(Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni Ata bin Khalil Abu al-Rashtah, Amiri wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook)
Jawabu la Swali: Ni upi ushahidi kwamba ardhi haikosi jukumu (waẓīfah)?
Kwa Abu Imran
Swali:
Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Imetajwa katika majibu ya maswali kwamba ardhi ya ushur mikononi mwa kafiri hulipiwa kharaji kwa sababu ardhi haikosi jukumu (waẓīfah), na kwa sababu ushur ni zaka na kafiri si miongoni mwa watu wa zaka (hapaswi kuitoa). Kwa hivyo, ni wajibu kwa kafiri ikiwa anamiliki ardhi ya ushur alipe kharaji kwa sababu ardhi haikosi jukumu (waẓīfah).
Ni upi ushahidi kwamba ardhi haikosi jukumu (waẓīfah), kwa maana ya kulipa zaka (ushur) au kharaji, pamoja na kwamba zaka haiwajibiki isipokuwa katika aina fulani (za mazao) na ikifikia kiwango (nisab)? Kwa mujibu wa hili, ardhi zote za ushur ambazo hupandwa mazao yasiyo katika aina zilizotajwa hazitalipiwa ushur wala kharaji. Kadhalika, kharaji ilistahiliwa kwenye ardhi ya kharaji kwa njia ya ushindi (fath), yaani Waislamu walimiliki asili yake (raqabah) walipoizuia (isiuzwe au kugawanywa).
Jibu:
Walaikum Assalam Warahmatullahi Wabarakatuh.
• Swali lako ni kuhusu ushahidi wa kwamba ardhi haikosi jukumu (waẓīfah), yaani ama ilipiwe ushur au nusu ya ushur kama zaka kwa mujibu wa hukumu za kisheria, au ilipiwe kharaji...
Jibu la hilo ni kwamba ushahidi uliokuja kuhusu hukumu za ardhi uliifanya iwe hivi: ama iwe ya ushur (ushriyah) au iwe ya kharaji (kharajiyah), na miongoni mwa ushahidi huu ni:
1- Ushahidi wa kijumla kuhusu kila ardhi, nao unawajibisha kwa Mwislamu ndani yake zaka ya ushur au nusu ya ushur...
فِيمَا سَقَتْ الأَنْهَارُ وَالْغَيْمُ الْعُشُورُ، وَفِيمَا سُقِيَ بِالسَّانِيَةِ نِصْفُ الْعُشْرِ
"Katika kile kilichonyoshewa na mito na mawingu (mvua) kuna Ushur (moja ya kumi), na katika kile kilichonyoshewa kwa kulingiwa (kama kwa kutumia mnyama) kuna nusu ya Ushur (moja ya ishirini)."
Hii ni kwa mujibu wa hukumu za kisheria zinazohusiana na aina ya mazao na kiwango chake.
2- Baada ya ushindi (fath), lilitokea tatizo jipya katika ardhi ambazo zilitolewa kwenye nusu hiyo ya jumla na kuwekewa kharaji:
قَضَى رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم فِيمَنْ أَسْلَمَ مِنْ أَهْلِ البَحْرَيْنِ أَنَّهُ قَدْ أَحْرَزَ دَمَهُ وَمَالَهُ إِلاَّ أَرْضَهَ، فِإِنَّهَا فَيْءٌ لِلْمُسْلِمِينَ؛ لأَنَّهُمْ لَمْ يُسْلِمُوا وَهُمْ مُمْتَنِعُونَ
"Mtume wa Allah (saw) alihukumu kwa aliyesilimu miongoni mwa watu wa Bahrain kwamba amehifadhi damu yake na mali yake isipokuwa ardhi yake, kwani hiyo ni fay-i kwa Waislamu; kwa sababu hawakusilimu bali walikataa (kujisalimisha)."
Na kile alichohukumu Umar (ra) katika ardhi ya Sawad: "Na nimeona niizuie ardhi pamoja na wakulima wake, na kuweka ndani yake kharaji...".
3- Kwa hiyo, kila ardhi katika Dar al-Islam ina zaka, isipokuwa aina maalum ambayo ina kharaji.
4- Hukumu ya jumla huenda kwa ujumla wake "kila ardhi katika Dar al-Islam kwa Mwislamu ndani yake ina zaka", na haitoki katika ujumla huo isipokuwa kile kilichohusishwa kwa nusu nyingine ya "ardhi ya kharaji".
5- Hii ndiyo hukumu ya ardhi za kilimo, na kama isingekuwepo nusu (maandiko) kuhusu ardhi ya kharaji, basi hukumu ya jumla ingebaki ambayo ni zaka ya ardhi kwa mmiliki wake Mwislamu kwa mujibu wa maandiko ya kisheria yaliyokuja. Hakuna hukumu nyingine zinazobainisha aina ya ardhi kwa upande wa kile kinacholipwa kwayo; ama ilipwe zaka au ilipwe kharaji, na hayo ni maandiko ya jumla ambayo kila ardhi inaingia chini yake.
6- Kutokana na ushahidi huu tuligundua kuwa ardhi haikosi jukumu (waẓīfah).
• Ama kuhusu swali lako ikiwa Mtume (saw) alifaradhisha kharaji kwa makafiri waliokuwa wanamiliki ardhi ya ushur, halijathibiti kwangu jambo lolote katika hayo kulingana na nijuavyo. Isipokuwa ushahidi uliotangulia unatosha kujua hukumu ya kisheria tuliyoigundua, nayo ni kwamba kauli yenye nguvu (rajih) kwetu ni kwamba ikiwa Ahlul Dhimma watamiliki ardhi ya ushur, basi ni lazima walipe kharaji juu yake, kwa sababu zaka inawajibika kwa Mwislamu pekee kwa mujibu wa hukumu za kisheria.
Pamoja na hayo, ikiwa unajua lolote kuhusu jambo hili basi unaweza kunitumia ili nilichunguze, nami nitakuwa mwenye shukrani kwako.
Ndugu yenu, Ata bin Khalil Abu al-Rashtah
Kiungo cha jawabu kutoka kwa ukurasa wa Amiri kwenye Facebook
Kiungo cha jawabu kutoka kwa tovuti ya Amiri
Kiungo cha jawabu kutoka kwa ukurasa wa Amiri kwenye Google Plus