Jawabu la Swali:
Mashambulizi ya Anga ya Marekani nchini Libya
Swali: Mashambulizi ya anga ya Marekani yanaendelea katika mji wa Sirte kwa ombi la serikali ya Sarraj. Vyanzo vya kijeshi vilivyo karibu na vikosi vya Baraza la Urais huko Sirte vimethibitisha kuwa ndege za Marekani jana Jumatatu zilitekeleza mashambulizi nane dhidi ya ngome za ISIS mjini humo (Al-Arabiya.net, 2016/8/9). Lakini inajulikana kuwa serikali ya Sarraj nchini Libya iliundwa kufuatia makubaliano ya Skhirat nchini Morocco, na mchezaji mkuu katika makubaliano haya alikuwa Ulaya, hususan Uingereza. Sera ya serikali hii, kulingana na sera ya Ulaya, ilikuwa ni kukataa uingiliaji wa kijeshi wa Marekani. Kwa nini basi wamekubali sasa? Je, sera ya Sarraj imebadilika kutoka kwenye mrengo wa Ulaya? Allah akujaze heri.
Jibu: Hakika serikali ya Sarraj bado inafuata mrengo wa Ulaya, na kwa usahihi zaidi mrengo wa Uingereza. Kukubali kwake uingiliaji wa kijeshi wa Marekani hakumaanishi kuwa imekuwa mfuasi wa kisiasa wa Marekani, bali ilisukumwa kufanya hivyo na Uingereza kama hatua ya kuivutia Marekani ili kuufanya bunge la Tobruk kuikubali serikali ya Sarraj. Hii ni kwa sababu Marekani, licha ya kuikubali serikali ya Sarraj kidhahiri kutokana na upandishaji chati wa kisiasa katika maoni ya umma uliofanywa na Uingereza, bado Marekani inaipinga kivitendo na kuijengea matatizo kupitia kwa Haftar na kundi lake, na haikuufanya bunge la Tobruk kuikubali serikali hiyo. Hivyo, hatua ya Sarraj ilichochewa na Uingereza kuomba uingiliaji wa kijeshi wa Marekani ili kuivutia Marekani kwa "tumaini" kwamba itaufanya bunge la Tobruk kuikubali serikali ya Sarraj. Ili kufafanua hili, tunapitia mambo yafuatayo:
1- Serikali ya Sarraj iliundwa kwa uungaji mkono wa Ulaya, hususan Uingereza, ambayo ilifanikiwa kufanya makubaliano ya Skhirat mnamo 2015/12/17. Uingereza ilikuwa ikizuia uingiliaji wa kijeshi nchini Libya kwa sababu haikuhitaji uingiliaji huo kwani inadhibiti mazingira ya kisiasa na serikali iko chini yake. Ilitoa maazimio ya kimataifa kuzuia uingiliaji wa kijeshi, lakini Marekani ilikuwa iking'ang'ania kuingilia kati na ilitekeleza mashambulizi ya peke yake tangu Novemba mwaka jana, na shambulio lake la mwisho lilikuwa mnamo Februari mwaka huu ambapo liliua watu 49 katika kambi nchini Libya, wengi wao wakiwa ni watu wa Tunisia. Hii ni kwa sababu uwepo wa Marekani ni mdogo nchini Libya, hivyo inataka kutegemea uingiliaji wa kijeshi na imemuunga mkono kibaraka wake Haftar kufuata mrengo huu. Marekani imekiri udhaifu wa uwepo wake nchini Libya, ambapo msemaji wa Pentagon, Peter Cook, mnamo 2016/5/17 alisema: "Marekani