Mfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut Tahrir, kwa Maswali ya Watembeleaji wa Ukurasa Wake wa Facebook "Fiqhi"
Jibu la Swali
Hukumu ya Chanjo Inayojumuisha Vitu Vilivyoharamishwa
Kwa Mohammad Abdul Basir
Swali:
As Salamu Alaykum Our Ameer and Sheikh
May Allah (swt) protect you and this noble party and grant the victory through your hands and bless this Ummah with the second Khilafah Rashida on the method of Prophethood. Ameen.
My question is, in the United Kingdom the government gives our children a flu vaccination for the winter period each year so children do not get the flu. This is a precautionary matter and parents are allowed to opt out and not give the flu vaccine to their children. From what I have been informed, the vaccine contains gelatine from pork, which they say has been purified and the vaccine is in the form of a nasal spray.
Is it permitted for children or adults to take precautionary vaccines and medicines which contain haram ingredients like pork, alcohol etc?
May Allah (swt) keep you in the best of health and reward you abundantly for your answer,
Wa alaykumus Salam wa rahmatullahi wa barakatuhu
Your brother in Islam Abdul Basir
Tafsiri ya Swali:
Assalamu Alaykum Amir wetu na Sheikh wetu,
Namuomba Mwenyezi Mungu akulinde wewe pamoja na chama hiki kitukufu na ajaalie ushindi upatikane kupitia mikono yako, na aikimu Umma huu kwa Khilafah ya Rashidah ya pili kwa njia ya Utume, Amin.
Swali langu ni: Katika nchi ya Uingereza, serikali huwapa watoto wetu chanjo dhidi ya mafua katika kipindi cha msimu wa baridi kila mwaka ili wasipatwe na mafua. Hili ni suala la kinga na wazazi wanaruhusiwa kuchagua kutowapa watoto wao chanjo hiyo. Kutokana na nilivyofahamishwa, chanjo hiyo ina jeli (gelatine) itokanayo na nguruwe, na wanasema kuwa imesafishwa, na chanjo hiyo ipo katika mfumo wa dawa ya kupulizia puani (nasal spray).
Je, inaruhusiwa kwa watoto au watu wazima kuchukua chanjo kama kinga, na pia dawa zenye viambata vilivyoharamishwa kama vile nguruwe na pombe... n.k?
Namudu kuomba Mwenyezi Mungu akuhifadhi katika afya bora na akujazi kheri nyingi kwa jibu lako.
Wassalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Ndugu yako katika Uislamu, Abdul Basir
Jibu:
Wa Alaykumus Salam Warahmatullahi Wabarakatuh,
Kwanza, Mwenyezi Mungu akubariki kwa dua yako njema kwetu, na sisi tunakuombea dua iliyo bora zaidi kuliko hiyo...
Unauliza kuhusu hukumu ya kisheria ya chanjo ambayo viambata vyake vina vitu vilivyoharamishwa, na pia unauliza kuhusu kujitibu kwa dawa zenye vitu vilivyoharamishwa... Tayari tulishajibu kuhusu hukumu ya chanjo, na pia tulijibu hukumu ya kujitibu kwa kitu kilichoharamishwa na najisi. Kutokana na majumuisho ya majibu haya, ndipo linapatikana jibu la swali lako la sasa, na nitakunukulia sehemu ya yale tuliyoyajibu:
Kwanza: Jibu la swali la tarehe 18/11/2013M kuhusu chanjo na hukumu yake, ambapo ilitajwa hivi:
[Chanjo ni dawa, na kujitibu ni jambo linalopendekezwa (mandub) na si faradhi, na dalili ya hilo ni:
1- Bukhari amepokea kutoka kwa Abu Hurairah amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema:
مَا أَنْزَلَ اللَّهُ دَاءً إِلَّا أَنْزَلَ لَهُ شِفَاءً
"Mwenyezi Mungu hakuteremsha ugonjwa isipokuwa ameteremsha na dawa yake."
