بسم الله الرحمن الرحيم
(Mfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Mheshimiwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizbut Tahrir, kwa Maswali ya Wageni kwenye Ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi")
Jibu la Swali
Kwa: Abu Al-Qasim Nassar
Swali:
Sheikh wangu mpendwa, Assalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh,
Ningependa kukuuliza kuhusu kanuni ya kisharia inayosema "Dharura huhalalisha vilivyoharamishwa" (Ad-Dharurat tubihu al-mahzhurat).. Ni ipi makusudio ya kisharia ya neno "Dharura"? Na nitataja visa viwili ili kubainisha kusudio langu:
Kwanza: Ni fatwa ya Sheikh Yusuf al-Qaradawi kuhusu uhalali wa kuvua khimar (hijabu) katika shule za kigeni kwa madhumuni ya elimu, na akahesabu jambo hilo kuwa ni miongoni mwa dharura.
Kisa cha pili: Kuzalisha wanawake kupitia madaktari wa kiume.
Na ikiwa tutasema kuwa dharura inamaanisha tu kutokea kwa kifo na maangamizi.. kwanini basi madaktari wa kiume huwakagua wanawake wajawazito na kuwazalisha nyakati nyingine, na hii ni miongoni mwa matakwa ya dharura kutokana na kutokuwepo kwa mwanamke (daktari wa kike) kwa mfano...
Tunaona kuwa dharura, ikiwa tutaisema kuwa ni kifo, haijafikiwa katika visa vyote viwili.. katika elimu na katika uzazi?
Barakallahu fika na ujaziwe Pepo.
Jibu:
Wa Alaikum Salaam Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh:
Baadhi ya wanachuoni wameichukua kanuni ya "Ad-Dharurat tubihu al-mahzhurat" (Dharura huhalalisha vilivyoharamishwa) na wale wanaosema kanuni hii wametoa dalili kwa mifano kama kauli ya Mwenyezi Mungu (swt) katika aya ya 173 ya Surat Al-Baqarah:
إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنْزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللَّهِ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ
"Yeye amekuharimishieni mzoga tu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kilicho tajiwa kwa jina lisilo kuwa la Mwenyezi Mungu. Lakini aliyefikwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." (QS. Al-Baqarah [2]: 173)
Na kauli yake Mwenyezi Mungu (swt) katika aya ya 3 ya Surat Al-Ma’idah:
فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لِإِثْمٍ فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ
"Lakini aliyefikwa na dharura kwa njaa, bila ya kuelekea kwenye madhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." (QS. Al-Ma'idah [5]: 3)
Na kauli yake Mwenyezi Mungu (swt) katika aya ya 115 ya Surat An-Nahl:
إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنْزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّهِ بِهِ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ
"Yeye amekuharimishieni mzoga tu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kilicho tajiwa kwa jina lisilo kuwa la Mwenyezi Mungu. Lakini aliyefikwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." (QS. An-Nahl [16]: 115)
Mwenye kuitazama kanuni hii itambainikia kuwa si sahihi:
Hakika dalili walizozileta wenye kusema kanuni hii hazionyeshi kile walichokielekea, bali mwisho wa kile zinachoonyesha ni kwamba inajuzu wakati wa dharura kula mzoga na mfano wake kwa sababu ya njaa: "Lakini aliyefikwa na dharura kwa njaa" na makhmasah ni njaa na ukame unaokaribia kuleta maangamizi... katika hali hiyo inamjuzia kula kilichoharamishwa... Na dharura kama inavyoonekana wazi katika aya imefungwa na njaa na haivuki hapo, kwani tamko si la kiujumla au la kiholela kiasi cha kuvuka maana yake, bali limefungwa na njaa kali (al-makhmasah).
Katika baadhi ya sharhi (maelezo) ya kipengele hiki kwa wale wanaosema kanuni hii, wanaifanya kuwa kama rukhas (ruhusa/punguzo), lakini hata ruhusa inahitaji nass (andiko) na si akili kuifafanua bila ya nass... Kwa mfano kufungua katika Ramadhani wakati wa safari au wakati wa ugonjwa ni ruhusa (rukhsah), na hiyo ni kutokana na kuwepo kwa nass kama kauli yake Mwenyezi Mungu (swt):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ * أَيَّامًا مَعْدُودَاتٍ فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَر
"Enyi mlioamini! Mmeandikiwa saumu kama walivyovyoandikiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kucha mungu. (Siku hizo ni) siku maalumu za kuhesabika. Na atakayekuwa miongoni mwenu ni mgonjwa au yuko safarini, basi (atatimiza) idadi katika siku nyingine." (QS. Al-Baqarah [2]: 183-184). Na hivi ndivyo ilivyo kwa ruhusa zote kutokana na kuwepo kwa nass.
