Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jawabu la Swali: Kuhusu Kupandisha Sauti kwa Wazazi Wawili

July 01, 2013
3932

(Mfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa Maswali ya Wafuasi wa Ukurasa Wake wa Facebook)

Jawabu la Swali:

Kwa Lamis Sh

Swali:

Ni ipi hukumu ya kukasirika (at-ta'sib) mbele ya wazazi wawili na kuwapandishia sauti? Ikizingatiwa kuwa mara nyingi wao husababisha matatizo na mtoto anakuwa ndiye mwenye kuyatua na kuyarekebisha... na badala ya wazazi kumtunza tangu udogo, yeye ndiye anayerekebisha misimamo na mienendo yao? Je, kukasirika na kuwapandishia sauti wakati mwingine huhesabika kuwa ni uasi kwa wazazi (uquq al-walidayn), na kunasababisha kukosa taufiki katika maisha?

Jibu:

Wa Alaykum Salaam Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh.

Hakika Allah (swt) amekataza kusema hata neno "Ah" (uff) kwa wazazi wawili, sasa itakuwaje kuhusu "kukasirika" (at-ta'sib) kwa wazazi na kuwapandishia sauti? Allah (swt) anasema:

وَقَضَى رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِنْدَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُلْ لَهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُلْ لَهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا

"Na Mola wako Mlezi amehukumu kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, au wote wawili, ukiwa naye, basi usiwaambie hata 'Ah!' wala usiwakemee, na useme nao kwa maneno ya heshima." (QS. Al-Isra [17]: 23)

Allah (swt) ameunganisha kuwatendea wema wazazi na ibada Kwake ili kuonesha ukuu wa faradhi hii. Kuna nusu (maandiko) nyingi kuhusu kuwatii wazazi wawili, na kwamba kuwatii wao kunarahisisha njia ya kuelekea Peponi kwa idhini Yake Subhaanahu. Mtume (saw) amesema katika hadith sahihi iliyopokelewa na Muslim kutoka kwa Abu Hurairah, kutoka kwa Mtume (saw) amesema:

رَغِمَ أَنْفُ، ثُمَّ رَغِمَ أَنْفُ، ثُمَّ رَغِمَ أَنْفُ، قِيلَ: مَنْ؟ يَا رَسُولَ اللهِ قَالَ: مَنْ أَدْرَكَ أَبَوَيْهِ عِنْدَ الْكِبَرِ، أَهَدُهُمَا أَوْ كِلَيْهِمَا فَلَمْ يَدْخُلِ الْجَنَّةَ

"Amepata hasara, kisha amepata hasara, kisha amepata hasara." Kukasemwa: Ni nani ewe Mtume wa Allah? Akasema: "Yule anayewadiriki wazazi wake wawili wakati wa uzee wao, mmoja wao au wote wawili, kisha (asifanye wema utakaomfanya) asiingie Peponi."

Hivyo basi, heri ni ya yule anayewadiriki wazazi wake wawili au mmoja wao katika uzee wao, akawatii na kusema nao maneno ya heshima, na wakamuingiza Peponi. Basi kila mmoja na awe na hamu ya kuwafanyia wema wazazi wake na kuwateremshia bawa la unyenyekevu kwa huruma...

Vyovyote iwavyo, ikiwa mtu ameteleza na "akasirika" mbele ya wazazi wake kama ilivyokuja katika swali, basi na amuombe msamaha Allah, na awaombe radhi na msamaha wazazi wake. Moyo wa mzazi ni wenye huruma na upendo, hivyo watawasamehe watoto wao makosa yao ikiwa watawaomba msamaha...

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Link ya jawabu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Facebook

Link ya jawabu kutoka kwenye tovuti ya Amir

Link ya jawabu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Google Plus

Share Article

Share this article with your network