Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

JIBU LA SWALI: INDIA, PAKISTAN NA KUSITISHA MAPIGANO

May 20, 2025
3504

Jibu la Swali

Swali:

Trump alitangaza jana Jumamosi kwa njia ya kushangaza katika chapisho kupitia jukwaa lake la Truth Social kwamba ("baada ya usiku mrefu wa mazungumzo yaliyopatanishwa na Marekani, nina furaha kutangaza kwamba India na Pakistan zimekubaliana kusitisha mapigano kikamilifu na mara moja," akiyasifu nchi hizo mbili kwa "kutumia akili timamu na akili kubwa... Al Jazeera, 11/05/2025). Mvutano ulikuwa umeongezeka kati ya India na Pakistan kufuatia shambulio lililolenga watalii katika Bonde la Baisaran katika eneo la Pahalgam huko Jammu na Kashmir inayotawaliwa na India mnamo Aprili 22, 2025, ambalo lilisababisha vifo vya Wahindi 25 na Mnepali mmoja. Mnamo Aprili 23, 2025, India ilitangaza kusitisha Mkataba wa Maji ya Mto Indus uliotiwa saini mwaka 1960 kama sehemu ya mfululizo wa hatua za kuadhibu Pakistan. Kwa kujibu hilo, Pakistan ilitangaza kusitisha Makubaliano ya Simla ya mwaka 1972 yanayosimamia uhusiano wa pande mbili. Mnamo Mei 7, India ilitangaza kutekeleza operesheni ya kijeshi chini ya jina "Operation Sindur"... kisha Pakistan ikajibu... Na sasa kama Trump alivyotangaza kwamba upatanishi wake umefanikiwa kusitisha mapigano... Je, ni upi ukweli wa mvutano huu na mgogoro huu? Na ni nini hasa Mkataba wa Maji ya Indus ambao India iliutelekeza kwa muda? Na je, Amerika ina mkono katika kuanza kwa shambulio hilo kama ilivyo na mkono katika kulisimamisha?

Jibu:

Ili kubainisha jibu la maswali haya, ni lazima kupitia ukweli ufuatao:

1- Chama cha Bharatiya Janata (BJP), kilichoingia madarakani nchini India kikiongozwa na Atal Bihari Vajpayee kuanzia mwaka 1998 hadi 2004, kisha kikarejea madarakani kikiongozwa na Narendra Modi mwaka 2014 baada ya miaka 10 ya utawala wa Chama cha Congress kinachoegemea Uingereza, ni chama kinachoifuata Amerika, kama sehemu ya mkakati wake wa Eurasia, yaani kukabiliana na China na kuizingira... Ni wazi kwamba maslahi ya haraka ya Amerika katika Mashariki ya Mbali yalikuwa nyuma ya ushindi wa Modi, Mhindu mwenye msimamo mkali, mwaka 2014 na bado inamuunga mkono.. Narendra Modi amekuwa akitekeleza maslahi ya Amerika daima, iwe ni katika kuunganisha Kashmir mwaka 2019, au katika mapigano ya mpakani aliyopigana na China mnamo miaka ya 2014, 2017 na 2020, au huko Afghanistan, au katika kukwamisha Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan (CPEC).

2- Baada ya Modi kuingia madarakani nchini India mwaka 2014, Amerika imeitumia India kwa ufanisi kuongeza shinikizo kwa China, kuizingira, na kuizuia kudhibiti maeneo yanayoizunguka, na kuibakisha ndani ya mipaka yake.. Hasa kwa kuwa Amerika imetangaza vita vya kiuchumi dhidi ya China, ambapo Trump ameweka ushuru mkubwa wa forodha kwa bidhaa za China. Trump analenga kupitia ushuru huu wa ziada kudhoofisha uchumi wa China. Kumekuwa na habari kwamba makampuni makubwa ya teknolojia, kama vile kampuni ya iPhone, yanakusudia kuhamisha viwanda vyao kwenda India kutokana na kuongezeka kwa ushuru. (Kampuni ya Apple ilifichua kuwa inapanga kuhamisha shughuli za kuunganisha simu zote za iPhone zinazouzwa Marekani kwenda India, kulingana na gazeti la "The Financial Times"... Euro News, 26/04/2025). Hivyo basi, katika mfumo wa mkakati wake wa kukabiliana na China, Marekani inatafuta kuimarisha hadhi ya India kama nguvu ya kiuchumi na kijeshi katika kanda hiyo.

