Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: Kuhusu Zaka

March 14, 2014
3847

** (Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni Ata bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wake kwenye ukurasa wake wa Facebook)**

Kwa Kartal Kara

Swali:

selamun aleykum, i've a question about zakat: first, i'll tell you the situation; i've make profit on selling appartement, for example: i bought an appartement for 30000 and sold it for 35000, after one year i've made 20000 profit. i had last year 100000 and now i have 120000: on which amount i have to pay the zakat? 120000 or 20000?

Tafsiri ya Swali:

Assalamu Alaikum, nina swali kuhusu Zaka: kwanza nitaelezea hali halisi ya suala langu. Nimepata faida kupitia uuzaji wa nyumba (apartmeni); kwa mfano, nilinunua nyumba kwa 30,000 na nikaiuza kwa 35,000. Baada ya mwaka mmoja, nimepata faida inayokadiriwa kuwa 20,000. Katika mwaka uliopita nilikuwa na 100,000 na sasa nina 120,000. Je, ni kiasi gani ambacho ninapaswa kulipia Zaka? Ni 20,000 au 120,000?

Jibu:

Wa Alaikum Salaam Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh.

Ni wazi kutokana na swali lako kwamba unafanya biashara ya kununua na kuuza nyumba, na kwa hivyo, Zaka hapa inaingia katika mlango wa Zaka ya biashara (Zakat al-Tijarah). Bidhaa zinazochukuliwa kwa ajili ya biashara ni wajibu kutolewa Zaka, bila ya kuwepo khilaf (tofauti) miongoni mwa Maswahaba. Kutoka kwa Samurah bin Jundub amesema:

أَمَّا بَعْدُ، فَإِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَأْمُرُنَا أَنْ نُخْرِجَ الصَّدَقَةَ مِنْ الَّذِي نُعِدُّ لِلْبَيْعِ

"Ama baada ya hayo, hakika Mtume wa Allah (saw) alikuwa akituamrisha tutoe sadaka (Zaka) kutokana na kile tulichokiandaa kwa ajili ya kuuza." (Imepokelewa na Abu Dawood)

Vilevile, uwajibu wa kutoa Zaka katika biashara umepokelewa kutoka kwa Umar, mwanawe (Abdullah bin Umar), Ibn Abbas, mafaqihi saba, Al-Hasan, Jabir, Tawus, Al-Nakha’i, Al-Thawri, Al-Awza’i, Al-Shafi’i, Ahmad, Abu Ubaid, As-habu Al-Ra’yi, Abu Hanifa, na wengineo.

Zaka katika bidhaa za biashara ni wajibu ikiwa thamani yake itafikia kiwango cha nisabu ya dhahabu, au thamani ya nisabu ya fedha, na ikapitiwa na mwaka (Hawl).

Ikiwa mfanyabiashara ataanza biashara yake kwa mali iliyo chini ya nisabu, na mwishoni mwa mwaka mali hiyo ikafikia nisabu, basi hana wajibu wa kutoa Zaka kwa wakati huo; kwa sababu nisabu haijapitiwa na mwaka. Atapaswa kutoa Zaka ya nisabu hiyo baada ya kupita mwaka mmoja kamili.

Lakini ikiwa mfanyabiashara ataanza biashara yake kwa mali inayozidi nisabu, kwa mfano alianza biashara yake kwa dinari elfu moja, na mwishoni mwa mwaka biashara yake ikakua, akapata faida, na thamani yake ikawa dinari elfu tatu, ni wajibu kwake kutoa Zaka ya dinari elfu tatu, na si ile elfu moja aliyoanza nayo; wala hatoi Zaka kwa faida pekee aliyoipata, bali hutoa kwa jumla ya kiasi chote alichonacho, yaani "3000". Hii ni kwa sababu ukuzi wa mali (nima' al-mal) uliotokana na mali ile ya mwanzo unafuata asili ya mali hiyo, na mwaka wa faida inayotokana nayo unakuwa ni uleule mwaka wa mali ya asili.

Kwa maneno mengine, suala hili ni kama ifuatavyo:

  1. Thamani ya bidhaa ya biashara inapofikia nisabu, ambayo ni dinari ishirini za dhahabu (sawa na gramu 85 za dhahabu), au dirham mia mbili za fedha (sawa na gramu 595 za fedha), hapo ndipo tarehe hiyo inarekodiwa na inakuwa ndiyo mwanzo wa mwaka (Hawl) wa Hijria.

  2. Mwishoni mwa mwaka, thamani ya bidhaa za biashara alizonazo inakokotolewa: (Mtaji na faida yake) na anatoa Zaka yake kwa kiwango cha (1 katika kila 40) au (2.5%).

  3. Kwa hivyo, jibu la swali lako ni kama ifuatavyo:

    a- Katika mwaka uliopita ulikuwa na 100,000 kwa ajili ya biashara, na hii ni zaidi ya nisabu.

    b- Kutokana na biashara ya kununua na kuuza nyumba, ulipata faida ya 20,000 katika kipindi cha mwaka.

    c- Mwishoni mwa mwaka (Hawl), umekuwa na 120,000.

    d- Zaka inayostahiki ni juu ya mali yote ya biashara, na si kwa faida pekee, yaani kwa kiasi chote cha biashara cha 120,000 kwa kiwango cha 2.5%, ambayo ni 3,000.

Ndugu yenu, Ata bin Khalil Abu al-Rashtah

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Amir: Facebook

Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir: Tovuti ya Amir

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Google Plus wa Amir: Google Plus

Share Article

Share this article with your network