Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jawabu la Swali: Takhrij ya Hadithi "Chukueni zawadi madamu bado ni zawadi"

May 31, 2020
8631

Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni mtukufu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi"

Jawabu la Swali

Takhrij ya hadithi «خُذُوا الْعَطَاءَ مَا دَامَ عَطَاءً» Kwenda kwa Suleiman Ruba'

Swali:

Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh..

Tunamuomba Allah akupeni afya na akuwafikishe katika yale anayoyapenda na kuyaridhia, na ajaalie mikononi mwenu nusura, tamkin, na utukufu wa dini Yake.

Ninakuomba unibainishie takhrij ya hadithi hii kwa upande wa usahihi, nguvu, udhaifu, na kuitolea ushahidi, na shukrani kwako. Kutoka kwa Muadh bin Jabal, amesema: Nilimsikia Mtume wa Allah ﷺ akisema:

خُذُوا الْعَطَاءَ مَا دَامَ عَطَاءً، فَإِذَا صَارَ رِشْوَةً فِي الدِّينِ فَلَا تَأْخُذُوهُ، وَلَسْتُمْ بِتَارِكِيهِ؛ يَمْنَعُكُمُ الْفَقْرَ وَالْحَاجَةَ، أَلَا إِنَّ رَحَى الْإِسْلَامِ دَائِرَةٌ، فَدُورُوا مَعَ الْكِتَابِ حَيْثُ دَارَ، أَلَا إِنَّ الْكِتَابَ وَالسُّلْطَانَ سَيَفْتَرِقَانِ، فَلَا تُفَارِقُوا الْكِتَابَ، أَلَا إِنَّهُ سَيَكُونُ عَلَيْكُمْ أُمَرَاءُ يَقْضُونَ لِأَنْفُسِهِمْ مَا لَا يَقْضُونَ لَكُمْ، إِنْ عَصَيْتُمُوهُمْ قَتَلُوكُمْ، وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ أَضَلُّوكُمْ

"Chukueni zawadi (al-ata’) madamu bado ni zawadi, lakini itakapokuwa ni rushwa katika dini basi msiichukue, na hamtoiacha; umasikini na haja vitawazuia. Jueeni kuwa kinu cha Uislamu kinazunguka, basi zungukeni pamoja na Kitabu popote kinapozunguka. Jueeni kuwa Kitabu na utawala (as-sultan) vitatengana, basi msifarikiane na Kitabu. Jueeni kuwa kutakuwa na viongozi juu yenu watakaojihukumia nafsi zao wasivyowahukumia ninyi; mkiwaasi watawaua, na mkiwatii watawapoteza."

Walisema: Ewe Mtume wa Allah, tufanye nini? Akasema:

كَمَا صَنَعَ أَصْحَابُ عِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ، نُشِرُوا بِالْمَنَاشِيرِ، وَحُمِلُوا عَلَى الْخَشَبِ، مَوْتٌ فِي طَاعَةِ اللَّهِ خَيْرٌ مِنْ حَيَاةٍ فِي مَعْصِيَةِ اللَّهِ

"Kama walivyofanya maswahaba wa Isa mwana wa Maryam, walipasuliwa kwa misumeno na kubebwa juu ya mbao. Kifo katika kumtii Allah ni bora kuliko maisha katika kumuasi Allah."

Jibu:

Wa Alaikum Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh.

Hadithi hii imesemwa kuwa katika baadhi ya wapokezi wa isnadi yake kuna udhaifu... na imesemwa kuwa ina mapokezi mengine ambayo wapokezi wake ni waaminifu (thiqat):

1- Imekuja katika (Jami' al-Ahadith) cha mtunzi wake Jalaluddin al-Suyuti (aliyefariki 911 H):

