Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: Hukumu ya Kushiriki katika Kuangalia Chaguzi za Kidemokrasia

February 15, 2021
3505

Mfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa Maswali ya Wafuasi wa Ukurasa Wake wa Facebook "Fiqhi"

Kwa Hisham Banibaker

Swali:

Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,

Nataka kuuliza kuhusu hukumu ya kushiriki katika kuangalia (muraqabah) chaguzi za bunge pamoja na dalili, Allah akubariki.

Ufafanuzi wa swali: Asili ya kazi hiyo haina uhusiano na upigaji kura au mambo ya maandalizi ya uchaguzi, asili ya kazi hiyo ni habari na takwimu kuhusu uchaguzi.

Jibu:

Wa Alaikum Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh,

Hakika wewe unajua kwamba chaguzi za bunge zinazofanyika sasa hivi hazijuzu kisharia kwa sababu, kulingana na mifumo iliyopo, iwe ni ya rais au ya bunge, ni chaguzi za utungaji sheria (tashri'i) kwa ajili ya dola isiyohukumu kwa Sheria ya Allah... na kwa ajili hiyo, kushiriki ndani yake, au kusaidia katika utekelezaji wake, au kuifanyia propaganda kwa ajili ya kuhimiza watu kuishiriki, au kuiunga mkono na mfano wa hayo, haijuzu.

Ama ikiwa kazi yako haina uhusiano na mambo haya (kushiriki, utekelezaji, kuhimiza, na kuunga mkono), kama ulivyotaja katika swali lako yaani (takwimu za kura) – na ninarudia: bila ya mambo haya manne (kushiriki, utekelezaji, kuhimiza, au kuunga mkono) – bali tu kama upande wa kimahesabu, yaani "kuhesabu idadi ya kura", basi sioni kuwa imeingia katika uharamu. Lakini swali hapa ni: Je, unahakikisha kuwa kazi hiyo ya kimahesabu haitachanganyika na lolote katika mambo hayo manne? Vyovyote iwavyo, ikiwa utahakikisha hilo, basi haijumuishwi katika uharamu... Lakini ni bora zaidi (al-awla) kutoifanya ili isitumiwe na watu wa mifumo hii katika kuonyesha wingi wa wafanyakazi wanaojishughulisha na kazi za uchaguzi. Kwani Maswahaba wa Mtume ﷺ walikuwa wakijiepusha na milango kadhaa ya mambo ya halali (mubah) kwa hofu ya kukaribia haramu. Imethibiti kutoka kwa Mtume wa Allah ﷺ kwamba alisema:

لَا يَبْلُغُ العَبْدُ أَنْ يَكُونَ مِنَ المُتَّقِينَ حَتَّى يَدَعَ مَا لَا بَأْسَ بِهِ حَذَراً لِمَا بِهِ البَأْسُ

"Mja hafikii kuwa miongoni mwa wacha-Mungu (Muttaqin) mpaka aache kile kisicho na neno (halali) kwa kuhofia kile chenye neno (haramu)." (Imepokelewa na At-Tirmidhi na akasema: Hii ni hadith Hasan).

Hili ndilo ninaloliona katika suala hili, na Allah ni Mjuzi zaidi na Mwenye Hekima zaidi.

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah

30 Jumada al-Akhirah 1442 H Sawia na 12/02/2021 M

Kiungo cha jibu kutoka kwa ukurasa wa Amir (Allah amhifadhi) kwenye Facebook

Kiungo cha jibu kutoka kwa tovuti ya Amir (Allah amhifadhi) Web

Share Article

Share this article with your network