(Sfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Mheshimiwa Ata bin Khalil Abu al-Rashta, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa Maswali ya Wageni kwenye Ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi")
Kwa Umm Mus'ab al-Ja'bari
Swali:
As-Salaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh, ningependa kuuliza kuhusiana na ardhi: Kuna tofauti gani kati ya ardhi ambayo umiliki wake wa asili (raqaba) na manufaa yake ni ya mtu binafsi, na ardhi ambayo manufaa yake ni ya mtu binafsi lakini umiliki wake wa asili (raqaba) ni wa dola? Na Mwenyezi Mungu awalipe heri.
Jibu:
Wa Alaykumus Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh.
Hakuna tofauti kati ya ardhi ya Ushri na ardhi ya Kharaj, zote ziko sawa isipokuwa katika mambo mawili:
1- Mmiliki wa ardhi ya Ushri anamiliki raqaba yake (umiliki wa asili wa dhati ya ardhi) na manufaa yake, wakati mmiliki wa ardhi ya Kharaj anamiliki manufaa yake pekee na hamiliki raqaba yake. Inatokana na hili kwamba mmiliki wa ardhi ya Ushri akitaka kuifanya ardhi yake anayoimiliki kuwa wakfu, anaweza kufanya hivyo wakati wowote anaotaka, kwa sababu anamiliki dhati yake yaani raqaba yake. Ama mmiliki wa ardhi ya Kharaj, akitaka kuifanya ardhi yake anayoimiliki kuwa wakfu, hawezi kufanya hivyo, kwa sababu sharti la wakfu ni kwamba mtoaji wa wakfu lazima awe mmiliki wa dhati ya kitu anachokifanya kuwa wakfu. Na mmiliki wa ardhi ya Kharaj hamiliki dhati ya ardhi yaani raqaba yake, bali anamiliki manufaa yake tu, kwani raqaba yake ni milki ya Baytul Mal.
2- Katika ardhi ya Ushri, Zaka ni lazima (nusu ya ushuru [5%] au ushuru kamili [10%])... Ama ardhi ya Kharaj, inatozwa Kharaj.
Zaidi ya hayo, zote mbili ziko sawa; mmiliki huzitumia kulingana na hukumu za Sharia: kwa kuuza na kununua, na katika urithi... n.k.
Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu al-Rashta
Link ya jibu kutoka ukurasa wa Amir kwenye Facebook
Link ya jibu kutoka tovuti ya Amir
Link ya jibu kutoka ukurasa wa Amir kwenye Google Plus