Jibu la Swali
Mapinduzi ya Kijeshi Nchini Mali
Swali: Baraza la kijeshi nchini Mali lilitangaza mnamo Alhamisi jioni tarehe 2020/08/27 kuachiliwa kwa Rais Ibrahim Boubacar Keïta, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Anadolu... Hapo awali ilikuwa imetangazwa jioni ya tarehe 2020/08/18 kuwa mapinduzi ya kijeshi yametokea nchini Mali dhidi ya Rais Ibrahim Boubacar Keïta, ambapo yeye na Waziri Mkuu wake Boubou Cissé walikamatwa. Ni nani aliye nyuma ya mapinduzi haya? Na je, yana uhusiano na mzozo kati ya Marekani na Ulaya?
Jibu: Ili picha iwe wazi, tunatathmini mambo yafuatayo:
1- Tunarejelea kile kilichotokea leo na kulinganisha na kile kilichotokea miaka minane iliyopita. Mapinduzi kama haya yalitokea mnamo 2012/03/22 wakati kundi la maafisa wa vyeo vya chini walipofanya mapinduzi dhidi ya Rais Amadou Toumani Touré, ambaye alikuwa amebakiza mwezi mmoja kumaliza muhula wake wa pili wakati huo... Tulibainisha kuwa Marekani ilikuwa nyuma ya mapinduzi hayo, tukisema katika Jibu la Swali tulilotoa tarehe 2012/03/24: ["Yote tuliyoyataja yanaashiria kuwa Marekani ilikuwa nyuma ya mapinduzi yaliyotokea nchini Mali ili kupenya katika nchi hii ya Kiislamu, kupanua ushawishi wake juu yake, na kuchukua nafasi ya Ufaransa—mkoloni wa zamani ambaye bado anadhibiti ushawishi wake huko. Marekani ilitaka kuvuruga mchakato wa uchaguzi uliokuwa unakuja nchini Mali kwa sababu tabaka la kisiasa lilikuwa tiifu kwa Ufaransa. Kwa njia ya mapinduzi haya, inapindua meza dhidi ya wachezaji ambao ni mawakala wa Ufaransa wanaofanya kazi kwa mujibu wa sera za Kifaransa. Hivyo, Mali inaunganishwa na Marekani kupitia udhibiti wake wa harakati za 'kijeshi'."] Na leo inatokea kwamba maafisa wa vyeo vya chini, ambapo mkubwa wao ni Kanali, wamefanya mapinduzi dhidi ya Rais Boubacar Keïta, ambaye alichaguliwa kwa mara ya kwanza tarehe 2013/08/15 na kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili mnamo 2018/08/12. Wanajeshi hao walitokea katika kambi ya "Kati", iliyoko kilomita 15 kutoka mji mkuu, kambi ile ile ambayo waasi wa mwaka 2012 walitokea. Ufaransa, baada ya mapinduzi ya Machi 2012, ilifanikiwa kupata maazimio kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuingilia kati kaskazini mwa Mali, azimio nambari 2071 la tarehe 2012/09/23 na azimio lingine nambari 2085 la tarehe 2012/12/20, kwa lengo la kulinda ukoloni wake kwa kisingizio cha kupambana na Al-Qaeda na makundi ya itikadi kali! Hivyo vikosi vya kimataifa vya wanajeshi 15,000 viliundwa, haswa kutoka Ufaransa na Ulaya, na vikosi vya Afrika ambavyo Ufaransa ilivifanya kuwa kikosi cha pamoja cha Afrika kinachoitwa vikosi vya nchi tano za Sahel (G5 Sahel), ambazo ni Mauritania, Mali, Niger, Burkina Faso, na Chad, ambako ushawishi wa Ufaransa ni mkubwa. Ikafanikiwa kurejesha ushawishi wake baada ya chini ya mwaka mmoja na nusu tangu mapinduzi ya 2012 kupitia kuchaguliwa kwa Ibrahim Boubacar Keïta mnamo 2013/08/15, kisha akachaguliwa tena kwa mara ya pili mnamo 2018/08/12! Ingawa Marekani haina nguvu katika tabaka la wananchi kama Ufaransa, lakini ina njia za kuingilia jeshini ambazo zimeiwezesha kufanikisha mapinduzi ya sasa kwa nguvu zaidi kuliko mapinduzi yake ya kwanza mwaka 2012! Baada ya kuanguka kwa mapinduzi yake ya kwanza yaliyomalizika chini ya mwaka mmoja na nusu baada ya kutokea, ilianza kufanya kazi ya kupata mawakala katika tabaka la kisiasa na mashirika ya kiraia, na si jeshini pekee, katika jaribio la kuwa na msingi wa kijamii wa kusaidia mapinduzi yake ya sasa...