bado ina uwepo mdogo nchini Libya ambao kazi yake ni kujaribu kutambua pande na makundi ambayo yanaweza kuisaidia Marekani katika vita vyake dhidi ya ISIS" (Al-Shorouk ya Tunisia, 2016/5/17). Kikwazo cha kurahisisha kazi ya serikali ya Sarraj kilikuwa ni sharti la Marekani kwamba Haftar awe na nafasi ya msingi katika jeshi na kisha bunge la Tobruk liitambue serikali ya Sarraj, lakini makubaliano ya Skhirat yanasema kinyume na hivyo. Mjumbe wa kimataifa amekariri jambo hili katika matukio kadhaa; mjumbe wa kimataifa nchini Libya, Martin Kobler, mnamo 2016/8/7 kwenye televisheni ya Al-Ghad alisema kuwa "makubaliano ya kisiasa yanatamka kuwa Baraza la Urais ndilo Amiri Jeshi Mkuu wa jeshi la Libya na pande zote za Libya lazima ziheshimu makubaliano haya..." Pia alidai kufanyika kwa mkutano wa bunge la Libya na wanachama wake wote ili kuikubali serikali ya maridhiano ya kitaifa, akibainisha kuwa bunge lilikubali makubaliano ya kisiasa baada ya kuweka pingamizi kwenye kipengele kimoja, nacho ni Kipengele cha Nane kinachohusiana na nafasi ya Haftar. Kipengele hicho kinasema: "Mamlaka yote ya nafasi za juu za kijeshi, kiraia na usalama yaliyoainishwa katika sheria za Libya yatahamishiwa kwa Baraza la Urais wa Mawaziri mara tu baada ya kutia saini makubaliano..." Na kipengele hiki ndicho kiini cha mgogoro.
2- Uingereza iligundua kuwa Marekani inataka uingiliaji wa kijeshi na tayari inautekeleza. Tovuti ya Africa News Gate mnamo 2016/1/8 iliripoti kuwa "Kamandi ya kijeshi ya Marekani barani Afrika (AFRICOM) ilitangaza rasmi uingiliaji wake wa kijeshi nchini Libya kulingana na mpango wa miaka 5, unaolenga kuimarisha udhibiti dhidi ya makundi ya kigaidi barani Afrika, hasa nchini Libya." Kwa hivyo, Marekani iliamua sera ya kuanzisha mashambulizi ya kijeshi au uingiliaji wa kijeshi bila azimio la kimataifa, kwani haikufikia inachotaka kupitia hatua za kisiasa za moja kwa moja. Baada ya hapo, White House mnamo 2016/1/28 ilitangaza kuwa "Rais Obama aliongoza mkutano wa Baraza la Usalama wa Kitaifa uliojitolea kujadili hali ya Libya. Alisisitiza kuwa Marekani itaendelea kushambulia ISIS katika nchi yoyote ikiwemo Libya ikiwa ni lazima." Pamoja na hayo, Marekani inajali upande wa kisheria kuwa uingiliaji wake uwe kwa ombi la serikali ya Sarraj kama kisingizio cha kisheria. Hivyo, Uingereza ilimuamuru Sarraj aiombe Marekani kuingilia kati ili kuupa uingiliaji wake sifa ya kisheria, na kisha kuanzia kwenye "huduma" hii anayoitoa kwa Marekani, iwe kama tumaini kutoka kwa Marekani kupunguza uungaji mkono wake kwa Haftar na kulifanya bunge la Tobruk kuipa serikali ya Sarraj kura ya imani!
