Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Pongezi za Amiri wa Hizb ut-Tahrir, Mwanachuoni Mheshimiwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Kwa Wageni wa Kurasa Zake Katika Maadhimisho ya Kuingia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wa Mwaka 1446 H sawia na 2025 M

March 09, 2025
2311
استمع للمقال

Kwa Umma bora uliotolewa kwa ajili ya watu... Umma wa Kiislamu ambao Mwenyezi Mungu ameuheshimu kwa utii Kwake...

Kwa wabebaji da’wah watukufu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu...

Kwa wageni wa kurasa watukufu wanaoelekea kwenye kheri iliyobebwa ndani yake...

Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,

Alhamdulillah, na swala na salamu zimwendee Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba zake na waliomfuata, na baada ya hapo:

Hakika mimi ninamuomba Yeye (Subhaanahu wa Ta'ala) aukubali funga na kisimamo cha Waislamu, na atusamehe sisi sote madhambi yetu yaliyotangulia kama alivyosema ﷺ katika hadithi iliyopokelewa na Bukhari na Muslim kutoka kwa Abu Hurairah, akisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema:

مَنْ صَامَ رَمَضَانَ، إِيمَاناً وَاحْتِسَاباً، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ

"Mwenye kufunga Ramadhani kwa imani na kutaraji malipo, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia."

Na katika riwaya nyingine kutoka kwa Abu Hurairah (ra): Kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema:

مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَاناً وَاحْتِسَاباً، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ

"Mwenye kusimama (kufanya ibada usiku) mwezi wa Ramadhani kwa imani na kutaraji malipo, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia."

Ndugu Watukufu: Hakika Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta'ala) alifaradhisha funga ya mwezi wa Ramadhani katika mwezi wa Shaaban mwaka wa pili wa Hijra, nao ni mwezi ambao Mwenyezi Mungu aliteremsha ndani yake Qur’an:

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ

"Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa ndani yake Qur'an, kuwa uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi." (Al-Baqarah [2]: 185)

Kadhalika ni mwezi ambao Mwenyezi Mungu ameuheshimu Umma huu kwa ushindi na ukombozi ulio wazi. Vita Vikuu vya Badr vilitokea tarehe kumi na saba ya Ramadhani ambapo washirikina wa Makkah walipata pigo kubwa la kushindwa... Kisha kulifuatia vita vingine vya maamuzi katika mwezi huu mtukufu kuanzia Ukombozi wa Makkah (Fath Makkah) tarehe ishirini ya mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka wa nane wa Hijra, mpaka Vita vya Al-Buwayb (karibu na mji wa Kufa hivi sasa) ambavyo vilikuwa ni sawa na Vita vya Yarmouk dhidi ya Waajemi, ambapo Waislamu walishinda chini ya uongozi wa Al-Muthanna tarehe kumi na mbili ya Ramadhani mwaka wa kumi na tatu wa Hijra. Kisha ukombozi wa Ammouriyah chini ya uongozi wa Al-Mu'tasim tarehe kumi na saba ya Ramadhani mwaka wa mia mbili ishirini na tatu Hijra, na Vita vya Ain Jalut ambavyo Waislamu waliwashinda Watartari tarehe ishirini na tano ya Ramadhani mwaka wa mia sita hamsini na nane Hijra, miongoni mwa ushindi mwingine mwingi katika mwezi huu mtukufu...

Hivyo basi, funga imeambatana na Qur’an Tukufu ambayo haifikiwi na batili mbele yake wala nyuma yake... na funga imeambatana na ukombozi na ushindi... funga imeambatana na Jihadi... funga imeambatana na utekelezaji wa sheria za Mwenyezi Mungu... Na kila mwenye jicho na busara anajua kuwa sheria za Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta'ala) hazitengani moja na nyingine, ziwe ni ibada, jihadi, miamala, maadili na tabia, au mipaka ya kisheria (hudud) na adhabu za makosa ya jinai... zote zinatoka katika chanzo kimoja. Na yeyote anayezingatia aya za Kitabu Kitukufu na nusu za Hadithi Sharifu atalikuta hilo liko wazi kabisa. Muislamu anasoma katika aya za ukumbusho wenye hekima:

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ

"Na simamisheni Swala." (Al-Baqarah [2]: 43)

Kama anavyosoma pia:

وَأَنِ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللهُ

"Na wahukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu." (Al-Ma'idah [5]: 49)

Na anasoma:

كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ

"Mmelazimishwa kufunga." (Al-Baqarah [2]: 183)

Kama anavyosoma:

كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ

"Mmelazimishwa kupigana." (Al-Baqarah [2]: 216)

Hali kadhalika anasoma kuhusu Hija katika hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ:

خُذُوا عَنِّي مَنَاسِكَكُمْ

"Chukueni kutoka kwangu ibada zenu za Hija." (Imepokelewa na Al-Bayhaqi katika Sunan al-Kubra kutoka kwa Jabir).