Na Muslim amepokea kutoka kwa Jabir bin Abdullah, kutoka kwa Mtume ﷺ amesema:
لِكُلِّ دَاءٍ دَوَاءٌ، فَإِذَا أُصِيبَ دَوَاءُ الدَّاءِ بَرَأَ بِإِذْنِ اللهِ عَزَّ وَجَلَّ
"Kwa kila ugonjwa kuna dawa, na ikipatikana dawa ya ugonjwa, basi hupona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Aliyeshinda na Atukukaye." Na Ahmad amepokea katika Musnad yake kutoka kwa Abdullah bin Mas'ud:
مَا أَنْزَلَ اللَّهُ دَاءً، إِلَّا قَدْ أَنْزَلَ لَهُ شِفَاءً، عَلِمَهُ مَنْ عَلِمَهُ، وَجَهِلَهُ مَنْ جَهِلَهُ
"Mwenyezi Mungu hakuteremsha ugonjwa isipokuwa ameteremsha na dawa yake; anayeijua anaijua, na asiyeijua haijui."
Hadithi hizi zina mwongozo kuwa kwa kila ugonjwa kuna dawa inayoutibu, ili iwe ni kichocheo cha kufanya juhudi ya kupata matibabu yanayopelekea kupona ugonjwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Subhanahu, na huu ni mwongozo (irshad) na si uwajibu.
2- Ahmad amepokea kutoka kwa Anas amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema:
إِنَّ اللَّهَ حَيْثُ خَلَقَ الدَّاءَ، خَلَقَ الدَّوَاءَ، فَتَدَاوَوْا
"Hakika Mwenyezi Mungu kila alipoumbia ugonjwa, aliumbia dawa, basi jitibuni." Na Abu Dawood amepokea kutoka kwa Usamah bin Sharik, amesema: Nilimjia Mtume ﷺ na maswahaba zake kama kwamba juu ya vichwa vyao kuna ndege, nikasalimia kisha nikaketi. Wakaja mabedui kutoka huku na huku, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je, tujitibu? Akasema:
تَدَاوَوْا فَإِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ لَمْ يَضَعْ دَاءً إِلَّا وَضَعَ لَهُ دَوَاءً، غَيْرَ دَاءٍ وَاحِدٍ الْهَرَمُ
"Jitibuni, kwani Mwenyezi Mungu (swt) hakuweka ugonjwa isipokuwa ameweka na dawa yake, isipokuwa ugonjwa mmoja; uzee (yaani kifo)."
Katika hadithi ya kwanza kuna amri ya kujitibu, na katika hadithi hii kuna jibu kwa mabedui kuhusu kujitibu, na kutoa wito kwa waja wajitibu, kwani Mwenyezi Mungu hakuweka ugonjwa isipokuwa ameweka na uponyaji wake. Maelekezo katika hadithi hizi mbili yamekuja kwa muundo wa amri, na amri inafahamisha takaba ya jumla (mutlaq al-talab), na haifahamishi uwajibu isipokuwa ikiwa ni amri yenye mkazo (jazim). Mkazo unahitaji kielelezo (qarina) kinachofahamisha hilo, na hakuna kielelezo chochote katika hadithi hizi mbili kinachofahamisha uwajibu. Isitoshe, zimekuja hadithi zinazofahamisha kuruhusiwa kwa kuacha kujitibu, jambo ambalo linaondoa dhana ya uwajibu katika hadithi hizi mbili. Muslim amepokea kutoka kwa Imran bin Husain kwamba Mtume ﷺ amesema:
يَدْخُلُ الْجَنَّةَ مِنْ أُمَّتِي سَبْعُونَ أَلْفاً بِغَيْرِ حِسَابٍ
"Wataingia Peponi kutoka katika Umma wangu watu sabini elfu bila hesabu." Wakasema: Ni kina nani ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni wale ambao hawajitibui kwa chuma cha moto (lā yaktawūna) wala hawapi hirizi/ruqya (lā yastarquna), na kwa Mola wao wanatawakali." Na matumizi ya chuma cha moto (kayi) na ruqya ni miongoni mwa matibabu. Na Bukhari amepokea kutoka kwa Ibn Abbas: amesema: ... Huyu mwanamke mweusi, alimjia Mtume ﷺ akasema: Mimi nina kifafa na mimi huwa ninakashifika (nguo zangu hufunuka), basi niombee kwa Mwenyezi Mungu. Mtume akasema:
إِنْ شِئْتِ صَبَرْتِ وَلَكِ الجَنَّةُ، وَإِنْ شِئْتِ دَعَوْتُ اللَّهَ أَنْ يُعَافِيَكِ
"Ukipenda subiri na utapata Pepo, na ukipenda nitakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuponye." Akasema: Nitavumilia. Kisha akasema: Mimi huwa ninakashifika, basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisikashifike, naye Mtume akamuombea... Hadithi hizi mbili zinafahamisha kuruhusiwa kuacha kujitibu.