3- Hivyo ndivyo uingiliaji wa Marekani ulivyoanza hadharani kwa ombi la serikali ya Sarraj, yaani kwa ombi la serikali inayojiona kuwa halali! Kama alivyosema msemaji wa Marekani wa Pentagon, Peter Cook, mnamo 2016/8/1 kuwa "mashambulizi yalikuja kulingana na ombi la serikali ya maridhiano ya kitaifa ya Libya." Ombi hili ni jinai kubwa, na Sarraj hatonufaika na tamko lake mnamo 2016/8/1 kwenye televisheni rasmi ya Libya kuwa: "Baraza la Urais limeamua kama Amiri Jeshi Mkuu kuomba msaada wa moja kwa moja kutoka Marekani kuelekeza mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za ISIS mjini Sirte... na kwamba operesheni hizi katika hatua hii zinakuja ndani ya muda maalum na hazitovuka mji wa Sirte... na zitajikita kwenye msaada wa kiufundi na vifaa." Hilo halimsaidii, kwani msemaji wa Pentagon, Peter Cook, alisema kinyume chake kuwa "mashambulizi hayana mwisho katika wakati huu... na kwamba katika siku zijazo kila shambulio litaratibiwa na serikali ya maridhiano na litahitaji idhini ya kamanda wa vikosi vya Marekani barani Afrika" (Al-Khabar ya Algeria, 2016/8/2). Marekani kwa mara ya kwanza imepata fursa ya kuruhusiwa na serikali ya Libya rasmi kufanya mashambulizi nchini humo, na inatangaza kuwa haitaishia kwenye mashambulizi haya tu, bali itafanya mengi zaidi. Inahusisha hilo na kamandi yake ya Afrika, yaani ndani ya sera ya Marekani barani Afrika, na kwamba kamandi yake huko itasimamia operesheni hizo. Kwa hiyo, lengo hapa si Libya pekee bali ni Afrika Kaskazini nzima! Vilevile, Sarraj hanufaiki na tamko lake la kutokubali kuingia kwa vikosi vya nchi kavu, ambapo shirika la habari la AFP mnamo 2016/8/10 liliripoti: (Rais wa serikali ya maridhiano ya kitaifa ya Libya, Fayez al-Sarraj, alitangaza Jumatano kuwa nchi yake haihitaji vikosi vya kigeni kwenye ardhi ya Libya kusaidia vikosi vinavyopambana na ISIS, katika mahojijiano na gazeti la Kiitaliano Corriere della Sera). Hii ni huku gazeti la Marekani la Washington Post mnamo Jumanne 2016/8/9 likifichua kuwa "vikosi maalum vya Marekani vipo uwanjani, na vinatoa kwa mara ya kwanza msaada wa moja kwa moja kwa vikosi vya Libya vinavyopambana na ISIS katika eneo la Sirte"! Ni wazi kutokana na yote hayo kuwa matamshi ya Sarraj ni kwa ajili ya matumizi ya ndani tu na yako mbali na ukweli kama umbali wa mashariki na magharibi!
4- Marekani inatazama uingiliaji huu kama uimarishaji wa ushawishi wake katika eneo hilo. Katika muktadha huu, Rais wa Marekani Obama alitangaza siku moja baada ya mashambulizi, yaani 2016/8/2, kuwa "kuunga mkono vita vya serikali ya Libya dhidi ya ISIS ni kwa maslahi ya usalama wa taifa wa Marekani... na kwamba mashambulizi ya anga yalitekelezwa ili kuhakikisha kuwa vikosi vya Libya vinaweza kukamilisha kazi ya kupambana na kundi la kigaidi na kuimarisha utulivu." Aliongeza kuwa "Marekani, Ulaya na ulimwengu wana maslahi makubwa katika kufikia utulivu nchini Libya kwa sababu kukosekana kwa utulivu kulisaidia kuzidisha baadhi ya changamoto tulizoziona kuhusiana na mgogoro wa wahamiaji Ulaya na baadhi ya majanga ya kibinadamu tuliyoyaona baharini kati ya Libya na Ulaya" (Reuters, 2016/8/2). Rais wa Marekani anaona hili kuwa ni maslahi ya usalama wa taifa la nchi yake, ikimaanisha kuwa ni suala muhimu linalohusiana na uwepo wa Marekani nchini Libya. Vinginevyo, usalama wa taifa wa Marekani una uhusiano gani na Libya isipokuwa uwe unahusiana na ushawishi wa Marekani huko?! Obama anadai kuwa anafanya hivyo si kwa maslahi ya nchi yake tu, bali kwa maslahi ya Ulaya na ulimwengu, kana kwamba Marekani ndiyo itakayopatikana utulivu kwa Ulaya hasa ambayo inashindana nayo huko. Hii ina maana kuwa inafanya kazi ya kupanua ushawishi wa Marekani huko na kisha kuifanya Ulaya kuwa chini ya udhibiti wake.