3- Hii ilihitaji upande mmoja kuunga mkono India kwa njia za nguvu za kijeshi na kiuchumi.. Na upande mwingine kutatua matatizo ya India na Pakistan, kwani tawala zote mbili ni mawakala wa Amerika.. Hiyo ni ili India iweze kujielekeza kikamilifu kwa upande wa China:

Ama upande wa kwanza: Amerika imeiunga mkono India na jeshi lake kwa njia zote kama vile kuhamisha teknolojia ya nyuklia ya Amerika kwenda India.. Swala la kukabiliana na China lilikuwepo kwa nguvu wakati wa mkutano wa Trump na Waziri Mkuu wa India huko Washington: (Viongozi hao wawili pia walijadili kuimarisha "Ushirikiano wa Nne" (Quad) wa kiusalama katika eneo la Asia-Pasifiki ambao pia unajumuisha Japan na Australia. India imepangwa kuwa mwenyeji wa viongozi wa kundi hilo baadaye mwaka huu, kundi ambalo linaonekana kama uzito wa kukabiliana na shughuli za kijeshi za China zinazoongezeka. Reuters, 14/02/2025).

Na ama upande wa pili, matatizo yaliyojitokeza zaidi yalikuwa:

a- Vikosi vya Pakistan mpakani: Vinazuia uhamishaji wa vikosi vya India kuelekea upande wa China, na kwa hivyo Amerika ilishinikiza Pakistan kuhamisha vikosi vyake kutoka mpaka wa India kwenda maeneo ya kikabila huko Waziristan kupambana na kundi la Taliban la Pakistan, na huko Balochistan kupambana na Jeshi la Ukombozi la Balochistan, na kwenye mpaka wa Afghanistan, ili India iweze kusonga kwa uhuru mbele ya China na kuhamisha majeshi yake kwenye mpaka wa China badala ya kuyatawanya kwenye mpaka wa Pakistan. Kisha Amerika ikaanza kuitaka Pakistan kutoa makubaliano moja baada ya jingine kwa India ili kurahisisha India kujiondoa kwenye makabiliano na Pakistan na kujiweka kwenye makabiliano na China.. Kwa ajili hiyo, kama tulivyosema awali, Pakistan ilihamisha vikosi vyake vingi vya kijeshi kutoka mpaka na India na kuvitumia katika mapigano ya ndani nchini Pakistan dhidi ya makundi ya jihadi, ... na ikaanza kupambana na kundi la Taliban nchini Afghanistan.

b- Mzozo wa Kashmir: India iliunganisha eneo hilo kwa uamuzi wake mnamo 05/08/2019.. Tulisema katika jibu la swali mnamo 18/08/2019:

(- Muda mfupi baada ya matukio ya Septemba 11, 2001, utawala wa Bush ulielekeza nguvu zake kwa India, na asilimia kubwa ya hatua za Amerika zilielekezwa katika kuziba mwanya wa kijeshi kati ya India na China kulingana na mipango ya Amerika, ikiwemo mkataba wa nyuklia wa Amerika na India...

