(Silsila ya Majibu ya Mwanachuoni Ata’ bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amiri wa Hizb ut-Tahrir, kwa Maswali ya Wafuasi wa Ukurasa Wake wa Facebook)
Jibu la Swali: Kuhusu Kuweka Muda Maalum wa Kumchagua Khalifah
Kwa Ahmad Nadhif
Swali:
Assalamualaykum warahmatullahi wa barakatuhu.
Yaa sheikh, i would like to ask you a question about the 3 days deadline of nashbul khalifah after the retirement of the previous imam. It is stated in the ajhizah book that this time-span is based on umar radhiyallahu anhu's order to kill any among the six sahabas if they reject the agreement of the others after 3 days. My question is that there are some people who state that this riwayat taken from tarikh thabari is categorized as dha 'if. What do you say about it? Baarakallaahu fiik wa jazaaka khayran jazaa
Jibu:
Wa alaikumus salam wa rahmatullahi wa barakatuh.
Mada ya Umar (ra) kuwapangia Maswahaba muda wa siku tatu kwa ajili ya kumchagua Khalifah... jambo hili lilifanyika mbele ya kundi kubwa la Maswahaba. Umar (ra) alimwambia Suhayb mbele ya umati wa Maswahaba:
«صَلِّ بِالنَّاسِ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ، وَأَدْخِلْ عَلِيًّا وَعُثْمَانَ وَالزُّبَيْرَ وَسَعْدًا وَعَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ عَوْفٍ وَطَلْحَةَ إِنْ قَدِمَ... وَقُمْ عَلَى رُءُوسِهِمْ، فَإِنِ اجْتَمَعَ خَمْسَةٌ وَرَضُوا رَجُلًا وَأَبَى وَاحِدٌ فَاشْدَخْ رَأْسَهُ أَوِ اضْرِبْ رَأْسَهُ بِالسَّيْفِ...»
"Waswalishe watu kwa siku tatu, na uwaingize (katika mashauriano) Ali, Uthman, Az-Zubayr, Sa'd, Abdurrahman bin Awf, na Talha ikiwa atafika... na simama juu ya vichwa vyao (wasimamie), kisha ikiwa watano watakubaliana na kumridhia mtu mmoja na mmoja akakataa, basi mpasue kichwa chake au mpige kichwa chake kwa upanga..."
Hayo yamepokewa na Ibn Shabba katika Tarikh al-Madinah, na Al-Tabari katika Tarikh yake, na Ibn Sa'd amepokea mfano wake katika Al-Tabaqat al-Kubra. Pamoja na kwamba watu hao walikuwa miongoni mwa watu wa Shura na miongoni mwa Maswahaba wakubwa, tukio hilo lilifanyika mbele ya macho na masikio ya Maswahaba, na hakuna yeyote aliyepokewa kupingana nalo au kulikataa. Kwa hivyo, huo ulikuwa ni Ijma’ (mwafaka) wa Maswahaba kwamba haijuzu kwa Waislamu kukaa bila Khalifah kwa zaidi ya siku tatu na masiku yake.
Ijma’ wa Maswahaba ni dalili ya kisheria kama ilivyo Kitabu (Qur'ani) na Sunnah. Kwa sababu hiyo, Waislamu hawapewi muhula katika kumchagua Khalifah baada ya Khalifah aliyetangulia ikiwa nafasi hiyo itakuwa wazi isipokuwa siku tatu pekee, isipokuwa ikiwa wamezuiwa na mambo ya lazima (ya nguvu) ambayo hawana uwezo wa kuyaepuka. Katika hali hiyo, dhambi huondoka kwao kwa sababu ya kushughulishwa kwao na kusimamisha faradhi, na kwa kulazimishwa kwao kuchelewa kutokana na yale yaliyowashinda nguvu. Ibn Hibban na Ibn Majah wamepokea kutoka kwa Ibn Abbas amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«إن الله وضع عن أمتي الخطأ، والنسيان، وما استُكْرِهوا عليه»
"Hakika Mwenyezi Mungu ameusamehe umma wangu makosa (yasiyokusudiwa), kusahau, na yale wanayolazimishwa (kwa nguvu) kuyafanya." (Ibn Majah [2043])
Na ikiwa hawajashughulishwa na hilo, basi watapata dhambi wote mpaka asimame Khalifah, na hapo ndipo faradhi itawaondokea. Ama dhambi waliyoipata kwa kukaa kwao bila kusimamisha Khalifah, hiyo haiondoki kwao, bali inabaki juu yao ambapo Mwenyezi Mungu atawahasibu kwayo, kama anavyowahasibu kwa maasi yoyote anayoyafanya Muislamu kwa kuacha kutekeleza faradhi.
Ndugu yenu, Ata’ bin Khalil Abu Al-Rashtah
Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amiri kwenye Facebook
Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amiri
Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amiri kwenye Google Plus