** (Silsila ya majibu ya mwanachuoni Ata bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wageni wa ukurasa wake wa Facebook "Feqhi")**
Jibu la Swali
Ubainifu wa Dhana ya Fitna
Kwa Nbiha Essam
Swali:
Bwana wangu, mbele ya kauli yenu "Je, hakuna miongoni mwenu mtu mwongofu atakayewaangamiza hao ruwaibidhah, na kurejesha mwenendo wa Ansar, akatunusuru kwa ajili ya kusimamisha hukumu ya Uislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume...?" nataka kuashiria hadithi ya Mtume ambapo Mtume (saw) anasema: «Ikiwa mtawaona watu ahadi zao zimeharibika, na amana zao zimepungua, na wakawa hivi» akashikanisha vidole vyake, (mpokeaji) akasema: Nikamwendea na kusema: Nifanye nini wakati huo, Mwenyezi Mungu anifanye fidia yako? Akasema: «Lazimiana na nyumba yako, na umiliki ulimi wako, na chukua unachokijua, na acha unachokikataa, na lazimiana na jambo la nafsi yako, na achana na mambo ya watu wote».
Inaonekana kuna mgongano kati ya yale aliyoamrisha Mtume na yale mnayolingania kwetu, Mwenyezi Mungu akubariki.
Jibu:
(Hadithi uliyoitaja imepokelewa kwa ukamilifu wake na Abu Dawood katika Sunan yake kama ifuatavyo:
"Haddathana Harun bin Abdullah, haddathana al-Fadl bin Dukain, haddathana Yunus bin Abi Ishaq, 'an Hilal bin Khabbab Abi al-'Ala', qala: haddathani 'Ikrimah, haddathani Abdullah bin 'Amr bin al-'Aas, qala: Wakati tukiwa pembeni ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), mara akataja fitna, akasema:
إِذَا رَأَيْتُمُ النَّاسَ قَدْ مَرِجَتْ عُهُودُهُمْ، وَخَفَّتْ أَمَانَاتُهُمْ، وَكَانُوا هَكَذَا
«Ikiwa mtawaona watu ahadi zao zimeharibika, na amana zao zimepungua, na wakawa hivi» na akashikanisha vidole vyake. (Mpokeaji) akasema: Nikamwendea na kusema: Nifanye nini wakati huo, Mwenyezi Mungu anifanye fidia yako? Akasema:
الْزَمْ بَيْتَكَ، وَامْلِكْ عَلَيْكَ لِسَانَكَ، وَخُذْ بِمَا تَعْرِفُ، وَدَعْ مَا تُنْكِرُ، وَعَلَيْكَ بِأَمْرِ خَاصَّةِ نَفْسِكَ، وَدَعْ عَنْكَ أَمْرَ الْعَامَّةِ
«Lazimiana na nyumba yako, na umiliki ulimi wako, na chukua unachokijua, na acha unachokikataa, na lazimiana na jambo la nafsi yako, na achana na mambo ya watu wote»") Mwisho.
Hadithi hii na nyinginezo miongoni mwa hadithi za fitna tofauti zimekuja katika hali ya kuchanganyika haki na batili kiasi kwamba haki haijulikani... Yule ambaye jambo linamchanganya, basi hukumu ya kisheria kwake ni kulazimiana na nyumba yake mpaka haki ibainike kutoka kwa batili, na hapo ndipo anapopaswa kuifuata haki.
Anayetafakari yaliyomo katika hadithi hii kwa maana na muundo wake, jambo hili linambainikia wazi... Angalia neno (wakawa hivi) na ubainifu wa mpokeaji juu ya kile kilichoashiriwa kwa kusema (na akashikanisha vidole vyake), yaani alichanganya vidole vya mikono yake miwili, ikiaashiria kuchanganyika kwa baadhi yao na wengine na kutatanika kwa mambo kwao... Na yote haya yanaonyesha kutatanika kwa haki na batili na kutopambanuka kwake, hivyo katika hali hii kama tulivyosema hapo awali, hukumu ya kisheria kwake ni kukaa... mpaka haki ibainike kutoka kwa batili na hapo ndipo anapopaswa kuifuata haki.