  • Amerika iliona kuwa mivutano kuhusu Kashmir kati ya India na Pakistan inaathiri na kudhoofisha ukabilianaji wa India dhidi ya China... Na ili kushinda mivutano hii, Marekani ilianza mchakato wa kuhuisha mahusiano (normalization) kati ya India na Pakistan, na lengo la kuhuisha mahusiano lilikuwa ni kuviondoa vikosi vya India na Pakistan kwenye kupigana vyenyewe kwa vyenyewe kwa sababu ya Kashmir, na kuelekeza juhudi kuelekeza ushirikiano na Marekani mwishowe kuzuia kuongezeka kwa China. Amerika ilifikiri kwamba kunyakua Kashmir na kuijumuisha na India na shinikizo la Amerika kwa utawala wa Pakistan kuuzuia kuirudisha kijeshi na kuhamishia swala hilo kwenye mazungumzo kungeua kadhia hiyo na kuzuia mzozo wa kijeshi kati yao, kama ilivyo hali ya mamlaka ya Abbas huko Palestina na nchi za Kiarabu zinazoizunguka bila mzozo wa kijeshi na dola ya Kiyahudi wakati ambapo wananyakua na kuunganisha kile wanachotaka huko Palestina! Hivyo ndivyo Modi alianza mpango wa kunyakua Jammu na Kashmir na kubadilisha idadi ya watu ndani yake na kisha ukafuata uamuzi uliochukuliwa na Modi mnamo 05/08/2019 wa kufuta Kifungu cha 370 cha katiba yao kinachohusiana na Kashmir..) Kwa dhana ya Amerika kwamba kunyakua huko kutawafanya Waislamu waisahau Kashmir na India na Pakistan ziwe bila matatizo kati yao kwa kuzingatia kuwa tawala zote mbili zinafuata njia ya Amerika sasa, lakini Amerika ilisahau au ilijisahaulisha yenyewe na India kwamba Kashmir iko ndani ya mioyo ya Waislamu na itarudi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu..

c- Tatizo la kugawana maji na Pakistan: India ilitaka kurejelea Mkataba wa Maji ya Indus uliopo, kwani India imekuwa ikijitahidi kwa muda mrefu kurejelea mkataba huo uliotiwa saini mwaka 1960 kwa upatanishi wa Benki ya Dunia kufuatia mazungumzo yaliyodumu kwa miaka tisa, ikisingizia ukuaji wa haraka wa idadi ya watu, huku Pakistan ikikataa mazungumzo yoyote mapya kuhusu mkataba huo. Gazeti la "India Today", likinukuu vyanzo vyenye habari ambavyo havikutajwa majina, lilisema (kwamba India ilisitisha mtiririko wa maji kutoka Bwawa la Baglihar kwenye Mto Chenab kwenda Pakistan. Gazeti hilo lilibainisha kuwa India pia inapanga kukata mtiririko wa maji kutoka Bwawa la Kishanganga kwenye Mto Jhelum. Anadolu, 05/05/2025). Kwa kuzingatia usitishaji huu wa upande mmoja wa mkataba na India na madai yake ya mara kwa mara ya kuurejelea kwa miaka mingi, hatua ya serikali ya Modi ya kusitisha mkataba baada ya shambulio la Pahalgam inaweza kufasiriwa kama jaribio la kuishinikiza Pakistan na kuilazimisha kukubali hitaji la kuurejelea mkataba huo. (Katika miaka michache iliyopita, serikali ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi imetafuta kufanya mazungumzo upya kuhusu mkataba huo, na nchi hizo mbili zilijaribu kusuluhisha baadhi ya tofauti zao katika Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishi huko The Hague kuhusu ukubwa wa eneo la kuhifadhia maji katika vituo vya umeme vya Kishanganga na Ratle... Arabi21, 27/04/2025).