Pia anasoma kuhusu mipaka ya kisheria (Hudud):

خُذُوا عَنِّي، خُذُوا عَنِّي، قَدْ جَعَلَ اللهُ لَهُنَّ سَبِيلاً، الْبِكْرُ بِالْبِكْرِ جَلْدُ مِائَةٍ وَنَفْيُ سَنَةٍ، وَالثَّيِّبُ بِالثَّيِّبِ جَلْدُ مِائَةٍ، وَالرَّجْمُ

"Chukueni kutoka kwangu, chukueni kutoka kwangu, hakika Mwenyezi Mungu amewawekea njia; bikira kwa bikira ni mijeledi mia na uhamisho wa mwaka mmoja, na aliyewahi kuoa/kuolewa kwa aliyewahi kuoa/kuolewa ni mijeledi mia na kupigwa mawe (rajm)." (Imepokelewa na Muslim kutoka kwa Ubada bin al-Samit).

Na anasoma katika miamala:

البيِّعَانِ بِالخِيَارِ مَا لَمْ يَتَفَرَّقَا - أو قال حتى يتفرقا -

"Wauzaji wawili wana hiyari (ya kuvunja mkataba) madamu hawajatengana – au alisema mpaka watengane." (Imepokelewa na Bukhari kutoka kwa Hakim bin Hizam).

Kama anavyosoma kuhusu bay'ah ya Khalifa:

وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً

"Na yeyote atakayekufa na huku shingoni mwake hana kiapo cha utiifu (bay'ah), basi amekufa kifo cha kijahilia." (Imepokelewa na Muslim kutoka kwa Abdullah bin Umar).

Kwa hivyo basi, Uislamu ni mfumo mmoja usiogawanyika, na ulinganizi kwake ni mmoja kwa ajili ya kuutekeleza katika dola, maisha, na jamii. Hivyo, yeyote anayetenganisha kati ya aya za Mwenyezi Mungu, na akasema kutenganisha dini na maisha, au kutenganisha dini na siasa, hakika amefanya dhambi kubwa na jinai kuu inayomvuta mhusika wake kwenye udhalilifu duniani na adhabu kali Akhera.

Enyi Waislamu: Ninawakumbusha yote hayo katika siku hizi ambapo mashambulizi ya kinyama ya Mayahudi yameongezeka katika Ukingo wa Magharibi pamoja na Gaza. Wameshtushwa na ushujaa wa watu wa Gaza; miezi mingi imepita bila dola haramu la Kiyahudi kupata mafanikio yoyote iliyokuwa ikidai dhidi ya watu wa Gaza. Hivyo lilipoteza mwelekeo, na badala ya kupigana ana kwa ana na kundi lile la waumini wenye silaha zao duni wakati wao wakiwa na silaha nzito za Amerika na nchi za Magharibi, badala yake waligeukia kuua wanawake na watoto ili wapate 'mafanikio' ya kuzungumzia!

Kisha uchokozi wa Mayahudi ukaenea mpaka Lebanon na Syria, wakishambulia huku na kule bila kukumbana na yeyote wa kuwarudisha nyuma. Wanashambulia Lebanon na kukaa katika sehemu zake... na wanashambulia Syria na kukaa katika sehemu zake mbele ya macho na masikio ya watawala katika nchi za Waislamu. Na badala ya watawala kuyaongoza majeshi ya Waislamu ili kupigana nao mapambano yatakayowatawanya Mayahudi na walioko nyuma yao, tunawaona wakisaini mikataba nao mmoja baada ya mwingine bila ya kumuonea haya Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na Waumini!

Enyi Waislamu: Hakika kupigana na Mayahudi, kuwaua na kuiondoa dola yao ni jambo ambalo hapana shaka litatokea chini ya uongozi wa Khalifa mwongofu, mujahid, baada ya huu utawala wa kidikteta (Mulkan Jabriyyah) na watawala vibaraka. Bishara ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ haitachelewa wakati wake kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, ikiwa ni uthibitisho wa hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ iliyopokelewa na Ahmad:

ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ. ثُمَّ سَكَتَ

"Kisha utakuwepo utawala wa kidikteta, na utakuwepo kwa muda anaoutaka Mwenyezi Mungu, kisha Atauondoa Atakapotaka Auondoe, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume. Kisha akanyamaza."

Pia ni kusadikisha hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu iliyopokelewa na Muslim:

لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ...

"Hakika mtapigana na Mayahudi na mtawaua..."

Mwishoni, kama tunavyopaswa kuwa na pupa ya kufunga ili Mwenyezi Mungu aturidhie na kutusamehe madhambi yetu yaliyotangulia, basi lazima tuwe na pupa vivyo hivyo kufanya kazi kwa ajili ya kuanza tena maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashidah. Ili tuwe miongoni mwa waliofuzu duniani kwa kutekeleza sheria za Mwenyezi Mungu, tukijikinga chini ya bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ, bendera ya Al-Uqab, bendera ya La ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah. Na tuwe miongoni mwa waliofuzu Akhera pia kwa idhini Yake (Subhaanahu wa Ta'ala), tukijikinga katika kivuli Chake siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli Chake. Hivyo tutafuzu katika nyumba zote mbili, na huo ndio ushindi mkuu.

Wassalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Mosi ya Ramadhani 1446 H Ndugu yenu Sawia na 01/03/2025 M Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Share Article

Share this article with your network