5- Uingereza, kama tulivyosema hapo awali, ilimuamuru Sarraj kuomba uingiliaji wa Marekani kwa "tumaini" kwamba Marekani italipa fadhila hiyo kwa kupunguza uungaji mkono wake kwa Haftar na kulifanya bunge la Tobruk kuikubali serikali ya Sarraj. Lakini wakati huo huo, Ulaya inatambua kuwa Marekani haijali Haftar wala mwingine yeyote isipokuwa jinsi vibaraka hawa wanavyotumikia maslahi yake. Kama Marekani ingeweza kuwanyonya Sarraj na wenzake ushawishi wa Ulaya na wabaki kwake pekee, basi ingekuwa rahisi kwake kumtupa Haftar kando. Lakini hili linawezekana ikiwa tu itafanikiwa kuwatoa Sarraj na wenzake kutoka mikononi mwa Ulaya. Kwa hiyo, Ulaya inahofia kuwa Marekani itachelewesha idhini ya bunge la Tobruk ili kupata shinikizo zaidi kwa serikali ya Sarraj na kisha kurefusha uingiliaji wa kijeshi kwa maslahi yake. Ndiyo maana Ulaya ilitumia fursa ya kutangazwa kwa uingiliaji wa Marekani ili na yenyewe itangaze uingiliaji wake ambao ilikuwa ikiuficha, ili uwanja wa kijeshi nchini Libya usibaki kwa Marekani pekee. Hapo ndipo uingiliaji ukawa wazi na mataifa ya Ulaya hayahitaji tena uingiliaji wa siri kama ilivyofanya Ufaransa ambapo wanajeshi wake waliuawa. Hivyo, kuwepo kwa vikosi vya Ulaya nchini Libya kutaizuia Marekani kufanya itakavyo. Gazeti la Sunday Times mnamo 2016/8/7 lilifichua kuwa "vikosi maalum vya Uingereza vilishiriki hapo awali katika kupambana na ISIS huko Sirte pamoja na vikosi vya Baraza la Urais." Balozi wa Uingereza nchini Libya, Peter Millett, kupitia ukurasa wake wa Twitter, alikaribisha "kujiunga kwa Libya kwenye muungano wa kimataifa wa kupambana na ISIS." Pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, alielezea kukaribisha kwa nchi yake hatua ya serikali ya Libya kuomba msaada wa kimataifa. Ufaransa inajaribu kucheza kote ili kuiridhisha Marekani kwa kumuunga mkono Haftar upande wa mashariki, na wakati huo huo inatangaza waziwazi kuunga mkono serikali ya Sarraj upande wa magharibi! Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Paolo Gentiloni, alisema: "Italia inakaribisha operesheni za anga zilizofanywa na Marekani... na ilielezea utayari wa nchi yake kuitikia ombi la Libya kwa aina zote za msaada ikiwemo wa kijeshi" (Anadolu, 2016/8/3). Waziri wa Ulinzi wa Italia, Roberta Pinotti, alisema kuwa "Italia huenda itaruhusu utumiaji wa kambi zake za anga na anga yake kwa ajili ya mashambulizi dhidi ya ISIS nchini Libya, ikiwa Marekani itaomba hivyo" (Reuters, 2016/8/3).
6- Hivyo ndivyo mfumo wa kisiasa nchini Libya uliojitokeza kutokana na makubaliano ya Skhirat yaliyoundwa na Uingereza, sasa unatangaza kuruhusu Marekani kuingilia kati! Hawakuona haya mbele ya Allah wala mbele ya Mtume Wake na Waumini kwa kuomba nchi kafiri ya kikoloni iingilie kijeshi katika nchi yetu! Ingawa wanaingilia kati kwa sababu ya usaliti wa watawala katika nchi zetu, lakini kuwa kwa ombi la watawala hao ni jambo baya zaidi. Kisha Sarraj, kama walivyo vibaraka wengine, haoni haya anapotenda jambo leo na kesho kutenda kinyume chake; jana alipinga uingiliaji wa Ufaransa, na leo anashangilia uingiliaji wa Marekani na kuuomba kwa ulimi wake! Vibaraka wanatekeleza wanachoamriwa; ni viziwi, mabubu, na vipofu, kwa hiyo hawaelewi... yote hayo ni kwa tumaini kuwa Marekani itakubali kulifanya bunge la Tobruk kuipa imani serikali ya Sarraj!