2- Kiongozi mpya wa mapinduzi, Kanali Assimi Goïta, mnamo 2020/08/19 alijitambulisha kama mwenyekiti wa kile alichokiita "Kamati ya Kitaifa ya Wokovu wa Watu" nchini Mali. Alionekana kwenye televisheni jioni ya Jumanne 18/08/2020 akiwa na kundi la maafisa waliofanya mapinduzi. Waasi hao walimpeleka Rais wa Jamhuri Keïta, Waziri Mkuu wake Cissé, mawaziri, na maafisa wengine wapatao 17 gerezani. Kisha wanajeshi walimwonyesha Keïta kwenye televisheni akitangaza kujiuzulu kwake, ambapo alisema katika hotuba yake: ("Hataki damu imwagike ili abaki madarakani"... Reuters 2020/08/19). Kanali Ismaël Wagué, msemaji wa kundi la waasi, alisema ("...nchi yetu inazama katika fujo na ukosefu wa usalama, na hii inatokana kwa kiasi kikubwa na makosa ya watu wanaowajibika na hatima yake"... Reuters 2020/08/19). Kanali Ismaël Wagué pia alisema ("Tutaunda baraza la mpito lenye rais wa mpito ambaye atakuwa mwanajeshi au raia; tuko katika mawasiliano na mashirika ya kiraia, vyama vya upinzani, walio wengi na kila mtu ili kujaribu kupanga mpito huu... Na kwamba Kamati ya Kitaifa iliyoundwa na baraza la mpito inajumuisha wanajeshi 6 na raia 18, na itafanya kazi kama chombo cha mpito cha kutunga sheria, huku rais wa baraza akichaguliwa na wanachama wake"... Al Jazeera 2020/08/21). Hapa inaonekana kuwa wanajeshi walipanga mapinduzi hayo pamoja na wanasiasa na makundi ya upinzani, yakiwemo yale yanayoitwa mashirika ya kiraia kama vyama vya wafanyakazi na vyama mbalimbali, ambavyo vimeanza kufanya kazi za kisiasa huku nchi za kikoloni zikizifadhili na kununua utii wao. Hivyo inaonekana kuwa Marekani imefanikiwa kupata wengi wao ili kumwangusha Keïta kabla ya kumaliza muhula wake wa pili, katika jaribio la Marekani la kuhakikisha mafanikio ya mawakala wake katika siku zijazo huku ikilenga jeshi na kupata mawakala miongoni mwa maafisa wake.
3- Inaonekana kuwa Marekani safari hii ilijaribu kufanya mapinduzi yake yawe na misingi ya wananchi, ndiyo maana iliyatayarisha tangu mwanzo wa Juni uliopita, ambapo maandamano yalizuka yakishirikisha maelfu ya waandamanaji katika mitaa ya Bamako, mji mkuu wa Mali, yakimtaka Rais Keïta kujiuzulu na kumtuhumu yeye na serikali yake kwa ufisadi, upendeleo, huduma duni za jamii, makosa katika uchaguzi, kutokuwa na uwezo wa uongozi, na kushindwa kupambana na kile wanachokiita itikadi kali na ugaidi. Vyama fulani viliunda muungano uliojulikana kama muungano wa Juni 5 au M5. Nouhoum Togo, mkuu wa muungano wa Juni 5 aliyeongoza maandamano hayo, alisema ("Anashirikiana na wanajeshi waliochukua mamlaka," na aliyataja vikwazo vya jumuiya ya ECOWAS kama "majibu yaliyopitiliza yaliyosababishwa na hofu ya baadhi ya viongozi wake kwamba mapinduzi hayo yatasababisha machafuko ya kisiasa katika nchi zao." Alizungumza na "kupongeza mapinduzi ya kijeshi" na kuyaelezea kama "yamekuja kukamilisha safari ya watu wa Mali na matamanio yao ya kuelekea katika nchi ya kidemokrasia, kiraia, na isiyofungamana na dini (secular)"... Al Jazeera 2020/08/21). Inaonekana kwamba maandamano nchini Mali hayakuwa ya ghafla, bali yaliongozwa na mawakala wanaobeba fikra za mkoloni za demokrasia, mfumo wa kiraia na usekulari. Wameungana na wanajeshi na kuunga mkono mapinduzi. Marekani inalenga kuifanya Mali kuwa kitovu na chanzo cha maambukizi ya mapinduzi katika eneo hilo ili kuangusha tawala tiifu kwa Ufaransa na Uingereza katika Afrika Magharibi na Kati.