Hakika kusimama na haki, iwe ni kuamrisha mema au kukataza maovu, au kunusuru aliyedhulumiwa, au kufanya kazi kwa bidii kutafuta nusuu (nusrah) kutoka kwa watu wenye nguvu ili kusimamisha Dola ya Kiislamu wakati haipo... ni jambo ambalo dalili za kisheria zinaliwajibisha, ikiwemo:
1- Katika Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu, miongoni mwazo:
- Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
وَلْتَكُنْ مِنْكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ
"Na uwe kutokana nanyi umma unaolingania kheri na unaoamrisha mema na unakataza maovu; na hao ndio waliofanikiwa." (QS. Ali 'Imran [3]: 104)
- Na akasema:
كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَر
"Nyinyi mmekuwa bora ya umma waliofanyiwa watu (waliojitokeza mbele ya watu); mnaamrisha mema na mnakataza maovu." (QS. Ali 'Imran [3]: 110)
- Ameitoa Ahmad kutoka kwa Abdullah bin Amr: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema: «Ikiwa mtauona umma wangu unaogopa kumwambia dhalimu: Hakika wewe ni dhalimu, basi wameachwa (hawana heri)». Na akaitoa Abu Dawood, akasema Abu Bakr: Baada ya kumhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu: Sisi tulimsikia Mtume (saw) akisema: «Hakika watu wanapomwona dhalimu na wasimshike mikono yake (wasimzuie), Mwenyezi Mungu anakaribia kuwaenea wote kwa adhabu». Na akaitoa At-Tirmidhi kutoka kwa Hudhayfah (ra) kutoka kwa Mtume (saw) akasema: «Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, lazima mtaamrisha mema na lazima mtakataza maovu, au Mwenyezi Mungu anakaribia kuwaletea adhabu kutoka Kwake kisha mtamwomba na hamtajibiwa». Na akaitoa At-Tirmidhi na Abu Dawood pia kutoka kwa Ibn Mas’ud (ra) akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «Hasha, naapa kwa Mwenyezi Mungu, lazima mtaamrisha mema, na lazima mtakataza maovu, na lazima mtamshika dhalimu mikononi mwake, na lazima mtaufanya urudi kwenye haki, na mtaufunga kwenye haki, au Mwenyezi Mungu atazipiga nyoyo za baadhi yenu kwa wengine, kisha atawalaani kama alivyowalaani wao». Na akaitoa Abu Dawood na At-Tirmidhi kutoka kwa Abu Said al-Khudri (ra) kutoka kwa Mtume (saw) amesema: «Jihadi bora zaidi ni neno la haki mbele ya mtawala dhalimu». Na kwa An-Nasa’i kutoka kwa Abi Abdillah Tariq bin Shihab al-Bajali al-Ahmasi (ra): Kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume (saw) naye ameweka mguu wake kwenye kanyagio (la farasi): Ni Jihadi gani bora zaidi? Akasema: «Neno la haki mbele ya mtawala dhalimu».
2- Katika kunusuru aliyedhulumiwa, miongoni mwazo:
- Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ
"Lakini wakiomba msaada kwenu katika (mambo ya) dini, basi ni juu yenu kuwasaidia." (QS. Al-Anfal [8]: 72)
- Ameitoa Al-Bukhari katika Sahih yake kutoka kwa Abdullah bin Umar (ra) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «Muislamu ni ndugu wa Muislamu, hamdhulumu wala hamtoi (kumkabidhi kwa adui)... Na anayemuondolea Muislamu tatizo, Mwenyezi Mungu atamuondolea tatizo miongoni mwa matatizo ya Siku ya Kiyama». Na akaitoa pia kutoka kwa Anas (ra), amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «Mnusuru ndugu yako dhalimu au aliyedhulumiwa» wakasema: Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu, huyu aliyedhulumiwa tunamnusuru, lakini tutamnusuru vipi akiwa dhalimu? Akasema: «Unamshika mikono yake (kumzuia)». Na pia akaitoa kutoka kwa Al-Bara bin Azib (ra) amesema: «Mtume (saw) alituamrisha mambo saba... na kunusuru aliyedhulumiwa».
3- Kisha katika kutafuta nusuu (nusrah) kutoka kwa watu wenye nguvu ili kusimamisha Dola ya Kiislamu ikiwa haipo, miongoni mwazo:
Ameitoa Ibn Hisham katika As-Sirah akasema: "Amesema Ibn Ishaq: ... Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alikuwa akijitokeza katika misimu ya Hijja, inapokuwa, kwa makabila ya Kiarabu akiwalingania kwa Mwenyezi Mungu, na kuwataarifu kuwa yeye ni Mtume aliyetumwa, na kuwaomba wamsadiki na wamlinde mpaka awabainishie yale aliyotumwa nayo na Mwenyezi Mungu." Mwisho.
