Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: Kuhusu Mtazamo wa Mwanadamu juu ya Silika ya Kuhifadhi Aina

February 12, 2015
6529

(Silsila ya majibu ya mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook "Fikri")

Jibu la Swali

Kuhusu Mtazamo wa Mwanadamu juu ya Silika ya Kuhifadhi Aina

Kwa Faisal Kazmi

Swali:

Assalam Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh,

Imekuja katika kitabu cha Nidhamu ya Kijamii katika Uislamu ukurasa wa 16, chapa ya 1424H - 2004M yafuatayo: (Na lengo la kuwepo kwake ni kizazi kwa ajili ya kuhifadhi aina. Kwa sababu hiyo, ilikuwa ni lazima kuufanya mtazamo wa mwanadamu kuelekea silika hii kuelekezwa kwenye lengo ambalo kwa ajili yake iliumbwa ndani ya mwanadamu, nalo ni kuhifadhi aina, hakuna tofauti katika hilo kati ya mwanamume na mwanamke), na imekuja katika ukurasa wa 148 (Na azal inaruhusiwa kwa namna yoyote ile bila kujali kusudi la anayefanya hivyo, iwe amekusudia kuzuia kizazi, au kupunguza watoto, au amekusudia kumhurumia mke kutokana na udhaifu wake wa kubeba mimba na kujifungua, au amekusudia kutomchosha ili abaki kijana wa kufurahia naye, au amekusudia lengo lingine lolote, kwani mume ana haki ya kufanya azal bila kujali kusudi lake... Wala haisemwi kwamba kupunguza kizazi kunapingana na kile kilichohimizwa cha wingi wa kizazi aliposema: "Oaneni, zaaneni, muwe wengi", haisemwi hivyo kwa sababu kuruhusiwa kwa azal hakupingani na kuhimizwa kwa kuongeza kizazi; kile ni kuhimiza kuongeza kizazi, na hiki ni kuruhusu azal).

Swali ni kwamba: Kuruhusu kusudi la starehe au kutopata kizazi kunapingana na kuhifadhi kizazi ambacho ndicho lengo lililofanya silika hiyo kuwepo. Na vipi tutaoanisha kati ya kauli yetu: "Ni lazima kuufanya mtazamo wa mwanadamu kuelekea silika hii kuelekezwa kwenye lengo ambalo kwa ajili yake iliumbwa ndani ya mwanadamu nalo ni kuhifadhi aina", na kati ya kauli yetu: "Azal inaruhusiwa kwa namna yoyote ile bila kujali kusudi la anayefanya hivyo"? Na kwa usemi mwingine; Je, inajuzu kwa mtu kupuuza lengo ambalo kwa ajili yake silika iliumbwa, kwa mfano kwa kufanya azal? Na malipo yenu yako kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Muulizaji: Muhibbu Al-Rasul - Lahore, Pakistan.

Jibu:

Wa Alaykum Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh

Kwa taarifa tu, yale uliyoyanukuu ni kwa mujibu wa chapa mpya ukurasa wa 17 na ukurasa wa 161...

Hakika lengo la kuufanya mtazamo wa mwanadamu kuelekea silika ya kuhifadhi aina (ghariizah an-naw’) kuelekezwa kwenye madhumuni ambayo kwa ajili yake iliumbwa ndani ya mwanadamu, nayo ni kizazi na kuhifadhi aina, ni kudhibiti utoshelezaji wa silika hii kati ya mwanamume na mwanamke ndani ya maisha ya ndoa au yale yaliyo katika maana yake kama vile vijakazi (milk al-yamin). Hii ni kwa sababu maisha ya ndoa hayawi isipokuwa kati ya mwanamume na mwanamke, na ndiyo yanayounda mfumo sahihi wa kuwepo kwa kizazi na watoto na malezi yao chini ya uangalizi wa wazazi wao ili kuhifadhi nasaba zao... Tofauti na kuufanya mtazamo wa silika kuelekezwa kwenye ladha na starehe pekee, kwani hilo humaanisha kuachia huru silika hiyo kiasi kwamba mwanadamu anaitosheleza kwa namna yoyote ile; mwanamume na mwanamume, mwanamke na mwanamke, mwanadamu na mnyama, na mwanamume na mwanamke nje ya maisha ya ndoa... kama ilivyo sasa katika nchi za Magharibi ambapo mtazamo wao umejikita kwenye starehe na ladha, hivyo kumeenea miongoni mwao ushoga na usagaji wa kila aina, kubadilishana wake, uzina na uchafu, na mahusiano ya kijinsia na wanyama...

