Home About Articles Ask the Sheikh
Sheria

Jibu la Swali: Zaka ya Bidhaa za Biashara

August 08, 2014
3889

(Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni mtukufu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amiri wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi")

Jibu la Swali

Zaka ya Bidhaa za Biashara

Kwa: Imad M. Sa'ad

Swali:

Assalamu Alaykum Sheikh wetu, Mwenyezi Mungu akutukuze kwa Uislamu na autukuze Uislamu kupitia kwako, na ninaomba kwa Mwenyezi Mungu niwe miongoni mwa wale watakaokupa baia ya Khilafah kwa njia ya Utume, hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu.

Nina swali kuhusu zaka; zaka ya bidhaa za biashara au mali; je, inafaa kuitoa yote au sehemu yake kabla ya kutimia mwaka mmoja (hawl) juu yake? Na je, kutimia kwa mwaka ni sharti la kuitoa?

Mwenyezi Mungu awasaidie kwa yale yenye kheri kwa Uislamu na Waislamu hapa duniani na Akhera. Wassalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Jibu:

Wa Alaykumussalam Warahmatullahi Wabarakatuh.

Hakika kutimia kwa mwaka (hawl) ni sharti katika sababu ya zaka (Nisab). Sharti likitimia, yaani mwaka kupita juu ya sababu hiyo (Nisab) bila kupungua, basi zaka inakuwa ni wajibu. Lakini, ikiwa itatolewa kabla ya kuwajibika kwake, basi kutoa huko kunajuzu kwa mujibu wa dalili za kisheria zilizopokelewa, miongoni mwazo ni:

  • Al-Bayhaqi ametoa katika As-Sunan al-Kubra kutoka kwa Ali:

عَنْ عَلِيٍّ، «أَنَّ الْعَبَّاسَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ سَأَلَ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم فِي تَعْجِيلِ صَدَقَتِهِ قَبْلَ أَنْ تَحِلَّ فَأَذِنَ لَهُ فِي ذَلِكَ»

"Kutoka kwa Ali, 'Kwamba Al-Abbas (ra) alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kuhusu kuharakisha kutoa zaka yake kabla haijawajibika, na akamruhusu kufanya hivyo'."

  • Na Al-Daraqutni ametoa katika Sunan yake kutoka kwa Hujr al-Adawi kutoka kwa Ali amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alimwambia Umar:

«إِنَّا قَدْ أَخَذْنَا مِنَ الْعَبَّاسِ زَكَاةَ الْعَامِ عَامِ الْأَوَّلِ»

"Hakika sisi tayari tumeshachukua kutoka kwa Al-Abbas zaka ya mwaka huu na ya mwaka ujao."

  • Na Al-Daraqutni ametoa kutoka kwa Musa bin Talhah kutoka kwa Talhah kwamba Mtume (saw) amesema:

«يَا عُمَرُ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّ عَمَّ الرَّجُلِ صِنْوُ أَبِيهِ؟ إِنَّا كُنَّا احْتَجْنَا إِلَى مَالٍ فَتَعَجَّلْنَا مِنَ الْعَبَّاسِ صَدَقَةَ مَالِهِ لِسَنَتَيْنِ»

"Ewe Umar, kwani hujui kwamba ami wa mtu ni sawa na baba yake? Hakika tulikuwa na uhitaji wa mali, kwa hiyo tukachukua zaka ya mali ya Al-Abbas mapema kwa ajili ya miaka miwili."

Wametofautiana kuhusu Al-Hakam katika isnadi yake, na usahihi ni kutoka kwa Al-Hasan bin Muslim ni Mursal.

Kwa msingi huo, kuharakisha utoaji wa zaka kabla ya kuwajibika kwake ni jambo linalojuzu. Na kwa taarifa, mafaqihi wengi wanasema hivyo.

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Kiungo cha jibu kutoka kwa ukurasa wa Amiri kwenye Facebook

Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amiri

Kiungo cha jibu kutoka kwa ukurasa wa Amiri kwenye Google Plus

Share Article

Share this article with your network