Na akaitoa Abu al-Fath, Fathuddin katika Uyun al-Athar akasema: "Na akataja Qasim bin Thabit... kutoka kwa Ali bin Abi Talib katika kutoka kwao yeye na Abu Bakr pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)... Abu Bakr akasema: Watu hawa ni wakina nani? Wakasema: Kutoka kwa Shayban bin Tha’laba. Abu Bakr akamgeukia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema: Baba na mama yangu wawe fidia kwako, hawa ni viongozi katika watu wao, na miongoni mwao ni Mafruq bin Amr, Hani’ bin Qabisah, Muthanna bin Harithah, na Nu’man bin Sharik... Abu Bakr akasema:
Je, imekufikieni kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu basi huyu hapa, Mafruq akasema: Imetufikia kwamba anataja hilo, unalingania nini ee ndugu wa Kikuraishi? Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasogea mbele na kusema: «Nalingania kwenye ushahidi wa kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke Yake hana mshirika, na kwamba mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kwamba mnihifadhi na mninusuru... Hani’ akasema... na akaonekana akipenda kumshirikisha katika mazungumzo Muthanna bin Harithah, akasema: Na huyu Muthanna bin Harithah ni mzee wetu na kiongozi wetu wa vita, Muthanna akasema: Nimeshasikia maneno yako ee ndugu wa Kikuraishi... Na sisi tumepiga kambi kati ya mito miwili ya Yamamah na Samamah, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema: «Ni ipi hiyo mito miwili» akasema: Mito ya Kisra (Uajemi) na maji ya Waarabu... Na sisi tumepiga kambi kwa makubaliano aliyotuchukulia Kisra kwamba tusizushe jambo jipya wala tusiwahifadhi wazushi... Basi ukipenda tukuhifadhi na kukunusuru kwa upande wa maji ya Waarabu tutafanya hivyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema: «Hamjafanya vibaya katika majibu kwani mmesema kweli, na hakika dini ya Mwenyezi Mungu hatainusuru isipokuwa yule anayeihami kutoka pande zake zote..." Mwisho.
Na hivi ndivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyokuwa akitafuta nusuu kutoka kwa watu wenye nguvu katika makabila ili wasilimu na wanusuru (saw) kusimamisha hukumu ya Mwenyezi Mungu miongoni mwao, lakini hawakumuitikia mpaka alipotaka Mwenyezi Mungu... Basi Mtume (saw) akamtuma Mus’ab kwenda Madina, na Ansar wakaitikia na wakampa baia Mtume (saw) katika Baia ya العقبة (Aqaba) ya pili, kisha Mtume (saw) akahamia Madina na akasimamisha Dola huko...
Ibn Hisham alitaja katika As-Sirah akasema: (Amesema Ibn Ishaq: Kisha Mus’ab bin Umair alirudi Makka, na wakatoka waliotoka katika Ansar miongoni mwa Waislamu kwenda kwenye msimu wa Hijja pamoja na mahujaji wa watu wao miongoni mwa washirikina, mpaka walipofika Makka, wakapeana ahadi na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kule Aqaba, katikati ya masiku ya Tashriq, wakati Mwenyezi Mungu alipotaka kuwatunuku heshima Yake, na ushindi kwa Mtume Wake, na kuutukuza Uislamu na watu wake, na kuudhalilisha ushirikina na watu wake... akasema: Tukatoka tukiulizia kuhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)... akasema: Tukaingia Msikitini tukamkuta Abbas ameketi, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ameketi naye, tukasalimia kisha tukaketi naye... Ka’ab akasema: Kisha tukatoka kwenda Hijja, na tukapeana ahadi na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kule Aqaba katikati ya masiku ya Tashriq. Akasema: Tulipomaliza Hijja, na ikawa ni usiku ule tuliowekeana ahadi na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)... akasema: Tukalala usiku ule na watu wetu katika mahema yetu, mpaka ulipopita thuluthi ya usiku tukatoka kwenye mahema yetu kuelekea sehemu ya ahadi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), tukijipenyeza kama wanavyojipenyeza ndege wa qata kwa siri, mpaka tukakusanyika kwenye bonde karibu na Aqaba, na tulikuwa wanaume sabini na watatu, na tukiwa na wanawake wawili miongoni mwa wanawake wetu: Nusaybah binti Ka’ab, Mama wa Umarah... na Asmaa binti Amr bin Adiyy...
Akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akazungumza, akasoma Qur’an, akalingania kwa Mwenyezi Mungu, akahimiza Uislamu, kisha akasema: Nawapa baia kwa sharti la kunilinda na yale mnavyowalinda kwayo wanawake wenu na watoto wenu. Akasema: Al-Bara bin Ma’rur akamshika mkono wake, kisha akasema: Ndiyo, naapa kwa Yule aliyekutuma kwa haki (kama Mtume), tutakulinda na yale tunayolinda kwayo nguo zetu (miili yetu), basi tupe baia ee Mtume wa Mwenyezi Mungu, sisi wallahi ni watoto wa vita, na watu wa silaha, tumeirithi kizazi baada ya kizazi... Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema: ... Mimi ni miongoni mwenu na nyinyi ni miongoni mwangu, napigana na mliopigana nao, na nina amani na mliokuwa na amani nao...