Na haya yote hayazingatii lengo ambalo silika iliumbwa kwa ajili yake, nalo ni kuhifadhi aina katika mfumo sahihi. Hii ndiyo maana ya kutoelekeza mtazamo kwenye ladha na starehe pekee na ulazima wa kuufanya uelekezwe kwenye lengo ambalo kwa ajili yake silika iliumbwa, nalo ni kizazi na kuhifadhi aina.

Ama kuhusu azal, hiyo ni suala jingine. Azal kisheria iko ndani ya mtazamo huu sahihi kwa sababu inafanyika ndani ya mfumo wa maisha ya ndoa au na vijakazi. Pia, azal inahusiana na lengo la kumwendea mke na si lengo la silika yenyewe. Sio lazima kila wakati lengo la kumwendea mke liwe ni kupata kizazi; kumwendea mke katika kipindi cha ujauzito hakulengi kupata kizazi, na mke anapofikia ukomo wa hedhi kumwendea kwake hukuwi kwa lengo la kupata kizazi, na kadhalika kumwendea mke ambaye ni tasa asiyezaa...

Na haya yote uhalisia wake ni sawa na azal kwa upande wa kutopata kizazi. Kwa hiyo, hakuna mgongano kati ya kauli ya kuruhusiwa kwa azal na kauli inayosema kuwa mtazamo wa silika lazima uelekezwe kwenye lengo ililoumbwa kwa ajili yake, nalo ni kizazi na kuhifadhi aina, kwa sababu hilo linapatikana kupitia ndoa hata kama ndani yake kutakuwa na azal.

Hii ni upande mmoja, na upande mwingine ni kwamba zimekuja hadithi kuhusu kuruhusiwa kwa azal, miongoni mwazo:

Ibn Hibban ametoa katika Sahih yake kutoka kwa Jabir bin Abdullah kwamba mtu mmoja katika Maansari alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema: "Nina kijakazi na huwa nafanya naye azal (namwaga mbegu nje)." Mtume (saw) akasema:

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ أَنَّ رَجُلًا مِنَ الْأَنْصَارِ جَاءَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ ﷺ فَقَالَ: إِنَّ عِنْدِي جَارِيَةً وَأَنَا أَعْزِلُ عَنْهَا فَقَالَ ﷺ: «إِنَّهُ سَيَأْتِيهَا مَا قُدِّرَ لَهَا» ثُمَّ أَتَاهُ بَعْدَ ذَلِكَ فَقَالَ: إِنَّهَا قَدْ حَمَلَتْ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «مَا قَدَّرَ اللَّهُ نَسَمَةً تَخْرُجُ إِلَّا هِيَ كَائِنَةٌ»

"Hakika kitamfika kile kilichokadiriwa kwake." Kisha akamjia baada ya hapo akasema: "Hakika amepata mimba." Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema: "Mwenyezi Mungu hakukadiria kiumbe kitoke isipokuwa lazima kiwepo." (Imepokelewa na Ibn Hibban).

Kwa muhtasari, hakuna mgongano katika yale yaliyokuja katika ukurasa wa 17 na ukurasa wa 161.

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Link ya jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir

Link ya jibu kutoka kwenye ukurasa wa Google Plus wa Amir

Share Article

Share this article with your network