7- Ombi rasmi la Sarraj kwa ajili ya uingiliaji wa kijeshi wa Marekani na kufuatiwa na tangazo la uingiliaji wa kijeshi wa Ulaya kumeifanya Libya kuwa uwanja wa moto, si tu kwa ushindani wa kisiasa bali pia kwa ushindani hatari zaidi wa kijeshi! Hii ni jinai kubwa ambayo mhusika wake na aliyeshiriki atapata udhalili duniani na adhabu kali Akhera.
سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ
"Saitawafika wale waliofanya uhalifu udhalili mbele ya Allah na adhabu kali kwa sababu ya vitimbi walivyokuwa wakivifanya." (QS Al-An'am [6]: 124)
Hakika Allah Mwenye Nguvu, Mtukufu, amekataza makafiri kuwa na njia ya kuwadhuru Waumini, na kutafuta msaada kwa makafiri kunawapa njia dhidi ya Waumini.
وَلَنْ يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا
"Wala Allah hatawafanyia makafiri njia ya kuwashinda Waumini." (QS An-Nisa [4]: 141)
Na Allah Mwenye Nguvu, Jabari, amekataza kuwafanya makafiri kuwa walinzi (marafiki wa karibu) na amemfanya anayewafanya kuwa marafiki kuwa ni miongoni mwa wanafiki na atapata adhabu iumizayo.
بَشِّرِ الْمُنَافِقِينَ بِأَنَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا * الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِنْ دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَيَبْتَغُونَ عِنْدَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا
"Wabashirie wanafiki kwamba watapata adhabu iumizayo. Ambao huwafanya makafiri kuwa marafiki (walinzi) badala ya Waumini; je, wanatafuta nguvu kwao? Hakika nguvu zote ni za Allah." (QS An-Nisa [4]: 138-139)
Na Mtume ﷺ amekataza kutafuta msaada kwa makafiri: Kutoka kwa Urwah, kutoka kwa Aisha (r.a), kwamba Mtume ﷺ alisema:
إِنَّا لَا نَسْتَعِينُ بِمُشْرِكٍ
"Hakika sisi hatuombi msaada kwa mshirikina." (Imetolewa na Ad-Darimi katika Sunan yake).
Na ametoa At-Tabarani katika Al-Mu'jam al-Kabir kutoka kwa Khubaib bin Abdirrahman bin Khubaib, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, alisema: Mtume ﷺ alisema:
فَإِنَّا لَا نَسْتَعِينُ بِالْمُشْرِكِينَ
"Basi hakika sisi hatuombi msaada kwa washirikina."
Na ametoa Al-Hakim katika Al-Mustadrak kutoka kwa Abu Humaid as-Sa'idi (r.a) alisema:
فَإِنَّا لَا نَسْتَعِينُ بِالْمُشْرِكِينَ
"Basi hakika sisi hatuombi msaada kwa washirikina."
Katika kuhitimisha, hakika serikali hizi zilizopo Magharibi mwa Libya na Mashariki mwa Libya ni vibaraka wa Magharibi, pande zote mbili za Ulaya na Marekani. Ni wajibu kwa watu wa Libya wenye wivu na dini yao, nchi yao na umma wao, kufanya kazi ya kuziangusha serikali hizo zilizomwezesha kafiri mkoloni, adui wa Uislamu na Waislamu, kuhalalisha ardhi ya mujahidina na waliohifadhi Qur'ani Tukufu... Kisha ni wajibu kwao pia kudhibiti mikono ya wanamgambo na makundi hayo yanayopigana baina yao na kumwaga damu iliyoharamishwa na kukufurishana, kwani kumwaga damu na kukufurisha Mwislamu ni mambo makubwa mbele ya Allah (swt) na Mtume Wake ﷺ. Kuhusu kumwaga damu, At-Tirmidhi ametoa katika Sunan yake kutoka kwa Abdullah bin Amr, kwamba Mtume ﷺ alisema:
لَزَوَالُ الدُّنْيَا أَهْوَنُ عَلَى اللَّهِ مِنْ قَتْلِ رَجُلٍ مُسْلِمٍ
"Kuangamia kwa dunia ni jambo jepesi mbele ya Allah kuliko kuuawa kwa mwanamume Mwislamu."
