Mfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir
Kwenye maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi"
Kwa Abdullah Ibn Al-Mufakkir
Swali:
Assalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuhu our dear Shaikh.
I ask Allah to strengthen you, give you long lasting health and age and allow you to witness the return of the Khilafah and lead us, Ameen.
I have a question regarding the Hizbs draft constitution. In article 7 clause F it states: "The State will implement the rest of the Shari’ah rules and all the Islamic Shari’ah matters, such as transactions, penal codes, testimonies, ruling systems and economics among others equally upon the Muslims and non-Muslims. The State will also implement the same upon those with a covenant, the asylum seekers and all those under the authority of Islam in the same way. It implements them upon all members of society except for the ambassadors, consuls, and similar for they have diplomatic immunity."
My question is regarding the point about Ambassadors. The reality is that sometimes there are temporary ambassadors who only stay for an amount of time then return to their countries and permanent ambassadors who stay in the Khilafah permanently. Does this article apply to both types of ambassadors?
Also, if either of the ambassadors commits a crime or undertakes an illegal activity beyond their remit as an ambassador, are they both judged and punished accordingly by the Khilafah? Or are temporary and permanent ambassadors treated differently in this matter.
Jazakumullahu Khairan.
From: Saifudeen Abdullah
Tafsiri ya Swali:
Assalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuhu, Sheikh wetu mpendwa.
Namuomba Allah akupe nguvu, akupe afya ya kudumu na umri mrefu, na akujaalie uwe miongoni mwa mashahidi wa kurejea kwa Khilafah na utuongoze, Amin.
Nina swali kuhusu mradi wa Katiba ya Hizb, katika Ibara ya "7" kipengele "f" inasema:
"[Dola itatekeleza hukumu zilizosalia za Sharia na mambo yote ya Sharia ya Kiislamu kuanzia miamala, adhabu, ushahidi, mifumo ya utawala na uchumi na mengineyo kwa wote sawia, na itatekelezwa kwa Waislamu na wasio Waislamu kwa usawa. Kadhalika itatekelezwa kwa watu wa mkataba (mu'ahidin), wanaoomba hifadhi (musta'minin) na kila aliye chini ya mamlaka ya Uislamu kama inavyotekelezwa kwa raia wengine, isipokuwa mabalozi, wajumbe na wanaofanana nao kwani wana kinga ya kidiplomasia.]"
Swali langu ni kuhusu nukta inayohusu mabalozi. Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya mabalozi (wajumbe) wa muda ambao hukaa kwa muda fulani kisha hurejea katika nchi zao, na kuna mabalozi ambao huishi katika nchi ya Khilafah kwa kudumu. Je, ibara hii inahusu aina zote mbili za mabalozi?
Na ikiwa mmoja wa aina hizi mbili atafanya uhalifu au kitendo kisicho cha kisheria nje ya mamlaka yake kama balozi, je, atahukumiwa na kuadhibiwa kwa mujibu wa nchi ya Khilafah? Au balozi wa muda na balozi wa kudumu wanatendewa kwa namna tofauti katika suala hili?
Jazakumullahu Khairan.
Kutoka kwa: Saifudeen Abdullah
Jibu:
Wa Alaikum Salaam Wa Rahmatullahi Wa Barakatuhu,
Barakallahu fika kwa dua yako njema kwetu, na tunamuomba Allah akujaalie kheri.
