Silsila ya Majibu ya Mwanachuoni Mtukufu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa Maswali ya Wafuasi wa Ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi"
Jibu la Swali
Dua ya Kuangamiza Chombo cha Kiyahudi
Kwa Agus Trisa
Swali:
assalamu alaikum wa rahmatullahi wa barakatuhu May Allah protect you wherever you are I want to ask you about this noble verse Allah Subhanahu Wa Ta'ala says: وَاِذَا سَاَلَكَ عِبَادِيْ عَنِّيْ فَاِنِّيْ قَرِيْبٌ ۗ اُجِيْبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ اِذَا دَعَانِ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِيْ وَلْيُؤْمِنُوْا بِيْ لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُوْنَ
Is it true that God answers all human prayers?
Is there a prayer that God does not answer?
Some people ask, we have prayed for Israel to be destroyed by Allah, but why are they still strong and continuing to attack Gaza?
Thank you for your answer, may Allah reward you with the best reply wassalamu alaikum wa rahmatullahi wa barakatuhu
Tafsiri ya Swali:
Amani iwe juu yenu na rehema za Allah na baraka zake, Allah akulinde popote ulipo.
Nataka kukuuliza kuhusu aya hii tukufu, Allah (swt) anasema:
وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِي فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ
"Na waja Wangu watakapokuuliza khabari Zangu, basi mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya muombaji anapo Niomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka." (QS. Al-Baqarah [2]: 186)
Je, ni kweli kwamba Allah anajibu kila dua ya mwanadamu?
Je, kuna dua ambayo Allah haijibu?
Baadhi ya watu wanauliza kuwa wameomba dua ili Allah akiangamize chombo cha Kiyahudi, lakini mbona chombo hicho bado kina nguvu na kinaendelea na uchokozi wake dhidi ya Gaza?
Nakushukuru kwa jibu lako, na namuomba Allah akujazi kheri kwa jibu lako zuri.
Wassalamu alaikum wa rahmatullahi wa barakatuhu.
Jibu:
Wa Alaikumus Salaam wa Rahmatullahi wa Barakatuh.
Kuna mambo ambayo ni lazima yajulikane kuhusu dua:
1- Hakika muumini anapomuomba Allah kwa moyo mkweli, dua ambayo haina kuvunja undugu ndani yake, basi Allah (swt) huijibu kwa mojawapo ya njia tatu, kama ilivyo katika Kitabu cha Allah (swt) na Sunnah za Mtume wake ﷺ:
Hakika Allah (swt) anajibu dua ya muombaji anapomuomba, na anamjibu mwenye dhiki anapomuomba;
وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ "Na Mola wenu amesema: Niombeni Nitakuitikieni." (QS. Ghafir [40]: 60)
وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ "Na waja Wangu watakapokuuliza khabari Zangu, basi mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya muombaji anapo Niomba." (QS. Al-Baqarah [2]: 186)
أَمَّنْ يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ "Au nani yule anayemuitikia mwenye dhiki anapomwomba, na akaiondoa dhiki." (QS. An-Naml [27]: 62)
Hata hivyo, kuijibu dua kuna uhalisia wa kisheria uliowekwa wazi na Mtume ﷺ:
«مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَدْعُو اللهَ عَزَّ وَجَلَّ بِدَعْوَةٍ لَيْسَ فِيهَا إِثْمٌ وَلَا قَطِيعَةُ رَحِمٍ، إِلَّا أَعْطَاهُ اللَّهُ بِهَا إِحْدَى ثَلَاثِ خِصَالٍ: إِمَّا أَنْ يُعَجِّلَ لَهُ دَعْوَتَهُ، وَإِمَّا أَنْ يَدَّخِرَهَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ، وَإِمَّا أَنْ يَصْرِفَ عَنْهُ مِنَ السُّوءِ مِثْلَهَا. قَالُوا: إِذًا نُكْثِرُ. قَالَ: اللهُ أَكْثَرُ»
"Hakuna Muislamu yeyote anayemuomba Allah (swt) kwa dua ambayo haina dhambi ndani yake wala kuvunja undugu, isipokuwa Allah humpa kwayo mojawapo ya mambo matatu: Ama amharakisishie dua yake, au amuekee akiba kwa ajili yake Akhera, au amuepushie ubaya mfano wake. Wakasema: Basi tutazidisha. Akasema: Allah ni mwingi zaidi." (Imetolewa na Ahmad), na pia:
«لَا يَزَالُ يُسْتَجَابُ لِلْعَبْدِ مَا لَمْ يَدْعُ بِإِثْمٍ أَوْ قَطِيعَةِ رَحِمٍ مَا لَمْ يَسْتَعْجِلْ. قِيلَ: يَا رَسُولَ اللهِ، مَا الِاسْتِعْجَالُ؟ قَالَ: يَقُولُ قَدْ دَعَوْتُ وَقَدْ دَعَوْتُ فَلَمْ أَرَ يَسْتَجِيبُ لِي فَيَسْتَحْسِرُ عِنْدَ ذَلِكَ وَيَدَعُ الدُّعَاءَ»
"Mja ataendelea kujibiwa maadamu haombi dhambi au kuvunja undugu, maadamu hafanyi haraka. Ikasemwa: Ee Mtume wa Allah, nini maana ya kufanya haraka? Akasema: Anasema nimeomba na nimeomba lakini sijaona nikijibiwa, kisha anakata tamaa wakati huo na kuacha dua." (Imetolewa na Muslim).