Yote hayo yanafahamisha kuwa amri iliyokuja ya "jitibuni" haimaanishi uwajibu, na hivyo amri hapa ni ya kuruhusiwa (ibaha) au kupendelewa (ndub). Na kutokana na ukali wa himaya ya Mtume ﷺ katika kujitibu, basi amri ya kujitibu iliyokuja katika hadithi ni ya kupendekezwa (ndub).
Kwa mujibu wa hapo, chanjo hukumu yake ni kupendekezwa (ndub), kwa sababu chanjo ni dawa, na kujitibu ni jambo lililopendekezwa. Isipokuwa ikithibitika kuwa aina fulani ya chanjo ina madhara, kama vile viambata vyake kuwa vimeharibika au vina madhara kwa sababu fulani... basi chanjo katika hali hii na kwa viambata hivyo itakuwa haramu kwa mujibu wa kanuni ya madhara kutokana na hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliyoitoa Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa Ibn Abbas, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema:
لَا ضَرَرَ وَلَا ضِرَارَ
"Hakuna kudhuru wala kudhurika." Isipokuwa hizi ni hali chache sana...
Ama katika Dola ya Khilafah, kutakuwa na chanjo dhidi ya magonjwa yanayohitaji hilo kama vile magonjwa ya kuambukiza na mfano wake, na dawa itakuwa safi kutokana na kila aina ya uchafu. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ndiye mponyaji:
وَإِذَا مَرِضْتُ فَهُوَ يَشْفِينِ
"Na ninapougua Yeye ndiye anayeniponya." (QS. Ash-Shu'ara [26]: 80)
Inajulikana kisheria kuwa utunzaji wa afya ni miongoni mwa majukumu ya Khalifa kutokana na mlango wa kusimamia mambo kwa mujibu wa kauli ya Mtume ﷺ:
الإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ
"Imamu ni msimamizi na anawajibika kwa raia wake." (Bukhari kutoka kwa Abdullah bin Umar). Hii ni nukuu ya jumla kuhusu jukumu la dola juu ya afya na matibabu kwa kuwa vinajumuishwa katika usimamizi wa mambo wa lazima kwa dola.
Na kuna dalili maalum kuhusu afya na matibabu: Muslim amepokea kutoka kwa Jabir amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alimtumia Ubay bin Ka'ab tabibu, naye akamkata mshipa mmoja kisha akampiga chuma cha moto (kayi). Na Al-Hakim ametoa katika Al-Mustadrak kutoka kwa Zaid bin Aslam, kutoka kwa baba yake amesema: Niliumwa sana katika zama za Umar bin Al-Khattab, basi Umar akaniitia tabibu, naye akaniwekea masharti makali ya chakula hadi nikawa ninanyonya kokwa ya tende kwa sababu ya ukali wa masharti hayo.
Mtume ﷺ kwa sifa yake ya kuwa mtawala alimtumia tabibu Ubay, na Umar (ra) ambaye ni Khalifa wa pili muongofu aliita tabibu kwa ajili ya Aslam ili amtibu. Hizi ni dalili mbili kuwa afya na matibabu ni miongoni mwa mahitaji ya kimsingi ya raia ambayo dola lazima iyatoe bure kwa anayeihitaji miongoni mwa raia.] Mwisho.
