** (Silsila ya Majibu ya Mwanachuoni Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa Maswali ya Wageni kwenye Ukurasa Wake wa Facebook)**
Kwa Al-Abid Lillah
Swali:
Imekuja katika kitabu cha Nidham al-Islam:
"Na kwa ajili hiyo, malengo makuu ya kulinda jamii hayakuwekwa na mwanadamu, bali ni miongoni mwa amri na makatazo ya Allah, nayo ni thabiti hayabadiliki wala kuendelezwa. Hivyo, kuhifadhi aina ya mwanadamu (nasaba), akili, heshima ya kibinadamu, nafsi ya mwanadamu, umiliki wa binafsi, dini, usalama, na dola, ni malengo makuu thabiti ya kulinda jamii, hayaguswi na mabadiliko wala maendeleo (ya kimazingira)."
Swali ni: Je, hakuna ijtihadi katika katiba ili kubadilisha baadhi ya maandiko (nussus) wakati imetajwa katika nukuu hiyo kuwa hayaguswi na mabadiliko wala maendeleo? Naomba ufafanuzi wa jambo hili, Allah akubarikini na akusaidieni.
Jawabu:
Wa Alaykum As-Salam wa Rahmatullahi wa Barakatuh.
Ewe ndugu yangu, ijtihadi haifanyiki katika maandiko ikiwa ni ya uhakika katika uthibiti wake (qat’i ath-thubut) na ya uhakika katika maana yake (qat’i ad-dalalah). Yaani, ya uhakika katika uthibiti wake kama vile aya ya Qur'ani na Hadithi Mutawatir, na ya uhakika katika maana yake kulingana na tafiti za kilugha na migawanyo ya Kitabu na Sunnah. Ijtihadi hufanyika tu katika maandiko yenye maana ya dhana (zanni ad-dalalah), iwe ni ya uhakika katika uthibiti (qat’i ath-thubut) au ya dhana katika uthibiti (zanni ath-thubut)... Maadamu maana yake ni ya dhana (zanni), basi ijtihadi hufanyika ndani yake kama inavyojulikana katika elimu ya Usul al-Fiqh.
Mambo yaliyotajwa katika kitabu kuwa ni malengo makuu ya kulinda jamii ya Kiislamu, ni ya uhakika katika uthibiti (qat’i ath-thubut) na ya uhakika katika maana (qat’i ad-dalalah). Hivyo basi, hukmu zake hazibadiliki kwa ijtihadi kwa sababu ijtihadi hapa haifanyiki; kwani maandiko yanayohusu mambo hayo ni ya uhakika (qat'i), na hakuna ijtihadi mbele ya maandiko ya qat'i.
Ndugu yenu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
Kiungo cha jawabu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Facebook
Kiungo cha jawabu kutoka kwenye tovuti ya Amir
Kiungo cha jawabu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Google Plus