Wakasema: ... Tutapata nini ee Mtume wa Mwenyezi Mungu ikiwa tutatekeleza (hayo)? Akasema: Pepo. Wakasema: Kunjua mkono wako, akaukunjua mkono wake wakampa baia.
Akasema: Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema: Tawanyikeni kuelekea kwenye mahema yenu. Abbas bin Ubadah bin Nadlah akamwambia: Wallahi kwa Yule aliyekutuma kwa haki: Ukipenda tutawaangukia watu wa Mina kesho kwa panga zetu? Akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema: Hatukuamrishwa hayo, lakini rudini kwenye mahema yenu...)
Na ameitoa Al-Bayhaqi katika Dala’il an-Nubuwwah akasema: (Alituhabarisha Al-Hasan bin Muhammad bin Ishaq... kutoka kwa Jabir bin Abdullah al-Ansari... akasema: Mtume akatuahidi bonde la Aqaba tukakusanyika huko mmoja mmoja na wawili wawili, mpaka tulipokamilika kwake tukasema: Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tunakupa baia juu ya nini? Akasema: Nipeni baia juu ya kusikia na kutii katika hali ya uchangamfu na uvivu, na juu ya kutoa katika hali ya dhiki na wasaa, na juu ya kuamrisha mema na kukataza maovu, na juu ya kusema kuhusu Mwenyezi Mungu pasina kuwaogopa walaumao, na juu ya kuninusuru nitakapofika kwenu Yathrib, mnilinde na yale mnavyojilinda kwayo nafsi zenu, wake zenu na watoto wenu, na mtapata Pepo... Tukamuinukia tukimpa baia mtu mmoja mmoja, akituchukulia sharti lake, na akitupa kwa ajili hiyo Pepo...) Mwisho.
Na dalili hizi zote, na nyinginezo kama hizo, zinawajibisha kutokaa nyumbani, bali ni katika hali tu ya fitna wakati mtu hajui haki kutoka kwa batili. Ikiwa anaijua, basi wajibu kwake ni kusema haki, akaamrisha mema na kukataza maovu, na kunusuru aliyedhulumiwa, na kutafuta nusuu kutoka kwa watu wenye nguvu ili kusimamisha Dola ya Kiislamu "Khilafah Rashida" kwa njia ya kisheria, ikiwa Khilafah haipo, basi hili ni jambo la wajibu, na katika kukaa nyumbani bila kulitekeleza kuna madhambi makubwa. Na kama Waislamu wangekaa, hususan watu wema, wakaacha kunusuru haki iliyo dhahiri na inayojulikana na wakalazimiana na nyumba zao, basi uharibifu ungedhihirika, na watu wadhalimu na wabatilifu wangetamalaki na kuwatawala waja, mbali na kwamba kukaa nyumbani katika hali hii kunapingana na nusuu za kisheria zinazowajibisha kunusuru haki kama tulivyobainisha hapo juu...
Hii ndiyo maana ya hadithi tukufu uliyoulizia, yaani ni katika fitna wakati haki haijapambanuliwa na batili... Basi wapi jambo hili ee muulizaji karimu kutokana na kauli yetu: (Sisi tunaelekea kwenye majeshi ya Waislamu: Je, hakuna miongoni mwenu mtu mwongofu atakayewapinga watawala kwa usaliti wao kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na waumini...? Je, hakuna miongoni mwenu mtu mwongofu anayeonea wivu dini yake na heshima yake akasimama mbele ya maadui wa Mwenyezi Mungu akizikata kamba zao na fimbo zao...? Je, hakuna miongoni mwenu mtu mwongofu atakayewaangamiza hao ruwaibidhah, na kurejesha mwenendo wa Ansar, akatunusuru kwa ajili ya kusimamisha hukumu ya Uislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume...?) Mwisho. Kwani haki ndani yake iko wazi na imebainika, na ni wito wa kunusuru dini ya Mwenyezi Mungu na kusimamisha hukumu ya Mwenyezi Mungu, na kukata mizizi ya makafiri, na kupinga wasaliti wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na waumini... Basi si wito wa kuelekea kwenye fitna, wala ushiriki katika fitna, bali ni wito wa haki iliyo wazi, ambao watu wawili hawatofautiani juu yake wala mbuzi wawili hawagongani vichwa kwa ajili yake, basi wapi kupingana kwake na hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)...! Je, wito wa Waislamu wa kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume Wake (saw), na kuwazuia madhalimu na makafiri, na kuitikia nusuu ya dini unaweza kuwa unapingana na yale yaliyokuja katika hadithi ya Mtume (saw)?!
Basi litafakari jambo hili Mwenyezi Mungu akurehemu... Mwenyezi Mungu atutuze sote kwa utukufu wa Uislamu na Waislamu.
Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah
Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir
Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Google Plus