1- Kuhusu swali lako kuhusu mabalozi wa kudumu na mabalozi wa muda, hakuna tofauti kati yao kwa upande wa kisheria. Mradi tu mtu huyo anahusika na maana ya neno "mjumbe" (rasul), basi anafurahia kinga ya kidiplomasia wakati wa kukaa kwake katika nchi ya Khilafah bila tofauti yoyote. Hapo awali, wakati wa Mtume ﷺ, Maswahaba, na karne zilizofuata, hapakuwa na mabalozi wa kudumu waliowekwa makazi, bali wajumbe walikuwa wakitumwa kufikisha ujumbe kisha hurejea nchini kwao, yaani walikuwa kwa mujibu wa usemi wako "mabalozi wa muda/wajumbe wa muda". Baadaye, suala la mabalozi wa kudumu na ofisi za ubalozi duniani liliibuka kutokana na ugumu wa mahusiano na ulazima wa mawasiliano ya kudumu kati ya mataifa na uwepo wa raia wa nchi ya ubalozi katika mataifa hayo. Hivyo, mataifa yakaanza kukubali kufungua balozi za kudumu kwa mataifa mengine katika ardhi zao na kukubali kuidhinisha mabalozi wakaazi katika nchi hizo. Ama huko nyuma, balozi au mjumbe alikuwa akienda mara moja tu kutekeleza ujumbe maalum. Na hili ndilo linalofahamika kutokana na hadithi tukufu kuhusu wajumbe. Ahmad amepokea kutoka kwa Ibn Mas'ud amesema:
جَاءَ ابْنُ النَّوَّاحَةِ وَابْنُ أُثَالٍ، رَسُولاَ مُسَيْلِمَةَ إِلَى النَّبِيِّ ﷺ، فَقَالَ لَهُمَا: أَتَشْهَدَانِ أَنِّي رَسُولُ اللَّهِ؟ قَالاَ: نَشْهَدُ أَنَّ مُسَيْلِمَةَ رَسُولُ اللَّهِ، فَقَالَ النَّبِيُّ ﷺ: آمَنْتُ بِاللَّهِ وَرُسُلِهِ، لَوْ كُنْتُ قَاتِلاً رَسُولاً لَقَتَلْتُكُمَا، قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: قَالَ: فَمَضَتِ السُّنَّةُ أَنَّ الرُّسُلَ لاَ تُقْتَلُ
"Ibn al-Nawwahah na Ibn Uthal, wajumbe wa Musaylimah, walikuja kwa Mtume ﷺ, naye akawauliza: 'Je, mnashuhudia kuwa mimi ni Mtume wa Allah?' Wakasema: 'Tunashuhudia kuwa Musaylimah ni Mtume wa Allah.' Mtume ﷺ akasema: 'Nimemuamini Allah na Mitume Wake; lau kama ningekuwa ni mwenye kumuua mjumbe, basi ningewaua nyinyi wawili.' Abdullah akasema: 'Hivyo basi, Sunnah ikapitika kuwa wajumbe hawauawi.'" (Imepokelewa na Ahmad na akaisahihisha Al-Haythami). Ni wazi kutokana na hadithi hii kwamba maneno yanahusu wajumbe wawili waliotumwa na Musaylimah al-Kadhdhab kwa mara moja.
2- Kuhusu ufafanuzi wako wa adhabu kwa mabalozi na wajumbe, jibu lake lipo katika maelezo ya kipengele "f" cha Ibara ya "7" katika kitabu cha Utangulizi wa Katiba (Muqaddimatul Dustur), na haya ndiyo maandishi yake: [Ama kipengele (f), kuhusu utekelezaji wa hukumu zote za Kiislamu, dalili yake ni yale yaliyotangulia kwamba kafiri analazimika kufuata misingi (usul) na matawi (furu'), na anadaiwa kufuata hukumu zote za Kiislamu. Na hili ni jumuishi kwa raia asiye Muislamu (dhimmi) na asiyekuwa dhimmi miongoni mwa wanaoishi chini ya mamlaka ya Uislamu. Hivyo makafiri wote wanaoingia katika Dar al-Islam, wawe ni mu'ahidin (wenye mkataba) au musta'minin (wanaoomba hifadhi), lazima watekelezewe hukumu za Kiislamu, isipokuwa masuala ya kiitikadi (aqaid), na kila kitendo kinachozingatiwa kuwa ni sehemu ya itikadi, na kila kitendo ambacho Mtume ﷺ aliwaachia wakitekeleze. Isipokuwa tu inatolewa nje ya hapo mabalozi, na wale walio katika nafasi yao, kwani hawatekelezewi hukumu za adhabu, na hupewa kile kinachoitwa kinga ya kidiplomasia, na hiyo ni kutokana na aliyoyapokea Ahmad kutoka kwa Ibn Mas’ud amesema:
جَاءَ ابْنُ النَّوَّاحَةِ وَابْنُ أُثَالٍ، رَسُولاَ مُسَيْلِمَةَ إِلَى النَّبِيِّ ﷺ، فَقَالَ لَهُمَا: أَتَشْهَدَانِ أَنِّي رَسُولُ اللَّهِ؟ قَالاَ: نَشْهَدُ أَنَّ مُسَيْلِمَةَ رَسُولُ اللَّهِ، فَقَالَ النَّبِيُّ ﷺ: آمَنْتُ بِاللَّهِ وَرُسُلِهِ، لَوْ كُنْتُ قَاتِلاً رَسُولاً لَقَتَلْتُكُمَا، قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: قَالَ: فَمَضَتِ السُّنَّةُ أَنَّ الرُّسُلَ لاَ تُقْتَلُ
"Ibn al-Nawwahah na Ibn Uthal, wajumbe wa Musaylimah, walikuja kwa Mtume ﷺ, naye akawauliza: 'Je, mnashuhudia kuwa mimi ni Mtume wa Allah?' Wakasema: 'Tunashuhudia kuwa Musaylimah ni Mtume wa Allah.' Mtume ﷺ akasema: 'Nimemuamini Allah na Mitume Wake; lau kama ningekuwa ni mwenye kumuua mjumbe, basi ningewaua nyinyi wawili.' Abdullah akasema: 'Hivyo basi, Sunnah ikapitika kuwa wajumbe hawauawi.'" (Imepokelewa na Ahmad na akaisahihisha Al-Haythami). Hadithi hii inafahamisha uharamu wa kuwaua wajumbe wanaokuja kutoka kwa makafiri, na mfano wa kuua ni adhabu nyinginezo zote. Isipokuwa jambo hili ni kwa yule ambaye sifa ya mjumbe (rasul) inamsadiki, kama vile balozi, kaimu balozi na wanaofanana nao. Ama yule ambaye sifa ya mjumbe haimfiti kama vile konsuli (qunsul) na mwakilishi wa kibiashara na mfano wao, basi hakuna kinga kwa mfano wa hao, kwa sababu sifa ya mjumbe haiwahusu.
Katika suala hili inarejewa kwenye desturi za kimataifa kwa sababu ni istilahi ambayo uhakiki wa uhalisia wake (tahqiq al-manat) unarejewa kwenye desturi, yaani kujua je, huyu anazingatiwa kuwa ni miongoni mwa wajumbe au la.] Mwisho wa nukuu kutoka kitabu cha Utangulizi wa Katiba.
Hivyo, kutofaa kutekeleza adhabu ya kifo na adhabu nyinginezo kunahusu balozi wa kudumu na balozi au mjumbe wa muda mradi tu uhalisia wa "mjumbe" unapatikana ndani yao. Kwa hiyo hakuna tofauti katika suala la kutotekelezwa kwa adhabu kati ya balozi wa kudumu na balozi wa muda, kwani wote wawili ni wajumbe na hukumu za mjumbe katika suala la adhabu zinawahusu.
Ama kuhusu sehemu ya mwisho ya swali lako: (Na ikiwa mmoja wa aina hizi mbili atafanya uhalifu au kitendo kisicho cha kisheria nje ya mamlaka yake kama balozi, je, atahukumiwa na kuadhibiwa kwa mujibu wa nchi ya Khilafah? Au balozi wa muda na balozi wa kudumu wanatendewa kwa namna tofauti katika suala hili?), hatukuchanganua kwa kina uhalisia wa adhabu ambazo zinaingia katika kinga na zile ambazo haziingii. Tutafanya hivyo katika kanuni za utendaji za ibara za katiba ambazo tumeanza kuzifanyia kazi, na tunamuomba Allah msaada katika kuzikamilisha kwa wakati unaofaa In Shaa Allah.
Natumai jibu hili linatosheleza, na Allah ndiye Mjuzi zaidi na Mwenye hikima zaidi.
Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
06 Safar 1445 H Malingana na 22/08/2023 M
Link ya jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir (Allah amuhifadhi) kwenye Facebook: https://www.facebook.com/HT.AtaabuAlrashtah/posts/849472483406789