4- Kisha mjumbe wa Marekani katika eneo la Sahel, J. Peter Pham, aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kufuatia mapinduzi nchini Mali: ("Marekani inapinga mabadiliko yote ya serikali yaliyo kinyume na katiba" na akasema "Marekani imesitisha ushirikiano wa aina zote na jeshi la Mali mpaka hali ya kisiasa itakapokuwa wazi baada ya maafisa kumwondoa Rais Ibrahim Keïta." Aliongeza, "uamuzi wa kama kile kilichotokea hivi karibuni kitatajwa rasmi kama mapinduzi unapaswa kutolewa baada ya mapitio ya kisheria"... Reuters 2020/08/22). Kutokana na hayo, inaonekana kuwa Marekani hailaani mapinduzi na waasi, na maneno ya mjumbe wake kuhusu kupinga mabadiliko yasiyo ya kikatiba ni maneno ya jumla yasiyo na uhusiano na mapinduzi haya. Badala yake, iliunga mkono mapinduzi ya Sisi nchini Misri na mapinduzi ya kijeshi nchini Sudan na haikuyaona kama mapinduzi kwa sababu yalitengenezwa nayo. Na vivyo hivyo katika mapinduzi ya Mali, ambapo ilisema kupitia mjumbe wake kuwa itafanya mapitio ya kisheria kuchunguza ikiwa kilichotokea ni mapinduzi au la!! Hii inaashiria kuwa ilikuwa nyuma ya mapinduzi hayo. Hili linaungwa mkono na kile kilichotajwa na tovuti ya Al Jazeera ya Qatar mnamo 2020/08/21 ("Marekani hutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wanajeshi wa Mali, akiwemo baadhi ya maafisa walioongoza mapinduzi dhidi ya Keïta"). Walioongoza mapinduzi ni miongoni mwa wale waliofunzwa na Marekani na kuwapata kama mawakala wake. Hali hii ni sawa na ile ya mapinduzi ya mwaka 2012, kama tulivyotaja katika jibu la swali tulilotoa kuhusu suala hili mnamo 2012/03/24: ("Tovuti ya Al-Asr mnamo 2012/03/24 ilinukuu vyanzo vya Marekani vilivyofahamishwa kuwa mwanadiplomasia mmoja wa Marekani aliyeomba jina lake lisitajwe aliiambia vyombo vya habari akisema: 'Kiongozi wa mapinduzi, Kapteni Amadou Sanogo, alikuwa amechaguliwa miongoni mwa wasomi wa maafisa na ubalozi wa Marekani kupata mafunzo ya kijeshi ya kupambana na ugaidi nchini Marekani.' Aliongeza kuwa 'Sanogo alisafiri mara kadhaa kwenda Marekani kwa misheni maalum...'"). Marekani inapiga hatua ile ile iliyoipiga mwaka 2012 kupitia mapinduzi ili kuwafukuza Wazungu na kuchukua nafasi yao ili ijitenge na ukoloni wa nchi hiyo. Lakini safari hii, huenda mwelekeo wake ukawa mkubwa kuliko awali, kwani imeanza kupata katika vyama vya kisiasa na mashirika ya kiraia tabaka la kisiasa mkabala na tabaka la kisiasa linaloifuata Ufaransa.
5- Maoni ya Ufaransa, ambayo ina ushawishi huko, yalikuja yakilaani vikali, kwani ilipatwa na taharuki. Urais wa Ufaransa ulisema ("Rais wa nchi Macron anafuatilia kwa karibu hali hiyo na analaani jaribio la uasi linaloendelea"... AFP 2018/08/18). Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Le Drian alisema: ("Ufaransa inalaani kwa maneno makali tukio hili hatari"... Al Hurra 2020/08/19). Macron alisema tarehe 2020/08/20 wakati wa mkutano wake na Kansela wa Ujerumani Merkel kujadili maendeleo nchini Mali: ("Ufaransa na Ujerumani zinalaani mapinduzi yaliyotokea Mali na zinataka nchi hiyo irejee haraka iwezekanavyo katika utawala wa kiraia. Haipasi kuwepo kwa kitu chochote kitakachozuia umakini dhidi ya vitendo vya ghasia vinavyofanywa na wanamgambo wa Kiislamu katika eneo la Sahel," kwa mujibu wa maneno yake. Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Florence Parly alisema "Ufaransa itaendelea na operesheni zake za kijeshi nchini Mali dhidi ya wanamgambo licha ya kuangushwa kwa rais wa nchi hiyo siku mbili zilizopita katika mapinduzi ya kijeshi"... Reuters 2020/08/20). Kauli hizi zinaonyesha jinsi Ufaransa ilivyokasirishwa na mapinduzi hayo, jambo linalothibitisha kuwa mapinduzi haya yalikuwa yanalenga ushawishi wake huko huku ikipora utajiri wa Mali na nchi jirani kwani ni tajiri wa rasilimali nyingi za madini adimu. Inaichukulia Mali kama eneo muhimu la kimkakati la kulinda ushawishi wake Afrika Magharibi, kwani inaunda na nchi za Sahel eneo moja ambalo likiondolewa katika nchi moja, huenda maambukizi yakahamia nchi nyingine. Ufaransa inafanya kazi kuimarisha uwepo wake wa kijeshi unaofikia takriban wanajeshi 5,100 kwa kutumia vikosi vya Ulaya, na inasaidiwa na Ujerumani ambapo nchi hiyo inashiriki pamoja na Ufaransa kwa wanajeshi wapatao 1,100 chini ya kile kinachoitwa operesheni ya "Barkhane". Imekimbilia nchi za Ghuba, ikiwemo Imarati, kufadhili kikosi cha pamoja cha Afrika, na Uingereza inashiriki kwa takriban wanajeshi 250 na helikopta tatu. Umoja wa Ulaya unashiriki kwa takriban wanajeshi 620. Marekani inakataa kufadhili kikosi cha "Barkhane" kwa fedha na vifaa, na inasema inachangia kupitia taarifa za kijasusi na uangalizi kwa msaada wa ndege zake zisizo na rubani (drones).