Hivyo basi, kanuni hii si sahihi kwa kuitekeleza kiujumla kama ilivyo nass yake kwa wale wanaosema kanuni hiyo. Na usahihi unaoonyeshwa na dalili ambazo wamezitegemea wenye kusema kanuni hii ni kwamba Muislamu anaruhusiwa kula au kunywa kile alichokiharamisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa vyakula vilivyoharamishwa katika hali ya dharura (njaa kali), na hazionyeshi kinyume na hivyo. Na ruhusa wakati wa dharura katika hali nyingine inahitaji dalili nyinginezo.
Ni vyema kutaja kuwa kanuni hii imekuwa katika zama zetu hizi ni egemeo la kuhalalisha kila kilichoharamishwa kwa kulifanya neno dharura kuwa neno pana linaloingiza mambo mengi chini yake kulingana na tafsiri yao ya dharura wanayoiona, mpaka yakakithiri maanguko katika haramu kwa jina la dharura!
Ama mifano iliyotajwa katika swali ambayo wanaihalalisha kwa kisingizio cha kanuni ya "dharura huhalalisha vilivyoharamishwa", hiyo haijuzu. Mwanamke wa Kiislamu aliyebalehe ni mukallaf (mwenye kuwajibika) kisharia kuvaa khimar, na haijuzu kwake kuvua khimar yake kwa kisingizio cha kusoma katika shule za kigeni. Bali anapaswa ikiwa anataka kusoma na haijafanya wepesi katika shule za kigeni kutafuta shule nyingine zinazomruhusu kuvaa khimar na jilbab, au kutegemea njia nyingine ya masomo, au kuhama (hijra) pamoja na mahram wake kwenda nchi ambayo itakuwa wepesi kwake kusoma huko... bila ya kuvua khimar yake, kwa sababu hakuna dalili zinazomhalalishia mwanamke aliyebalehe kuvua khimar yake kwa ajili ya masomo na kujifunza.
Ama daktari kuangalia tupu (awrah) ya mwanamke kwa ajili ya kumtibu, hiyo pia haimo chini ya kanuni ya "dharura huhalalisha vilivyoharamishwa", bali inaonyeshwa na dalili za kujuzu kwa tadawi (kujitibu) kama kauli ya Mtume (saw) katika hadith iliyopokelewa na At-Tirmidhi katika Sunan yake kutoka kwa Usamah bin Sharik, amesema: Mabedui walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je tusitibiwe? Alisema:
نَعَمْ، يَا عِبَادَ اللَّهِ تَدَاوَوْا، فَإِنَّ اللَّهَ لَمْ يَضَعْ دَاءً إِلَّا وَضَعَ لَهُ شِفَاءً، أَوْ قَالَ: دَوَاءً إِلَّا دَاءً وَاحِدًا
"Ndiyo, enyi waja wa Mwenyezi Mungu, jitibuni, kwani hakika Mwenyezi Mungu hakuweka ugonjwa isipokuwa ameuwekea ponyo – au alisema: dawa – isipokuwa ugonjwa mmoja"
Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni upi huo? Akasema: "Uzee (al-haram)". Na hapana shaka kuwa kufunua tupu ni miongoni mwa mahitaji ya kujitibu katika hali nyingi, na inatumikiwa na dalili za kujuzu kujitibu. Na katika hali hizi, ufichuaji (wa tupu) unakuwa kwa sehemu tu zinazohitajika kwa ajili ya matibabu na kujitibu, na haijuzu kufunua sehemu nyingine za tupu, yaani ni mahali pa matibabu pekee panapohitajika.
Ndugu yenu, Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah
Kiungo cha jibu kutoka ukurasa wa Facebook wa Amir: facebook
Kiungo cha jibu kutoka ukurasa wa Google Plus wa Amir: Googleplus
Kiungo cha jibu kutoka ukurasa wa Twitter wa Amir: Twitter
Kiungo cha jibu kutoka tovuti ya Amir: Amir