Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

JAWABU LA SWALI: HAKI YA KHALIFAH YA KUMFUTA KAZI MSAIDIZI (MUAWIN)

July 18, 2014
3647

Mfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut Tahrir, kwa Maswali ya Wageni wa Ukurasa Wake wa Facebook "Fiqhi"

Swali:

Ilitajwa katika Utangulizi wa Katiba (Muqaddimatul Dustur) Sehemu ya Kwanza, Ibara ya 36 - d: Katika ufafanuzi kwamba Khalifah ana haki ya kumfuta kazi Msaidizi (Muawin) kwa kulinganisha na mwakilishi (wakil), isipokuwa kama kuna andiko linalomzuia kumfuta kazi katika hali maalum. Naomba ufafanuzi wa hali hizi maalum zinazomzuia Khalifah kumfuta kazi Msaidizi? Na mbarikiwe mapema kwa jibu, Assalamu Alaykum na muendelee kubaki katika ulinzi Wake. Mwisho.

Jibu:

(Wa Alaykumus Salam wa Rahmatullahi wa Barakatuh)

Andiko lililomo katika kitabu cha Muqaddimah uk. 151 ni: (...lakini kwa kuwa Msaidizi (Muawin) hupata mamlaka kutoka kwa Khalifah, na yeye ni kama naibu wake, basi (Khalifah) anakuwa na haki ya kumfuta kazi kwa kulinganisha na mwakilishi (wakil), kwa sababu mwenye kuwakilisha (muwakkil) ana haki ya kumfuta mwakilishi wake, isipokuwa kama kutakuja andiko la kumzuia kumfuta kazi katika hali maalum.) Mwisho.

Kauli yake "isipokuwa kama kutakuja andiko la kumzuia kumfuta kazi katika hali maalum" hairudi kwa Msaidizi bali inarudi kwa mwakilishi (wakil). Asili katika mkataba wa uwakala ni kwamba ni mkataba wa hiyari (aqd ja’iz), hivyo mwenye kuwakilisha na mwakilishi wanaweza kuuvunja wakati wowote watakapo. Lakini mafakihi wametaja hali ambazo mkataba unakuwa wa lazima (aqd lazim), ambapo mwenye kuwakilisha hana haki ya kumfuta mwakilishi, kama vile mwakilishi anapokuwa wakili wa mizozo ya kisheria. Wanavyuoni wa Hanafi wamebainisha:

إِذَا تَعَلَّقَ بِالْوَكَالَةِ حَقُّ الْغَيْرِ فَإِنَّهُ لاَ يَجُوزُ الْعَزْل بِغَيْرِ رِضَا صَاحِبِ الْحَقِّ

"Ikiwa haki ya mtu mwingine imefungamana na uwakala, basi haijuzu kumfuta kazi bila ridhaa ya mwenye haki hiyo."

Na kuna baadhi ya hali nyingine zilizotajwa na mafakihi katika kumzuia mwenye kuwakilisha kumfuta mwakilishi wake.

Hivyo basi, maana ya sentensi uliyouliza ni tofauti na vile ulivyoielewa, kwani maana yake ni kwamba mwenye kuwakilisha anaweza kumfuta mwakilishi wake isipokuwa kama kuna andiko linalomzuia kumfuta mwakilishi wake katika hali maalum, na hii haihusu Msaidizi. Kwani Msaidizi inajuzu kwa Khalifah kumfuta kazi wakati wowote na hakuna hali maalum ambazo haifai kumfuta kazi.

Sentensi hii imetajwa kwa njia hii kwa sababu kumetumiwa ushahidi wa mada ya uwakala. Na asili ya uwakala ni mkataba wa hiyari ambao unaruhusu mwenye kuwakilisha kumfuta mwakilishi wake, isipokuwa katika hali maalum ambapo haijuzu kumfuta mwakilishi. Na Msaidizi ni kama mwakilishi wa Khalifah, hivyo inajuzu kwa Khalifah kumfuta kazi kwa kulinganisha na mwenye kuwakilisha anavyomfuta mwakilishi wake akifuata hukumu ya asili ya uwakala ambayo pia inatumika kwa Msaidizi. Na hali maalum hazitumiki katika haki yake, hivyo inajuzu kumfuta kazi Msaidizi wakati wowote.)

Ndugu yenu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Facebook

Kiungo cha jibu kutoka tovuti ya Amir

Kiungo cha jibu kutoka ukurasa wa Amir wa Google Plus

Share Article

Share this article with your network