Ni vyema kutaja kwamba Mkataba wa Maji ya Indus (ISA) unawakilisha mkataba wa usambazaji wa maji kati ya mataifa ya India na Pakistan, na uliandaliwa na kufanyiwa mazungumzo chini ya uangalizi wa Benki ya Dunia. Mji wa Karachi ulishuhudia sherehe za utiaji saini wa mkataba huu muhimu mnamo Septemba 19, 1960. Pakistan ilipewa haki ya kutumia maji ya mito mitatu katika sehemu ya magharibi ya bonde la Indus (Mto Jhelum, Mto Chenab, na Mto Indus wenyewe), wakati India ilihifadhi udhibiti kamili wa maji ya mito mitatu ya mashariki (Mto Sutlej, Mto Beas, na Mto Ravi).

d- Harakati za kijihadi huko Kashmir: Zilikuwa zikiisababishia India wasiwasi, hivyo Amerika ilitaka kuanzisha mapigano huko kama kisingizio cha shambulio la India dhidi ya mizizi ya harakati hizo huko Kashmir na kujaribu kuuhusisha utawala wa Pakistan katika kushambulia harakati hizo nchini Pakistan.. Na hiyo ilikuwa katika hatua mbili:

Kwanza: Kuanzisha shambulio huko Kashmir ambalo italinukuu kwa harakati hizo na kulifanya kisingizio cha operesheni kubwa ya kijeshi dhidi ya vituo vya harakati hizi nchini Pakistan kama inavyosema.. Na dhidi ya mizizi ya harakati hizo huko Kashmir na dhidi ya Waislamu huko ili kuwaua au kuwafukuza kwa kisingizio cha kuunga mkono harakati hizo kama wanavyofanya Mayahudi huko Gaza kwa mauaji yao dhidi ya watu wake kwa kisingizio cha kuunga mkono upinzani.. Kisha kuufedhehesha utawala nchini Pakistan ili usinusuru Kashmir kwa sababu shambulio lilianzishwa na harakati hizo!

Hivyo India ilianza kwa amri ya Amerika shambulio hili la kutengenezwa huko Kashmir.. Na ushahidi wa hilo ni:

  • Shambulio lililolenga watalii katika Bonde la Baisaran katika eneo la Pahalgam huko Kashmir inayotawaliwa na India mnamo Aprili 22, 2025, ambalo India inadai kuwa lilitekelezwa na kikundi cha wapiganaji kinachoungwa mkono na Pakistan, wakati Pakistan inakanusha hilo; shambulio hili lilitokea huko Kashmir mnamo 22/04/2025 wakati wa kuwepo kwa Makamu wa Rais wa Amerika JD Vance huko New Delhi, ("JD Vance" Makamu wa Rais wa Amerika aliwasili India leo, Jumatatu, mwanzoni mwa ziara ya siku nne, ambapo anafanya mazungumzo na Waziri Mkuu "Narendra Modi". Shirika la Habari la Bahrain, 21/04/2025), na India ilichukua hatua zake zote za awali dhidi ya Pakistan ikiwemo kusitisha Mkataba wa Mto Indus wakati wa kuwepo kwa ofisa huyu wa Amerika huko New Delhi, jambo ambalo linaashiria uratibu wa Amerika na India, na haijuzu kabisa kudhani kuwa yote hayo ni sadfa tupu.

  • Serikali ya India kufanya haraka kuelekeza tuhuma kwa Pakistan kufuatia kutokea kwa shambulio hilo mnamo Aprili 22 katika dakika chache tu, na kabla ya kuanza kwa uchunguzi wowote au kazi za utafiti, na hiyo ni licha ya ombi la Pakistan la kufanya uchunguzi wa kimataifa kuhusu tukio hilo. Aidha, utangazaji wa vyombo vya habari vya India uliofanya haraka kuashiria kwa "The Resistance Front" (TRF), ambayo inachukuliwa kuwa tawi la kundi la Lashkar-e-Taiba (LET), huku kundi hilo likitangaza kukanusha kuhusika na shambulio hilo; yote hayo yanaashiria kuwa ni operesheni "ya kutengenezwa". ("The Resistance Front" ilidai kuhusika na shambulio hilo kupitia mitandao ya kijamii, kisha ikajiondoa baadaye, ikihalalisha hilo kwa udukuzi wa kielektroniki... Tovuti ya 24, 30/04/2025).

