Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

JAWABU LA SWALI: KUHUSU PESA ZA KARATASI KWA HAFEDH GHARSALLAH

May 17, 2013
4797

** (Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni mtukufu Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amiri wa Hizb ut Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wake kwenye ukurasa wake wa Facebook)**

Jawabu la Swali:

Kuhusu Pesa za Karatasi

Kwa Hafedh Gharsallah

Swali:

Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh,

Ndugu yangu mpendwa, Mwenyezi Mungu akulipe kheri kwa maelezo uliyotoa.

Niruhusu ndugu yangu nikuulize maswali haya:

Fikiria unajiona kuwa ni kibarua au mwajiriwa na ukanyimwa ujira wako au mshahara wako kwa miaka kadhaa iliyopita. Je, unaona ni uadilifu kuhukumiwa upewe ujira wako ule ule uliokanyimwa kwa thamani ile ile ya miaka 10 iliyopita kwa mfano? Kwa mfano, nikichukua kwako gramu 84 za dhahabu, inatakiwa kwangu nikurudishie gramu 84 za dhahabu hata baada ya miaka kumi, na hii ndiyo sheria ya Allah. Bwana wangu, gramu 84 za dhahabu = dinari 7230 kwa sasa, wakati miaka 10 iliyopita gramu 84 za dhahabu = dinari 1200. Hivyo, ikiwa nilikopa kwako dinari 1200 na nikakurudishia baada ya miaka 10 dinari 1200, nitakuwa nimekurudishia sehemu moja ya sita ya thamani, yaani gramu 14 za dhahabu. Huku ni kuipunguza thamani ya mali yako, na Allah (swt) ametukataza akisema katika Qur'ani Tukufu:

وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ

"Wala msiwapunguzie watu vitu vyao, wala msieneze uharibifu katika nchi kwa kufanya ufisadi." (QS. Ash-Shu'ara [26]: 183)

Na huu, kulingana na ufahamu wangu, ndio mradi wa haramu ya riba. Je, huoni ndugu yangu kuwa kitu (dinari ambayo haipati thamani yake kutoka ndani yake yenyewe, bali ni thamani iliyokubaliwa tu) kirudishwe kwenye asili yake (dhahabu)?

Jawabu:

Ndugu mpendwa Hafedh Gharsallah,

Wa Alaikum Salaam wa Rahmatullahi wa Barakatuh.

Kuhusu pesa za karatasi za sasa, zinatendewa kwa mujibu wa hukumu za naqd (pesa) kwa sababu ya kuwepo kwa sababu ya kisheria (illah) ya "unari" (naqdiyah), yaani kutumika kwa karatasi hizi kama thamani ya vitu (athman) na ujira wa huduma (ujur). Na kila kitu kinachofanyiwa muamala kama thamani ya bidhaa na ujira kinachukuliwa kuwa ni pesa (naqd) na hukumu za pesa zinatumika kwake madamu zinazunguka kati ya watu na hazijafutwa kutumika, yaani hazijabatilishwa kisheria.

Ama dalili ya kuzingatia karatasi hizi kuwa ni pesa zinazopaswa kutumiwa hukumu za pesa ni:

Kwani karatasi hizi za lazima (ilzamiyah), zimekubaliwa kufanywa kuwa ni pesa na thamani ya vitu, na ujira wa manufaa na huduma, na kwayo dhahabu na fedha hununuliwa, kama ambavyo kwayo bidhaa nyinginezo na vitu hununuliwa. Hivyo, ndani yake imepatikana illah (sababu ya kisheria) ya unari, yaani "kutumika kwake kama thamani (athman) na ujira (ujur)". Hizi ni sifa mbili zilizopatikana katika dhahabu na fedha zilizopigwa chapa kama dinari na dirhamu. Kwa sababu hiyo, hukumu za pesa (naqd) za dhahabu na fedha zinatumika kwa pesa za karatasi za lazima. Hivyo, zaka hutolewa kwayo, na hukatazwa ndani yake riba ya fadhli (riba al-fadl) na riba ya kuchelewesha (riba al-nasi’ah). Kwa hivyo, haijuzu kulipa deni kwa kiasi kikubwa zaidi yake, kwani kufanya hivyo itakuwa ni riba ya kuchelewesha. Kadhalika, haijuzu kubadilisha sarafu ya aina moja isipokuwa kiasi sawa kwa kiasi sawa na mkono kwa mkono... kulingana na hukumu za kisheria zinazohusu pesa, dhahabu na fedha.

Kwa mujibu wa hayo, deni lako kwa wengine hulipwa kwako kama lilivyo bila ziada yoyote hata kama thamani ya sarafu imeshuka au imeongezeka... madamu sarafu hiyo bado inatumika kisheria.

Ninathamini matatizo uliyoyataja yanayotokana na kushuka kwa thamani ya pesa. Kama ulivyotaja, ikiwa unamdai mtu dinari "1000" kwa mfano miaka kumi iliyopita na anataka kukulipa leo, ni wazi kuwa athari yake ni nzito kwako kutokana na kushuka kwa thamani ya karatasi hii katika kipindi cha miaka kumi. Lakini haki ina haki zaidi kufuatwa. Na madamu karatasi hii inatandawa na uhalisia wa pesa (naqd), basi hukumu zake zinatumika katika masuala ya riba. Kwa hiyo, haijuzu kulipa deni kwa kiasi kikubwa zaidi yake madamu karatasi hii ya pesa inafaa kisheria kwa mzunguko wa muamala.

Namuomba Allah (swt) akubariki katika mali yako, familia yako na watoto wako.

Ndugu yenu, Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah

Kiungo cha jawabu kutoka kwenye ukurasa wa Amiri katika Facebook

Kiungo cha jawabu kutoka kwenye tovuti ya Amiri

Kiungo cha jawabu kutoka kwenye ukurasa wa Amiri katika Google Plus

Share Article

Share this article with your network