(Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni mheshimiwa Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wageni wa ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi")
Jibu la Swali
Sharti la Uadilifu katika Kusimama kwa Ukhalifa
Kwenda kwa Abdul Kareem
Swali:
Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh
One of the conditions of the Khaleefah is that he must be 'adl (just). We use qiyas to derive this hukm but can the following verse of Qur'an be used as a daleel for this condition also
وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَن تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ
"Na mtakapohukumu baina ya watu, basi hukumuni kwa uadilifu." (An-Nisaa [4]: 58)?
Jazakallahu khayran.
Jibu:
Wa Alaikum Salaam wa Rahmatullahi wa Barakatuh,
Swali lako linahusu moja ya sharti za kusimama kwa Ukhalifa (shurut al-in’iqad) kama ilivyoelezwa katika vitabu vyetu:
(Katika kitabu Al-Ajhizah: [Tano: Lazima awe mwadilifu ('adl). Kwa hiyo, haisihi (haifai) kuwa fasiki. Uadilifu ni sharti la lazima kwa ajili ya kusimama kwa Ukhalifa na kuendelea kwake; kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) ameshurutisha kwa shahidi kuwa mwadilifu. Amesema (swt):
وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِّنكُمْ
"Na washuhudisheni watu wawili waadilifu miongoni mwenu." (At-Talaq [65]: 2)
Basi yule aliye mkuu kuliko shahidi, naye ni Khalifah, kwa kipaumbele zaidi (min bab al-awla) ni lazima awe mwadilifu; kwa sababu ikiwa uadilifu umeshurutishwa kwa shahidi, basi kuushurutisha kwa Khalifah ni muhimu zaidi.])
Suala hili kama uonavyo linahusu Khalifah kuwa mwadilifu, yaani uadilifu upatikane ndani ya Khalifah kama sifa miongoni mwa sifa zake, na si tu kuhukumu kwa uadilifu au kuamua migogoro kwa haki. Kwani kafiri anaweza kuhukumu baina ya watu wawili wenye ugomvi kwa uadilifu, pamoja na kwamba kafiri kwa ufasiki wake si mwadilifu ('adl)... Kwa ajili hiyo, kutoa dalili sahihi juu ya sharti la uadilifu ni kile tulichokitaja kuwa ni wajibu kwa shahidi, hivyo kwa Khalifah ni kwa kipaumbele zaidi.
Muhtasari ni kwamba, kupatikana kwa sharti la uadilifu kwa Khalifah maana yake ni kwamba yeye ni mwadilifu na anahukumu kwa uadilifu. Dalili hapa ni sharti la uadilifu kwa shahidi, na kwa Khalifah ni kwa kipaumbele zaidi, na ikiwa Khalifah ni mwadilifu basi atahukumu kwa uadilifu.
Ama kutoa dalili kwa aya tukufu (An-Nisaa: 58), hiyo inamaanisha kuhukumu kwa uadilifu, na si lazima kwamba anayehukumu kwa uadilifu au anayeamua migogoro kwa haki awe ni mwadilifu ('adl). Kwani kafiri anaweza kufanya uadilifu kama tulivyotaja hapo awali baina ya wagomvi wawili naye si mwadilifu, na kwa ajili hiyo, dalili yenye nguvu zaidi ni ile tuliyoitajia.
Wallahu A'lam wa Ahkam.
Ni vyema kutaja kwamba neno "حَكَمَ" (hakama) lililowekwa na Waarabu, yaani katika lugha au kile kinachoitwa ukweli wa kilugha (al-haqiqah al-lughawiyyah), ni "قضى" (qadha - aliamua/alihukumu):
Imekuja katika Al-Lisan: (Na Al-Hukmu: ni elimu, fikihi, na kuhukumu kwa uadilifu, nalo ni chimbuko (masdar) la hakama yahkumu... qadha: al-qadhaa: ni al-hukmu...)
Na katika Al-Qamus al-Muhit: (Al-Hukmu, kwa dhamma: ni al-qadhaa)... na katika Mukhtar as-Sihah: (Al-Hukmu ni al-qadhaa...)
Lakini neno hili "حكم" lilitumika kama istilahi katika zama za Mtume (saw) na Makhalifa Waongofu na Waarabu baada yao kwa maana ya utawala na mamlaka (al-mulk wa as-sultan), yaani ni matumizi ya kiistilahi (haqiqah urfiyyah khassah).
Hivyo basi, neno "حكم" ni ukweli wa kilugha katika maamuzi ya kisheria (mahakama), na ni ukweli wa kiistilahi mahususi katika utawala na mamlaka.
Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah
02 Dhul-Qa'dah 1439 H 15/07/2018 M
Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir (Mungu amuhifadhi) kwenye Facebook
Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir (Mungu amuhifadhi) kwenye Google Plus
Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir (Mungu amuhifadhi) kwenye Web