Kisha ikaanza hatua ya pili, India ilianzisha shambulio la makombora dhidi ya Pakistan jioni ya 06/05/2025 na haikuishia tu kwenye sehemu ya Pakistan ya Kashmir kama ilivyozoeleka, bali ilipiga malengo katika mkoa wa Punjab pia. Pakistan haikujibu kwa kupiga malengo ndani ya India na ilitosheka na mapigano ya mpakani na kuangusha ndege za India mipakani. India ilijaribu kupunguza makali ya shambulio dhidi ya Pakistan ikisema kuwa haikushambulia malengo ya jeshi la Pakistan bali ilishambulia "magaidi" pekee... Television ya Arabi, 07/05/2025). Mapigano yaliendelea kuongezeka kati ya pande hizo mbili, (Mapigano makali yalizuka kando ya mstari wa udhibiti huko Kashmir kati ya vikosi vya India na Pakistan, na milipuko ilisikika kando ya mstari wa udhibiti huko Kashmir huku kukiwa na ripoti za vifo, kulingana na vyombo vya habari vya India... Al Arabiya, 09/05/2025). India ilikiri kuanguka kwa ndege zake 3, na kutangaza kuuawa kwa raia 7 huko Kashmir inayoidhibiti kutokana na mashambulizi ya Pakistan. Wakati huo huo, Pakistan ilisema kuwa iliangusha ndege 5 za India zikiwemo tatu za aina ya Rafale za Ufaransa na pia droni 25 zilizotengenezwa na chombo cha Kiyahudi. Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif alisema ("Tungeweza kuangusha ndege 10 za kivita za India, wakati wa kujibu shambulio la India lililolenga maeneo ya Pakistan lakini viongozi wa jeshi walionyesha kujizuia na wakaangusha ndege 5 pekee"... Asharq News, 07/05/2025). Msemaji wa jeshi la Pakistan Ahmad Sharif Chaudhry alitangaza kuwa jeshi lilipiga vituo 26 vya kijeshi na makumi ya droni yalipaa juu ya miji mikuu ya India ikiwemo mji mkuu New Delhi"... Sky News, 10/05/2025). Inadhihirika kwamba Pakistan ilikuwa na uwezo wa kuanzisha shambulio kubwa na pana na kuingia kwenye makabiliano na India na kuishinda. Lakini imefungwa na Amerika ambayo haikuiruhusu kufanya mapambano kama hayo na kuipiga India kipigo kikali kitakachopelekea kuanguka kwa wakala wake Modi.. Na ingawa Amerika iliweza kuushinikiza utawala ambao ni wakala wake nchini Pakistan ili utosheke na jibu lenye mipaka dhidi ya uvamizi wa India, lakini kile kilichodhihirika katika jibu hili lenye mipaka kinaonyesha ushujaa wa askari Waislamu nchini Pakistan na nguvu ya kusukumwa kwao kupigana, hata kama utawala nchini Pakistan unashirikiana na Amerika na kuweka vikwazo kwenye harakati za jeshi, jeshi hili la Kiislamu lilileta hasara kubwa kwa adui mshirikina kama tulivyotaja hapo awali.. Haya yote yaliisukuma Amerika kuhitimisha mpango wa mapigano kama ilivyouanzisha na kukimbilia kusitisha uvamizi kama ilivyouanza na kubadilisha mpango wa mapigano kuwa mtego wa kisiasa wa mazungumzo kati ya tawala mbili vibaraka kwake, India na Pakistan, ili kuipatia India kile ambacho haikuweza kukipata kwa uvamizi wa kijeshi...

