani, maarufu kama Ibn Zanjawayh (aliyekufa mwaka 251 H) katika kitabu chake Al-Amwal, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliandika barua kwa kabila la Thaqif waliposilimu, na ndani yake ilikuja: "Humayd alituhadithia... kutoka kwa Urwah bin al-Zubayr, amesema: Hii ni barua ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa Thaqif: 'Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu. Hii ni barua kutoka kwa Muhammad Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa Thaqif...
وَلَا يُعْشَرُونَ
"...na hawatozwi ushuru (ushur)...'" Yaani hauchukuliwi kutoka kwao ushuru wa forodha kwenye biashara zao.
- Na ameeleza Ibn Shabba katika Tarikh al-Madinah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliandika barua kwa Wakristo wa Najran kama Ahlu Dhimma kwamba usichukuliwe ushuru wa forodha kwenye biashara zao... Na imekuja ndani yake: "Abu al-Walid alituhadithia... kutoka kwa Abi al-Fath, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alifanya suluhu na watu wa Najran, na akawaandikia barua: 'Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu. Hii ni barua ya Muhammad Nabii, Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa watu wa Najran wakati hukumu yake iko juu yao...
وَلَا يُعْشَرُونَ
"...na hawatozwi ushuru (ushur).'" Yaani hauchukuliwi ushuru wa forodha kwenye biashara kutoka kwa Ahlu Dhimma, na hiyo ni kwa sababu Wakristo wa Najran walifanyiwa suluhu kama Ahlu Dhimma kwa ushahidi wa yale yaliyokuja katika barua hiyo: "Wakati hukumu yake iko juu yao...", yaani hukumu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).
- Na Abu Ubayd ametoa katika Al-Amwal kutoka kwa Abdul-Rahman bin Ma'qal amesema: Nilimuuliza Ziyad bin Hudayr: Ni nani mliokuwa mkiwatoza ushuru? Akasema: "Hatukuwa tukimtoza Muislamu wala Mu'ahid (aliye na mkataba). Nikasema: Basi nani mliokuwa mkiwatoza? Akasema: Wafanyabiashara wa Harbi (nchi za vita) kama walivyokuwa wakitutoza ushuru tunapowaendea." Na Al-Ashir ni yule anayechukua ushuru (moja ya kumi) kwenye bidhaa zinazoingia katika Dar al-Islam kutoka Dar al-Harb.
• Kwa hivyo, mfanyabiashara mwenye uraia wa Kiislamu, awe Muislamu au Dhimmi, hatozwi ushuru wa forodha...
• Ama kuhusu nchi za Harbi Hukman (zile ambazo si katika vita vya moja kwa moja lakini hazina mkataba), huchukuliwa ushuru kwenye biashara zao kama nchi zao zinavyochukua ushuru kutoka kwa wafanyabiashara wetu... Hilo ni kama ilivyokuja kwa Abu Ubayd katika Al-Amwal: "Nikasema: Basi nani mliokuwa mkiwatoza? Akasema: Wafanyabiashara wa Harbi kama walivyokuwa wakitutoza ushuru tunapowaendea," na kama ilivyokuja kwa Ibn Qudama katika Al-Mughni: "Kutoka kwa Abi Mijlaz Lahiq bin Humayd amesema: 'Walimwambia Umar: Tutachukuaje kutoka kwa watu wa Harb wanapotujia?
قَالَ: كَيْفَ يَأْخُذُونَ مِنْكُمْ إذَا دَخَلْتُمْ إلَيْهِمْ؟ قَالُوا الْعُشْرَ. قَالَ: فَكَذَلِكَ خُذُوا مِنْهُمْ
"Akasema: Wanachukuaje kutoka kwenu mnapoingia kwao? Wakasema: Moja ya kumi (ushur). Akasema: Basi chukueni vivyo hivyo kutoka kwao.'"
Muhtasari:
• Hawatozwi ushuru wa forodha wafanyabiashara wa Dola ya Kiislamu, iwe mfanyabiashara ni Muislamu au Dhimmi.
• Unachukuliwa ushuru wa forodha kutoka kwa mfanyabiashara Mu'ahid kulingana na masharti yaliyowekwa katika mkataba (mu'ahadah).
• Unachukuliwa ushuru wa forodha kutoka kwa wafanyabiashara wa nchi za Harbi Hukman kama nchi hizo zinavyochukua kutoka kwa wafanyabiashara wetu.
• Ama kuhusu nchi za Harbi Fi'lan (ambazo tuko nazo katika vita vya moja kwa moja), wafanyabiashara wao hawaingii katika nchi yetu kwa sababu uhusiano nao ni wa vita vya kivitendo.
Ndugu yenu, Ata bin Khalil Abu al-Rashta
Kiungo cha jibu kutoka kwa ukurasa wa Amir kwenye Facebook
Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir
Kiungo cha jibu kutoka kwa ukurasa wa Amir kwenye Google Plus