Hivyo basi, tunamuomba Allah (swt), na ikiwa sisi ni wakweli, wenye ikhlasi na watiifu, basi tunakuwa na yakini ya kujibiwa kwa maana aliyoibainisha Mtume wa Allah ﷺ.
2- Hakika dua pekee siyo njia ya kisheria (Tariqah Shar'iyyah) ya kufikia lengo katika hali zote.. Dua ni jambo lililopendekezwa (Mandub), lakini siyo njia ya kupata ushindi katika vita au kusimamisha Dola... n.k. Kwani Mtume ﷺ aliandaa jeshi katika vita vya Badr, akapanga wanajeshi kila mmoja katika nafasi yake, na akawaandaa maandalizi mazuri ya vita, kisha Mtume ﷺ akaingia katika kibanda chake akimuomba Allah ushindi na akazidisha dua mpaka Abu Bakr (ra) akamwambia: "Baadhi ya haya yanakutosha ee Mtume wa Allah." (Sirah Ibn Hisham 2/626). Kwa hiyo dua haimaanishi kuacha kuchukua sababu (al-akhdhu bil-asbaab), bali huambatana nazo.
Pia, yule anayependa Khilafah isimamishwe upya, hapaswi kutosheka tu na kumuomba Mola wake ili kufanikisha hilo, bali anafanya kazi pamoja na wale wanaofanya kazi ya kuisimamisha, na anamuomba Allah msaada katika hilo na haraka ya kulifanikisha, na anang’ang’ania katika dua kwa ikhlasi kwa ajili ya Allah huku akichukua sababu.
Na hivi ndivyo ilivyo katika matendo yote; mtu anafanya kazi kwa ikhlasi kwa ajili ya Allah na ukweli pamoja na Mtume ﷺ, kisha anaomba na kung’ang’ania katika dua, na Allah ni Msikivu mwenye Kuitikia.
3- Tayari tulishajibu swali kama hili mnamo tarehe 4 Dhul-Qi'dah 1432 H - 01/10/2011 M, ambapo ilielezwa hivi:
[...……
- Ama dua pamoja na kuchukua sababu, ina athari katika matokeo, na hivi ndivyo alivyokuwa Mtume ﷺ, na maswahaba wake (ra). Mtume ﷺ aliandaa jeshi na akaingia katika kibanda chake akiomba, na Waislamu katika vita vya Qadisiyah waliandaa zana za kuvuka mto huku Saad (ra) akielekea kwa Allah akiomba... Na hivi ndivyo waumini wakweli wanavyoandaa zana na kuanza kuomba. Hivyo anayetafuta riziki anafanya juhudi na kutaabika huku akiomba, na mwanafunzi anasoma na kujitahidi huku akimuomba Allah (swt) mafanikio, na jambo hilo huwa na athari katika matokeo kwa idhini ya Allah.
Imekuja katika kitabu Al-Mafahim ukurasa wa mwisho 58: (Isipokuwa lazima ijulikane kwamba, hata kama kitendo ambacho kimeashiriwa na njia (Tariqah) ni kitendo cha kimaada chenye matokeo yanayohisika, lakini ni lazima kitendo hiki kiongozwe na amri na makatazo ya Allah, na ikusudiwe katika kukiendesha kwa amri na makatazo hayo radhi za Allah. Vilevile ni lazima muislamu atawaliwe na utambuzi wa uhusiano wake na Allah (swt), hivyo ajikurubishe Kwake kwa swala, dua, kusoma Qur'ani na mfano wake. Na ni lazima Muislamu aamini kwamba ushindi unatoka kwa Allah. Na kwa ajili hiyo, hapana budi kuwa na ucha Mungu uliokita vifuani ili kutekeleza hukumu za Allah, na hapana budi kuwa na dua, na hapana budi kumdhukuru Allah, na hapana budi kudumisha mafungamano na Allah wakati wa kufanya matendo yote). Ni wazi kutokana na hayo umuhimu wa dua kuambatana na kuchukua sababu katika matendo yote ya muumini, na umuhimu huo umeongezeka kwa kurudiwa kwa maneno "hapana budi" kuashiria umuhimu mkubwa wa kuoanisha matendo yote na dua pamoja na kudumisha mafungamano na Allah...
- Hakika kutumia dua pamoja na kuchukua sababu ndivyo alivyokuwa Mtume ﷺ, maswahaba wake na waumini, na pindi vinapoambatana huwa vina athari katika matokeo kwa idhini ya Allah, na kuvitumia pamoja hakupingani na njia ya Uislamu, bali kinachopingana nayo ni kutosheka na dua pekee bila ya njia iliyobainishwa na maandiko kwa ajili ya kutekeleza fikra ya Kiislamu...].
Kwa hivyo, kile kilichokuja katika swali lako kuhusu dua ya kuangamiza chombo cha Kiyahudi... hili halitosheki na dua pekee, bali ni lazima kuwepo na jeshi la Dola litakalopigana na Wayahudi likiambatana na dua kama alivyokuwa Mtume wa Allah ﷺ na maswahaba wake (ra), na Allah ndiye wa kuombwa msaada.
Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah
04 Rabi' al-Akhar 1446 H Sawa na 07/10/2024 M
Link ya jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir (Allah amuhifadhi) kwenye: Facebook