(Mfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizbut Tahrir, kwa Maswali ya Wafuasi wa Ukurasa Wake wa Facebook)
Jibu la Swali:
Kuhusu Sehemu ya Awrah ya Mwanamke kwa Mwanamke
Kwa Shadi Sunoqrot
Swali:
Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Tafadhali fafanua kiwango cha awrah ya mwanamke kwa mwanamke mwenzake pamoja na dalili za kisheria, na ufafanuzi wa suala hili kwa ukamilifu. Pia bainisha upande wa kutoa dalili (وجه الاستدلال) kwa wale wanaosema kuwa ni kati ya kitovu na goti, na upande wa kutoa dalili kwa wale wanaosema kuwa ni sehemu za mapambo kama ilivyo awrah ya mwanamke mbele ya mahram wake.
Jibu:
Wa Alaikum Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh.
Kuhusu awrah ya mwanamke mbele ya mwanamke mwenzake, kuna maoni mawili ya kifaqihi ambayo yana upande wa kutoa dalili:
Kwanza: Kwamba awrah ya mwanamke kwa mwanamke ni kama awrah ya mwanamume kwa mwanamume, yaani kati ya kitovu na goti; na baadhi ya mafaqihi wanasema hivyo.
Pili: Kwamba awrah ya mwanamke kwa mwanamke ni mwili wake wote isipokuwa sehemu ambazo mwanamke hupambwa nazo kwa kawaida. Yaani, isipokuwa kichwa ambacho ni sehemu ya taji, uso sehemu ya kohl, shingo na kifua sehemu ya kidani, masikio sehemu ya hereni, mkono wa juu sehemu ya dumluj (pingu ya mkono), mkono wa chini sehemu ya bangili, kiganja sehemu ya pete, muundi sehemu ya kikuku, na unyayo sehemu ya hina.
Na kando na hizo, yaani kando na sehemu za mapambo ya kawaida ya mwanamke, sehemu nyingine zilizobaki ni awrah mbele ya mwanamke mwenzake. Yaani siyo tu kati ya kitovu na goti...
Na dalili ya hilo ni kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):
وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أأَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَواتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَى عَوْرَاتِ النِّسَاءِ
"...wala wasionyeshe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au wana wao, au wana wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi wanaume wasio na matamanio (kwa wanawake), au watoto ambao hawajajua siri za uchi wa wanawake." (QS. An-Nur [24]: 31)
Watu hawa wote inaruhusiwa kwao kuuona nywele wa mwanamke, shingo yake, sehemu ya pingu ya mkono wake, sehemu ya kikuku chake, sehemu ya kidani chake, na viungo vinginevyo ambavyo ni kweli kwamba ni sehemu ya mapambo, kwa sababu Mwenyezi Mungu anasema:
وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ
"wala wasionyeshe mapambo yao" (QS. An-Nur [24]: 31)
Yaani sehemu za mapambo yao.
Na yametajwa katika aya hii mahram na pia yametajwa wanawake. Hivyo inaruhusiwa kutazamana sehemu za mapambo kati ya wanawake wao kwa wao, lakini sehemu ambazo si za mapambo zinabaki kuwa ni awrah ya mwanamke mbele ya mwanamke mwingine.
Hili ndilo lenye nguvu (rajih) kwetu kulingana na dalili, na tunasema lenye nguvu kwa sababu wapo wanaofanya awrah ya mwanamke kwa mwanamke kuwa kama awrah ya mwanamume kwa mwanamume, yaani kati ya kitovu na goti.
Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
Link ya jibu kutoka kwa ukurasa wa Amir kwenye Facebook
Link ya jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir
Link ya jibu kutoka kwa ukurasa wa Amir kwenye Google Plus