An-Nasa'i ametoa katika Sunan yake kutoka kwa Abdullah bin Amr, kutoka kwa Mtume ﷺ alisema:
لَزَوَالُ الدُّنْيَا أَهْوَنُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ قَتْلِ رَجُلٍ مُسْلِمٍ
"Kuangamia kwa dunia ni jambo jepesi mbele ya Allah kuliko kuuawa kwa mwanamume Mwislamu."
Na kuhusu kumkufurisha Mwislamu, Al-Bukhari ametoa katika Sahih yake kutoka kwa Abdullah bin Umar (r.a) kwamba Mtume ﷺ alisema:
أَيُّمَا رَجُلٍ قَالَ لِأَخِيهِ يَا كَافِرُ، فَقَدْ بَاءَ بِهَا أَحَدُهُمَا
"Mtu yeyote anayemwambia ndugu yake: 'Ewe kafiri', basi mmoja wao ameshakata hukumu hiyo (amekuwa hivyo)."
Muslim ametoa kutoka kwa Ibn Umar kwa tamko kuwa Mtume ﷺ alisema:
إِذَا كَفَّرَ الرَّجُلُ أَخَاهُ فَقَدْ بَاءَ بِهَا أَحَدُهُمَا
"Mtu anapomkufurisha ndugu yake, basi mmoja wao ameshakuwa hivyo."
Na imekuja katika Al-Adab al-Mufrad kutoka kwa Abdullah bin Umar kwamba Mtume ﷺ alisema:
إِذَا قَالَ لِلْآخَرِ: كَافِرٌ، فَقَدْ كَفَرَ أَحَدُهُمَا، إِنْ كَانَ الَّذِي قَالَ لَهُ كَافِرًا فَقَدْ صَدَقَ، وَإِنْ لَمْ يَكُنْ كَمَا قَالَ لَهُ فَقَدْ بَاءَ الَّذِي قَالَ لَهُ بِالْكُفْرِ
"Anapomwambia mwingine: 'Kafiri', basi mmoja wao ameshakufuru; ikiwa yule aliyeambiwa ni kafiri basi amesema kweli, na ikiwa sivyo kama alivyosema, basi aliyesema amerudiwa na ukafiri huo."
Hivyo basi, kumwaga damu ya Mwislamu ni jambo zito sana, na kadhalika kumkufurisha Mwislamu ni jambo zito sana.
Mwisho kabisa, tunatambua kuwa katika nchi nzuri ya Libya kuna wanaume wengi, mujahidina shujaa, wachamungu na wasafi kwa idhini ya Allah. Na hawa ndio tunaotegemea heri kutoka kwao. Wasimame msimamo wa kweli na haki dhidi ya ule uovu wa pande nne: Makafiri wakoloni, watawala wasaliti walioasi wanaopiga vita sheria ya Uislamu na Khilafah Rashidah, na wale wanaotangaza Khilafah kwa upuuzi na kumwaga damu iliyoharamishwa kwa jina lake ili kuichafua... Upande huu wa uovu wa nne ni lazima usimamiwe kidete kwa msimamo wa haki na kweli... Na pamoja na hayo yote, hatukati tamaa na rehema ya Allah, bali tunatarajia kheri kwa kurejea kwa Khilafah ya kweli, Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, itakayolinda usalama wa watu na kusimamia mambo yao, na kwayo Uislamu na Waislamu watatukuka na makafiri na wanafiki watadhalilika.
وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
"Na Allah ni Mshindi katika jambo Lake, lakini watu wengi hawajui." (QS Yusuf [12]: 21)
9 Dhul-Qi'dah 1437 H 2016/8/12 M