  • 11863 «Chukueni zawadi madamu bado ni zawadi, lakini itakapokuwa ni rushwa katika dini basi msiichukue, na hamtoiacha; umasikini na haja vitawazuia. Jueeni kuwa kinu cha Uislamu kinazunguka, basi zungukeni pamoja na Kitabu popote kinapozunguka. Jueeni kuwa Kitabu na utawala vitatengana, basi msifarikiane na Kitabu. Jueeni kuwa kutakuwa na viongozi juu yenu watakaojihukumia nafsi zao wasivyowahukumia ninyi; mkiwaasi watawaua, na mkiwatii watawapoteza. Walisema: Ewe Mtume wa Allah, tufanye nini? Akasema: Kama walivyofanya maswahaba wa Isa mwana wa Maryam, walipasuliwa kwa misumeno na kubebwa juu ya mbao. Kifo katika kumtii Allah ni bora kuliko maisha katika kumuasi Allah» (Al-Tabarani kutoka kwa Muadh kwa isnadi: Alituhadithia Al-Qasim bin Yusuf bin Yaqub al-Balkhi, alituhadithia Ali bin Hujr al-Marwazi, (h) na alituhadithia Khattab bin Said al-Dimashqi, na Al-Hussein bin Ishaq al-Tustari, wakasema: Alituhadithia Hisham bin Ammar, wakasema: Alituhadithia Abdullah bin Abdulrahman bin Yazid bin Jabir, kutoka kwa Al-Wadhin bin Ata, kutoka kwa Yazid bin Marthad, kutoka kwa Muadh bin Jabal, amesema: Nilimsikia Mtume wa Allah ﷺ akisema...

Imeandikwa na Al-Tabarani (16599), Al-Haythami amesema (5/238): Yazid bin Marthad hakusikia kutoka kwa Muadh, na Al-Wadhin bin Ata amethibitishwa kuwa mwaminifu na Ibn Hibban na wengineo na amedhoofishwa na kikundi fulani, na wapokezi wake waliosalia ni waaminifu (thiqat). Imeandikwa pia na: Al-Tabarani katika al-Shamiyyin (1/379, nambari 658), na Al-Tabarani katika al-Saghir (2/42, nambari 749). Na kama unavyoona, baadhi ya wapokezi wa isnadi wana maneno (mapungufu) kwa baadhi ya wanazuoni wa hadithi, lakini baadhi yao ni waaminifu kwa wanazuoni wengine.

2- Na imekuja katika (Ithaf al-Khairat al-Mahara) cha mtunzi wake Al-Hafiz Ahmad bin Abi Bakr bin Ismail al-Busiri (aliyefariki mwaka 840 H):

[7571] Kutoka kwa Muadh bin Jabal (ra) kutoka kwa Mtume wa Allah ﷺ: «Chukueni zawadi madamu ni zawadi, na itakapokuwa ni rushwa katika dini basi msiichukue, na hamtoiacha; hofu na umasikini vitawazuia kufanya hivyo. Jueeni kuwa kinu cha imani kinazunguka na kinu cha Uislamu kinazunguka, basi zungukeni pamoja na Kitabu popote kinapozunguka. Jueeni kuwa utawala na Kitabu vitatengana, basi msifarikiane na Kitabu. Jueeni kuwa kutakuwa na viongozi juu yenu, mkiwatii watawapoteza, na mkiwaasi watawaua. Walisema: Tufanye nini ewe Mtume wa Allah? Akasema: Kama walivyofanya maswahaba wa Isa mwana wa Maryam, walibebwa juu ya mbao, na walipasuliwa kwa misumeno. Kifo katika kumtii Allah ni bora kuliko maisha katika kumuasi Allah».

Imepokelewa na Ishaq bin Rahwayh kutoka kwa Suwaid bin Abdulaziz al-Dimashqi, naye ni dhaifu, na imepokelewa na Ahmad bin Mani', na wapokezi wake ni waaminifu (thiqat), na tamko la wote wawili ni moja.

Kama unavyoona, baadhi ya mapokezi ni dhaifu, ama isnadi ya mapokezi ya Ahmad bin Mani' wao ni waaminifu (thiqat).

Natumai hapo pana kutosheleza, na Allah ni Mjuzi zaidi na Hakimu zaidi.

Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah

09 Shawwal 1441 H Inayoambatana na 31/05/2020 M

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir (Allah amuhifadhi) kwenye Facebook

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir (Allah amuhifadhi) kwenye Tovuti

Share Article

Share this article with your network