Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: Zaka na Kukamilika kwa Mwaka (Hawl) - Kwa Heba Shaderma

February 02, 2015
3857

(Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni mtukufu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi")

Swali:

As-Salaam Alaykum, nina kiasi cha pesa kilichofikia Nisab na kimekaa kwa takriban mwaka mmoja. Wakati wakati wake wa kutoa Zaka ulipofika, nilihitaji pesa hizo kwa ajili ya mahitaji fulani na kikasalia kiasi kidogo tu.. Je, inanipasa kutoa Zaka kwa kiasi cha awali cha pesa kwa kuwa kimepita mwaka?

Jibu:

Wa Alaykumus-Salaam wa Rahmatullahi wa Barakaatuh.

Zaka haiwi wajibu kwenye mali mpaka ifikie Nisab na kupita mwaka mzima (Hawl) tangu kufikiwa kwa Nisab hiyo. Kutoka kwa Ali bin Abi Talib, kutoka kwa Mtume ﷺ amesema:

إِذَا كَانَتْ لَكَ مِئَتَا دِرْهَمٍ، وَحَالَ عَلَيْهَا الْحَوْلُ، فَفِيهَا خَمْسَةُ دَرَاهِمَ، وَلَيْسَ عَلَيْكَ شَيْءٌ - يَعْنِي فِي الذَّهَبِ - حَتَّى يَكُونَ ذَلِكَ عِشْرُونَ دِينَاراً، فَإِذَا كَانَتْ لَكَ عِشْرُونَ دِينَاراً، وَحَالَ عَلَيْهَا الْحَوْلُ، فَفِيهَا نِصْفُ دِينَارٍ

"Ikiwa una dirham mia mbili, na mwaka ukapita juu yake, basi ndani yake mna dirham tano, na huna jukumu la chochote - yaani katika dhahabu - mpaka iwe dinari ishirini. Basi ikiwa una dinari ishirini, na mwaka ukapita juu yake, basi ndani yake mna nusu dinari." (Imepokelewa na Abu Dawood)

Na kipimo ni mwaka wa Hijri si wa Miladi, yaani ikiwa yamepita siku 354 tangu kufikia Nisab, basi mwaka umetimia na Zaka imekuwa wajibu. Na mara tu Zaka inapokuwa wajibu kwenye mali ya Muislamu, haiondoki kwake.

Hivyo basi, ikiwa mali yako iliyofikia Nisab imepitikiwa na mwaka mzima kama tulivyoeleza, basi Zaka imekuwa wajibu juu yake. Kutumia mali hiyo au sehemu yake baada ya mwaka kutimia hakubatilishi wajibu huo; Zaka inabaki kuwa wajibu, na unapaswa kuitoa kwa kiasi chote cha pesa, iwe ni kile ulichokitumia au kilichobaki. Hii ni deni katika dhamana yako mpaka utakapoilipa, hivyo fanya haraka, Allah akurehemu, kuitoa.

Hii ni ikiwa ulichotumia ni baada ya mwaka kupita. Lakini ikiwa matumizi yalikuwa kabla ya mwaka kutimia, basi Zaka ni wajibu tu kwa kiasi kilichopo wakati wa kutimia kwa mwaka.

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

AF2

Link ya jibu kutoka kwa tovuti ya Amir

Link ya jibu kutoka ukurasa wa Amir wa Google Plus

Share Article

Share this article with your network