(Silsila ya majibu ya mwanachuoni Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook)
Kwa Muafa Abu Haura
Swali:
Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Je, ni kweli kama inavyovuma nchini Indonesia kuwa Hizb ut-Tahrir na Amir wake wanakataa ukosoaji, masahihisho, na mijadala ya kielimu mpaka ikasemwa: "Ikiwa unataka kuibadilisha Hizb ut-Tahrir, basi lazima uwe Amir wake kwanza!"?
Je, inawezekana tukaendesha mjadala wa kielimu na mazungumzo ya utulivu katika ukurasa huu? Tunapenda kujadiliana kuhusu mada mbalimbali zinazohusu hukmu ya kisharia, fikra za Kiislamu, mambo ya kiutawala na mengineyo.
Jibu:
Wa Alaikumus Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh,
Tunakaribisha mjadala wowote wenye malengo, maadamu umejengwa juu ya yale yaliyomo ndani ya vitabu vyetu miongoni mwa fikra na hukmu... na wala siyo yale yanayosemwa kutuhusu katika vitabu vingine miongoni mwa uzushi... Yaani, tunakubali useme: "Imekuja katika kitabu chenu kadha...", kisha baada ya hapo sema lolote unalotaka miongoni mwa swali au ukosoaji, na sisi tutakujibu kwa idhini ya Allah. Lakini hatukubali kupoteza muda katika kunukuu yale yaliyozushwa dhidi yetu na baadhi ya wenye chuki dhidi ya Uislamu, kisha ukatuuliza kana kwamba unasema: "Imekuja katika kitabu cha fulani kwamba ninyi ni kadha wa kadha...". Hili ndilo ambalo hatupendi kupoteza muda nalo, bali tunawaacha wazushi hao kwa Mwenye Nguvu, Mwenye Kushinda Daima.
Vilevile, hatujadili mambo ya kiutawala ya mshikamano wa chama (taktul) kwa sababu mahali pake si hapa katika ukurasa huu.
Ewe ndugu yangu, hatujaweka neno lolote katika vitabu vyetu isipokuwa baada ya utafiti wa kina kwa dalili na njia ya utoaji dalili (wajh al-istidlal)... Kwa sababu hiyo, tuko tayari kufanya mjadala na kujibu ufafanuzi wowote kuhusu hayo.
Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah
Link ya jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir kwenye Facebook
Link ya jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir
Link ya jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir kwenye Google Plus