Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: "Je, Hadithi ya Dhanni Inapanda Daraja Kufikia Kiwango cha Mutawatir kwa Kuzingatia Kuwa Sehemu Yake Imeshatokea?"

January 28, 2013
4214

Swali:

Assalamu alaikum wa rahmatullahi wa barakatuh, kuna hadithi ambazo ni dhanni ath-thubut tunazozitumia kama dalili tunapozungumza na watu kueneza fikra ya Uislamu na kufurahishwa na bishara ya Mtume (saw) kama hadithi ya:

تَكُونُ النُّبُوَّةُ فِيكُمْ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ... ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ نُبُوَّةٍ

"Utume utakuwepo kati yenu kwa muda ambao Mwenyezi Mungu atapenda uwepo... kisha kutakuwa na Khilafah kwa njia ya Utume."

Swali ni: Hadithi hii ni dhanni na inazungumzia hali za kisiasa zinazoipitia Umma. Kutokana na maana ya hadithi, tumeona kuwa Mtume (saw) amegawanya hali hizi katika tano (Utume - Khilafah Rashidah - Ufalme wa kung’ang’ania - Utawala wa kijabari - Khilafah Rashidah). Tunapoona kuwa sehemu nne kati ya tano za hadithi hiyo zimeshapita kwa Umma, je, hadithi hii haipandi hadi kufikia daraja ya mutawatir kwa kuzingatia kuwa sehemu yake imeshatokea?

Jibu:

Hakika hadithi ambayo iko katika maana ya utendaji kazi (amal) inatosha, iwe ni mutawatir au dhanni. Maadamu hadithi ni sahihi, basi inasukuma kuelekea kwenye utendaji kazi kwa nguvu kulingana na kile ilichobeba katika faradhi.

Kwa mfano hadithi:

لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ، فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا، وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ

"Hakika Constantinople itafunguliwa (itakombolewa), amiri wake ni amiri bora zaidi, na jeshi lake ni jeshi bora zaidi." (Imepokelewa na Ahmad)

Licha ya kuwa ni habari (habar), lakini iko katika maana ya utendaji kazi. Ndio maana kila kiongozi wa Kiislamu alikuwa na hamu ya kuhakikisha kuwa hadithi hiyo inatimia kupitia mikono yake. Hivyo, majeshi mengi yalitumwa kwenda Constantinople hadi Mwenyezi Mungu akatunuku ukombozi huu kupitia kwa "Muhammad al-Fatih". Na mfano wa hadithi hii ni ile ya kupigana na dola ya Kiyahudi na kuiondoa... Kadhalika hadithi ya Khilafah ijayo kwa njia ya Utume. Hivyo basi, kutoathiriwa kwa jambo hili kwa kuwa kwake mutawatir au si mutawatir maadamu ni hadithi sahihi. Sisi tunaharakisha mwendo ili itimie kupitia mikono yetu InshaAllah, na tunaiombea kheri, na tuna utulivu wa kutokea kwake iwe ni sasa au baadaye, wala hatujichoshi kwa kuzama ndani ya undani wake ili kujua utawatir wake au uahad wake.

Pamoja na hayo yote, kutokea kwa sehemu ya hadithi huongeza utulivu wa kutimia kwa sehemu iliyobaki ya hadithi, kama vile kufunguliwa kwa Roma baada ya kutimia kwa ukombozi wa Constantinople, ambapo ukombozi wa miji hiyo miwili ulitajwa katika hadithi nyingine ya Mtume (saw). Lakini kama nilivyokutajia awali, kwa kuwa hadithi iko katika maana ya utendaji kazi, hakuna haja ya kuingia kwa ndani kuhusu utawatir wake kwa sababu hadithi sahihi ya dhanni inatosha kwa ajili ya kuifanyia kazi, kuisadikisha, kupata utulivu, na kufurahia kutimia kwake. Hivyo Muislamu ana pupa ya kushinda fadhila hii.

Ama kauli yako "maadamu sehemu yake imeshatimia, je, tuihesabu kuwa ni mutawatir?..." Jibu ni kwamba mutawatir ina masharti katika sanad yanayotegemewa na elimu ya istilahi za hadithi (ilm mustalah al-hadith) ili kuamua utawatir wake. Yaani, utawatir katika elimu hii hautegemei kufuatilia ikiwa hadithi imetimia au la, kwa sababu utawatir unahukumiwa kulingana na sanad ya hadithi na mambo yanayoandamana nayo. Pamoja na hayo, kutimia kwa sehemu za hadithi huongeza utulivu wa nafsi juu ya daraja ya usahihi wake, na huwa kichocheo cha kufanya kazi ili kutimiza sehemu iliyobaki kwa nguvu na bidii. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kutoa taufiki.

Share Article

Share this article with your network