6- Umoja wa Afrika na jumuiya ya ECOWAS zililaani mapinduzi hayo. Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, aliandika kwenye Twitter: "Nalaani vikali kukamatwa kwa Rais Ibrahim Keïta, Waziri Mkuu na wanachama wengine wa serikali ya Mali na naitaka waachiliwe mara moja." Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), yenye wanachama 15, ilikubaliana kufunga mipaka yake na Mali, kusitisha mtiririko wote wa fedha nchini humo, na kuifukuza Mali kutoka kwa vyombo vyote vya kufanya maamuzi katika jumuiya hiyo. Ujumbe kutoka jumuiya hii ulitembelea Mali tarehe 2020/08/22 na kukutana na viongozi wa mapinduzi. Mkutano huo ulitarajiwa kudumu kwa saa moja na nusu lakini ulidumu kwa dakika 20 tu, jambo linaloonyesha kufeli kwa ujumbe wa kundi hili uliokuja kuwashawishi viongozi wa mapinduzi kumrejesha Keïta na serikali yake madarakani, kama vilivyoripoti mashirika ya habari. Lakini viongozi wa mapinduzi walikataa hilo na kushikilia mapinduzi yao, wakisema kuwa mazungumzo na ujumbe wa jumuiya hiyo yanaweza kufanyika kuhusu muda wa kipindi cha mpito. Ikumbukwe kwamba Umoja wa Afrika na jumuiya ya ECOWAS vinatawaliwa na mawakala wa Ulaya, haswa Afrika Magharibi.
7- Muhtasari ni kwamba Marekani inapambana na Ulaya, hususan Ufaransa na Uingereza, barani Afrika na haswa katika nchi za Kiislamu ikiwemo Mali. Mali ni nchi ya Kiislamu inayong'ang'aniwa na wakoloni ili kupanua ushawishi wao na kuweza kupora utajiri wake, kwani Ufaransa kwa sasa ina sehemu kubwa ya utajiri huo. Vilevile, wakoloni wanang'ang'ania Mali kutokana na eneo lake la kimkakati Afrika Magharibi ambalo linaunda eneo moja na nchi za Sahel. Wanawaacha watu wake Waislamu wakiteseka kwa umaskini, uhitaji na maradhi, huku watawala mawakala wakimhakikishia mkoloni kile anachotaka ili wapate kiti chenye hitilafu huku wakiwa dhalili. Mali ni nchi dhaifu inayokabiliwa na ukoloni kwani hakuna nguvu ya Waislamu inayoweza kuilinda dhidi ya uvamizi wa wakoloni, ambapo wanatoa maazimio ya kuingilia kijeshi moja kwa moja kwa visingizio dhaifu. Hakuna nguvu ya Kiislamu kama dola ya Khilafah Rashidah inayongojewa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu ili kukabiliana na uvamizi wao na kuwapa somo ambalo hawatolisahau. Hivyo, kufanya kazi ya kusimamisha dola hii ni miongoni mwa wajibu mkubwa zaidi, kwani ndani yake mna utukufu, ushindi na kinga dhidi ya kila kafiri jabari... Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema:
وَإِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ
"Hakika Imamu ni ngao, ambapo hupiganwa nyuma yake na hukingiwa kwayo." (Imepokelewa na Muslim)
13 Muharram Al-Haram 1442 H 2020/09/01 M