Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jawabu la Swali: Kuhusu kukatika kwa swala kutokana na kupita kwa mwanamke mbele ya mwenye kuswali

May 08, 2014
4649

(Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni mtukufu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wageni wa ukurasa wake wa Facebook)

Kwa Ziyad Abu Tariq

Swali:

Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh

Niko hospitalini nikimsindikiza mwanangu mgonjwa katika chumba cha matibabu. Wakati nikiswali, muuguzi (ambaye ni kafiri) alipita mbele yangu. Je, swala yangu inabatilika, ikizingatiwa kuwa siwezi kukiondoka chumba hicho?

Jawabu:

Wa Alaikum Assalam wa Rahmatullahi wa Barakatuh

Hakika kukatika kwa swala kwa sababu ya mwanamke kupita mbele ya mwenye kuswali ni jambo ambalo mafaqihi (wanachuoni wa sheria) wametofautiana, na hili ni miongoni mwa masuala ya ibada. Sitaki kutabanni (kuchagua maoni rasmi) katika suala hili, lakini nitakuelezea maoni ya mafaqihi wanaoaminika kuhusu mada hii, nawe unaweza kufuata (taqlid) yeyote unayetulia na ijtihad yake katika suala hili:

Maoni ya Masheikh wa Hanafi: Swala haikatiki kwa kupita mwanamke wala kiumbe kingine. Imeelezwa katika kitabu Al-Mabsut cha mwandishi wake: Muhammad bin Ahmad bin Abi Sahl Shams al-Aimmah al-Sarakhsi (aliyefariki 483 H):

(وَإِنْ مَرَّ بَيْنَ يَدَيْهِ مَارٌّ مِنْ رَجُلٍ أَوْ امْرَأَةٍ أَوْ حِمَارٍ أَوْ كَلْبٍ لَمْ يَقْطَعْ صَلَاتَهُ عِنْدَنَا... "وَلَنَا" حَدِيثُ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ - رَضِيَ اللَّهُ تَعَالَى عَنْهُ - قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: لَا يَقْطَعُ الصَّلَاةَ مُرُورُ شَيْءٍ وَادْرَءُوا مَا اسْتَطَعْتُمْ...)

"Na akipita mbele yake mpitaji awe mwanamume, mwanamke, punda, au mbwa, haikati swala yake kwetu... na hoja yetu ni hadithi ya Abu Sa’id al-Khudri (ra) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

لَا يَقْطَعُ الصَّلَاةَ مُرُورُ شَيْءٍ وَادْرَءُوا مَا اسْتَطَعْتُمْ

'Hapana kitu kinachokata swala kwa kupita (mbele ya anayeswali), na zuieni (mpitaji) kadiri mnavyoweza.' ..."

Maoni ya Masheikh wa Maliki: Imeelezwa katika kitabu Al-Dhakhira cha mwandishi wake Abu al-Abbas Shihab al-Din Ahmad bin Idris bin Abd al-Rahman al-Maliki, maarufu kama al-Qarafi (aliyefariki 684 H):

(السَّادِسُ قَالَ فِي الْكِتَابِ لَا يَقْطَعُ الصَّلَاةَ شَيْءٌ يَمُرُّ بَيْنَ يَدَيِ الْمُصَلِّي...)

"Sita: Amesema katika Kitabu: Hapana kitu kinachopita mbele ya mwenye kuswali kinachokata swala..."

Maoni ya Masheikh wa Shafi'i: Imeelezwa katika kitabu Al-Majmu' Sharh al-Muhadhdhab cha mwandishi wake Abu Zakaria Muhyi al-Din Yahya bin Sharaf al-Nawawi (aliyefariki 676 H):

(الْمَسْأَلَةُ الثَّالِثَةُ: إذَا صَلَّى إلَى سُتْرَةٍ فَمَرَّ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا رَجُلٌ أَوْ امْرَأَةٌ أَوْ صَبِيٌّ أَوْ كَافِرٌ أَوْ كَلْبٌ أَسْوَدُ أَوْ حِمَارٌ أَوْ غَيْرُهَا مِنْ الدَّوَابِّ لَا تَبْطُلُ صَلَاتُهُ عِنْدَنَا...)

"Suala la tatu: Ikiwa ataswali kuelekea sutra (kizuizi), kisha akapita kati yake na hiyo sutra mwanamume, mwanamke, mtoto, kafiri, mbwa mweusi, punda, au wanyama wengineo, swala yake haibatiliki kwetu..."

Maoni ya Masheikh wa Hanbali: Imeelezwa katika kitabu Al-Mughni cha mwandishi wake Abu Muhammad Muwaffaq al-Din Abdullah bin Ahmad bin Muhammad bin Qudamah al-Maqdisi (aliyefariki 620 H):

(مَسْأَلَةٌ؛ قَالَ: "وَلَا يَقْطَعُ الصَّلَاةَ إلَّا الْكَلْبُ الْأَسْوَدُ الْبَهِيمُ". يَعْنِي إذَا مَرَّ بَيْنَ يَدَيْهِ. هَذَا الْمَشْهُورُ عَنْ أَحْمَدَ - رَحِمَهُ اللَّهُ ، نَقَلَهُ الْجَمَاعَةُ عَنْهُ. قَالَ الْأَثْرَمُ: سُئِلَ أَبُو عَبْدِ اللَّهِ مَا يَقْطَعُ الصَّلَاةَ؟ قَالَ لَا يَقْطَعُهَا عِنْدِي شَيْءٌ إلَّا الْكَلْبُ الْأَسْوَدُ الْبَهِيمُ... وَمَعْنَى الْبَهِيمِ الَّذِي لَيْسَ فِي لَوْنِهِ شَيْءٌ سِوَى السَّوَادِ. وَعَنْ أَحْمَدَ رِوَايَةٌ أُخْرَى، أَنَّهُ يَقْطَعُهَا الْكَلْبُ الْأَسْوَدُ، وَالْمَرْأَةُ إذَا مَرَّتْ، وَالْحِمَارُ...).

"Suala: Amesema: 'Na haikati swala isipokuwa mbwa mweusi tititi'. Yaani akipita mbele yake. Hili ndilo maarufu kutoka kwa Ahmad (rh), limepokewa na kundi kutoka kwake. Amesema al-Athram: Abu Abdullah aliulizwa ni nini kinachokata swala? Akasema: Kwangu mimi hakuna kinachoikata isipokuwa mbwa mweusi tititi... na maana ya tititi ni yule ambaye rangi yake haina kitu kingine isipokuwa weusi. Na kuna riwaya nyingine kutoka kwa Ahmad kwamba inakatwa na mbwa mweusi, mwanamke akipita, na punda...".

• Kama unavyoona, kwa Masheikh wa Hanafi, Maliki, na Shafi'i swala haikatiki, na kwa Masheikh wa Hanbali katika kauli moja swala inakatika.

Namuomba Mwenyezi Mungu (swt) aufungue kifua chako kwa lile lililo la kheri. Wassalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh.

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Kiungo cha jawabu kutoka kwa ukurasa wa Amir kwenye Facebook

Kiungo cha jawabu kutoka kwenye tovuti ya Amir

Kiungo cha jawabu kutoka kwa ukurasa wa Amir kwenye Google Plus

Share Article

Share this article with your network