Pili: Jibu la swali la tarehe 26/01/2011M kuhusu kunufaika na kilichoharamishwa na najisi na kujitibu navyo, ambapo ilitajwa hivi:
[... 2- Kunufaika na najisi na kilichoharamishwa ni haramu, na miongoni mwa dalili za hilo ni:
- Bukhari ametoa kutoka kwa Jabir bin Abdullah (ra) kwamba alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akisema mwaka wa kukombolewa Makka akiwa Makka:
إِنَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ حَرَّمَ بَيْعَ الْخَمْرِ وَالْمَيْتَةِ وَالْخِنْزِيرِ وَالْأَصْنَامِ فَقِيلَ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَرَأَيْتَ شُحُومَ الْمَيْتَةِ فَإِنَّهَا يُطْلَى بِهَا السُّفُنُ وَيُدْهَنُ بِهَا الْجُلُودُ وَيَسْتَصْبِحُ بِهَا النَّاسُ فَقَالَ لَا هُوَ حَرَامٌ ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ عِنْدَ ذَلِكَ قَاتَلَ اللَّهُ الْيَهُودَ إِنَّ اللَّهَ لَمَّا حَرَّمَ شُحُومَهَا جَمَلُوهُ ثُمَّ بَاعُوهُ فَأَكَلُوا ثَمَنَهُ
"Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wameharamisha uuzaji wa pombe, mzoga, nguruwe na masanamu. Pakasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unaonaje kuhusu mafuta ya mzoga kwani yanapakwa katika merikebu na kusingwa kwayo ngozi na watu hutumia kwa taa zao? Akasema: Hapana, hiyo ni haramu. Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akasema wakati huo: Mwenyezi Mungu awaangamize Mayahudi, kwani Mwenyezi Mungu alipoharamisha mafuta yake, waliyayeyusha kisha wakayauza na wakala thamani yake."
- Na katika Tahdhib al-Athar cha At-Tabari kutoka kwa Jabir amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema:
لا تَنْتَفِعوا مِنَ الميْتَةِ بِشَيْءٍ
"Msitumie chochote kutokana na mzoga."
- Na imevuliwa ngozi ya mzoga kama ilivyokuja katika hadithi ya Abu Dawood kutoka kwa Ibn Abbas... kutoka kwa Maymunah amesema: Mtumishi wetu alipewa zawadi ya mbuzi kutokana na sadaka kisha akafa. Mtume ﷺ akampita na kusema:
أَلَا دَبَغْتُمْ إِهَابَهَا وَاسْتَنْفَعْتُمْ بِهِ قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهَا مَيْتَةٌ قَالَ إِنَّمَا حُرِّمَ أَكْلُهَا
"Je, hamkuitengeneza ngozi yake kwa kuitia rangi na mkanufaika nayo? Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, huyu ni mzoga. Akasema: Hakika kilichoharamishwa ni kuila tu."
Na Bukhari ametoa kutoka kwa Jabir bin Abdullah (ra) kwamba alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akisema mwaka wa kukombolewa Makka akiwa Makka: "Hakika Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wameharamisha uuzaji wa pombe."
Na Bukhari pia ametoa kutoka kwa Anas (ra): Nilikuwa ninawanywesha watu katika nyumba ya Abu Talha na pombe yao siku hiyo ilikuwa ni Al-Fadikh. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akaamuru mpiga mbiu atangaze: "Fahamuni kuwa pombe imeharamishwa." Akasema: Abu Talha akaniambia: Toka nje ukaimwage. Nikatoka na kuimwaga ikatiririka katika vichochoro vya Madina.
Na Abu Dawood ametoa kutoka kwa Abu Hurairah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: "Mwenyezi Mungu ameharamisha pombe na thamani yake, na ameharamisha mzoga na thamani yake, na ameharamisha nguruwe na thamani yake."
3- Kujitibu kunavuliwa katika uharamu huo, kwani kujitibu kwa kilichoharamishwa na najisi si haramu:
Kuhusu kuwa kujitibu kwa kilichoharamishwa si haramu, ni kutokana na hadithi ya Muslim kutoka kwa Anas: "Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alimruhusu Az-Zubair bin Al-Awwam na Abdurrahman bin Awf kuvaa hariri kwa sababu ya mwasho uliokuwa ukiwasumbua." Na kuvaa hariri kwa wanaume ni haramu, lakini kuliruhusiwa kwa ajili ya matibabu. Pia kutokana na hadithi ya An-Nasa'i, Abu Dawood na At-Tirmidhi... amepokea kutoka kwa babu yake Arfajah bin As'ad kwamba pua yake ilikatwa siku ya Al-Kulab katika zama za ujahiliya, akatengeneza pua ya fedha na ikanuka. "Basi Mtume ﷺ akamuamuru atengeneze pua ya dhahabu." Na dhahabu kwa wanaume ni haramu, lakini iliruhusiwa kwa ajili ya matibabu.
