Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: Safari ya Mwanamke

March 01, 2016
7993

لا يحل لامرأة تؤمن بالله واليوم الآخر تسافرُ مسيرة يوم وليلة إلا مع ذي محرم عليها

"Haizuiwi (si halali) kwa mwanamke anayemwamini Allah na Siku ya Mwisho kusafiri mwendo wa siku na usiku isipokuwa akiwa na mahram wake." (Imepokewa na Muslim kupitia kwa Abu Hurayrah radhi za Allah ziwe juu yake).

1 - Ni haramu kwake kusafiri peke yake bila mahram kwa muda uliotajwa, yaani siku nzima (saa 24), usiku na mchana.

2 - Naswi (maandiko) inaashiria wakati na siyo umbali. Hivyo, akisafiri kwa ndege bila mahram umbali wa kilomita elfu moja, kisha akaenda na kurudi bila kukaa muda huo (saa 24), basi inajuzu kwake kufanya hivyo. Lakini akitembea kwa miguu umbali wa kilomita ishirini na safari hiyo ikamchukua zaidi ya mchana na usiku, basi ni haramu kwake kusafiri bila mahram.

3 - Naswi zilizokuja kuhusu kufupisha swala (qasr) na ruhusa ya kufungua saumu wakati wa kusafiri zinahusisha umbali (maburudi manne/ arba’atu burud) unaokadiriwa kuwa takriban kilomita 89. Kwa hivyo, umbali katika kufupisha swala ndio unaozingatiwa; yeyote anayesafiri umbali huu kwa ndege, meli, gari, au kwa miguu, inajuzu kwake kufupisha swala bila kujali muda wa safari unachukua muda gani.

4 - Hivyo basi, kigezo cha safari bila mahram kwa mwanamke ni wakati, mchana na usiku, bila kujali umbali. Ikiwa mwanamke hatakaa muda huu, bali akasafiri na kurudi kabla ya hapo, basi inajuzu kwenda kwake bila mahram. Ama katika kufupisha swala na kufungua saumu, kigezo ni umbali bila kujali kama muda ni mwingi au mchache.

5 - Ama kuhusu usalama wake binafsi, hilo ni suala jingine. Ikiwa hajisikii salama isipokuwa akiwa na mahram, basi asisafiri hata kama muda ni nusu mchana tu, kwani usalama wa nafsi yake ni suala tofauti.

6 - Mahram ni mwanamume miongoni mwa maharim wa mwanamke. Ama kuhusu wanawake wanaoaminika (nisa’ thikat), baadhi ya mafaqihi wanaliruhusu hilo, lakini sisi tunachagua kauli yenye nguvu zaidi (turajjiha) kuwa kusafiri kwake kuwe na mahram mwanamume kwa umbali/muda unaohitajika.

7 - Msafiri kwa ajili ya kozi fupi kwa muda wa miezi mitatu kwa mfano, hukumu yake ni hukumu ya msafiri ikiwa hajaifanya nchi anayosomea kuwa sehemu yake ya makazi (makan iqama), bali ni kwa ajili tu ya kutekeleza kozi na kurudi katika nchi yake ya asili. Katika hali hii, hukumu yake ni hukumu ya msafiri. Lakini ikiwa ataifanya nchi hiyo ya kozi kuwa sehemu yake ya makazi, basi katika hali hiyo safari yake inakatika na anachukua hukumu ya mkazi (muqim).

Share Article

Share this article with your network