Ama kuhusu kujitibu kwa najisi si haramu, ni kutokana na hadithi ya Bukhari kutoka kwa Anas (ra): "Kwamba watu waliumwa na maradhi ya tumbo (ajtawwū) huko Madina, basi Mtume ﷺ akawaamuru waungane na mchungaji wake (wa ngamia) wakanywe maziwa yake na mikojo yake. Wakajiunga na mchungaji na wakanywa maziwa yake na mikojo yake..." Na maana ya ajtawwū ni kuwa chakula cha hapo hakikuwafaa, wakaugua. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliwaruhusu katika kujitibu kutumia "mkojo" ambao ni najisi. Bukhari ametoa kutoka kwa Abu Hurairah kwamba amesema: "Mbedui alisimama na kukojoa msikitini, watu wakamvamia, Mtume ﷺ akawaambia: Mwacheni na mwagieni juu ya mkojo wake ndoo ya maji - kwani mmetumwa kuwa wafanyaji wepesi na hamkutumwa kuwa wafanyaji uzito."] Mwisho.
Tatu: Na ilikuja katika jibu la swali la tarehe 19/09/2013M:
[... Na jibu ni kuwa matumizi ya pombe katika dawa, na pia dawa ambayo inaingia ndani yake kileo (alcohol)... basi hukumu yake ni kuruhusiwa pamoja na karaha (makruhu), na dalili ya hilo ni:
Ibn Majah ametoa kupitia Tariq bin Suwaid Al-Hadhrami amesema: "Nilisema, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, katika ardhi yetu kuna zabibu tunazozikamua kisha tunazinywa. Akasema: Hapana. Nikamrudia tena nikasema: Sisi tunajitibu kwayo kwa ajili ya mgonjwa. Akasema: Hakika hiyo si dawa bali ni ugonjwa." Huu ni ukatazo wa kutumia najisi au haramu "pombe" kama dawa. Lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliruhusu kujitibu kwa najisi "mkojo wa ngamia"... hadithi ya Anas (ra): "Watu kutoka Uraynah waliumwa na hali ya hewa ya Madina, basi Mtume ﷺ akawaruhusu waende kwenye ngamia wa sadaka wakanywe maziwa yake na mikojo yake..." Hii ina maana kuwa hali ya hewa haikuwafaa wakaugua, basi Mtume ﷺ akawaruhusu wajitibu kwa mikojo ya ngamia ambayo ni najisi. Kadhalika, Mtume ﷺ aliruhusu kujitibu kwa haramu "kuvaa hariri", kama ilivyopokewa na Tirmidhi na Ahmad kutoka kwa Anas: "Kwamba Abdurrahman bin Awf na Az-Zubair bin Al-Awwam walimlalamikia Mtume ﷺ kuhusu chawa katika vita vyao, naye akawaruhusu kuvaa kanzu za hariri. Akasema: Nikaziona zikiwa kwao." Hadithi hizi mbili ni kielelezo (qarina) kuwa ukatazo katika hadithi ya Ibn Majah si wa mkazo (ghayr jazim), yaani kujitibu kwa najisi na haramu ni makruhu.
Kwa hivyo, matumizi ya dawa ambayo kileo (alcohol) inaingia katika utengenezaji wake ni jaiz (inaruhusiwa) pamoja na karaha (makruhu). Na lililo bora ni kutoitumia alcohol katika utengenezaji wa dawa, lakini ikitumiwa, hukumu yake ni makruhu. Vivyo hivyo ikiwa mgonjwa atatumia dawa yenye alcohol, ni makruhu. Yote hayo ni ikiwa mchanganyiko huo wenye alcohol ni dawa kwa mujibu wa maoni ya wataalamu, na si kitu kingine.] Mwisho.
Kutokana na hayo, chanjo zenye viambata vilivyoharamishwa au najisi ni jaiz pamoja na karaha (makruhu) kwa sababu chanjo inaingia katika mlango wa kujitibu (tadaawi), na kujitibu kwa kilichoharamishwa na najisi kama ilivyobainishwa hapo juu ni jaiz pamoja na karaha... isipokuwa ikibainika kuwa ina madhara, hapo haitaruhusiwa.
Natumai kuwa jambo hili limekuwa wazi, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi na Mwenye Hekima zaidi.
Ndugu yenu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
08 Sha'ban 1442 H Sawa na 21/03/2021 M
Kiungo cha jibu kutoka ukurasa wa Amir (Mungu amuhifadhi) kwenye Facebook
Kiungo cha jibu kutoka ukurasa wa Amir (Mungu amuhifadhi) kwenye Web