4- Kwa hivyo, baada ya siku nne tangu kuanza kwa shambulio la India, mnamo 10/05/2025 usitishaji mapigano ulitangazwa kwa amri za Amerika. Rais wa Amerika Trump aliandika kwenye jukwaa lake la Truth Social mnamo 10/05/2025 ("Baada ya usiku mrefu wa mazungumzo kupitia Marekani, nina furaha kutangaza kwamba India na Pakistan zimekubaliana kusitisha mapigano kikamilifu na mara moja. Ninazipongeza nchi zote mbili kwa kutumia akili timamu na akili ya juu. Nawashukuru kwa kulijali suala hili"). Waziri wa Mambo ya Nje wa Amerika Marco Rubio alisema kwenye jukwaa la X mnamo 10/05/2025 "Kwamba serikali za India na Pakistan zimekubaliana kusitisha mapigano mara moja na kuanza mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sehemu isiyo na upande wowote" na akaongeza kuwa yeye na Makamu wa Rais JD Vance walifanya kazi na Mawaziri Wakuu wa India Narendra Modi na Pakistan Shehbaz Sharif na Waziri wa Mambo ya Nje wa India Subrahmanyam Jaishankar na Mkuu wa Majeshi ya Pakistan Asim Munir na Washauri wa Usalama wa Taifa wa India Ajit Doval na Pakistan Asim Malik katika siku mbili zilizopita kufikia makubaliano"). Yaani Amerika haikuthamini ushujaa wa jeshi la Pakistan licha ya uaminifu wa uongozi wake kwake, hivyo iliogopa kwa ajili ya Modi kutokana na kuendelea kwa mapigano na kupoteza utawala wake badala ya kutekeleza kile ambacho Amerika ilimtaka akifanye katika kukabiliana na China! Hivyo basi, ikaamuru kusitisha vita na kuelekea kwenye mtego wa kisiasa kwa kufikia malengo yake kupitia mazungumzo kati ya tawala mbili vibaraka kwake!

5- Katika kuhitimisha, Hizbut Tahrir inawatahadharisha Waislamu kwa ujumla na watu wa Pakistan kwa mahususi, kutokana na mtego wa kisiasa na mazungumzo yanayofanyika na maadui wa Uislamu na Waislamu, hasa washirikina Wahindu nchini India na Mayahudi huko Palestina. Mazungumzo haya hayaleti kheri yoyote, hasa ikiwa Amerika kafiri mkoloni ndiyo inayaendesha kama inavyotokea sasa, kwani wanapigana na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika kila wakati na mahali.. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ ametujulisha kuhusu kupigana nao na ushindi dhidi yao, na katika hilo kuna ujira mkubwa.. Muslim ametoa katika Sahih yake kutoka kwa Ibn Umar, kutoka kwa Mtume ﷺ amesema:

لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ...

"Hakika mtapigana na Mayahudi na mtawauwa..." (HR. Muslim)

Na Ahmad na An-Nasa’i wametoa kutoka kwa Thawban, mtumishi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema:

عِصَابَتَانِ مِنْ أُمَّتِي أَحْرَزَهُمَا اللهُ مِنَ النَّارِ؛ عِصَابَةٌ تَغْزُو الْهِنْدَ، وَعِصَابَةٌ تَكُونُ مَعَ عِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ عَلَيْهِمَا السَّلَام

"Makundi mawili katika Ummah wangu Mwenyezi Mungu ameyaokoa na moto; kundi litakaloivamia India, na kundi litakalokuwa pamoja na 'Isa bin Maryam (as)."

Hivyo kupigana na Mayahudi huko Palestina na kuwauwa, na kuivamia India na ushindi wa Uislamu ndani yake, ni lazima vitatokea kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kwani hiyo ni kauli ya mkweli mwenye kusadikiwa ﷺ.. Isipokuwa kwamba Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta'ala aliamua kwamba ushindi hautashuka kwetu kutoka mbinguni, huku ukibebwa na Malaika Wake kwetu tukiwa tumeketi, bali tufanye kazi, tujitahidi na tujikakamue, na tutafute ukweli na ikhlasi katika kile tunachokifanya, na hivyo ndivyo tunavyopaswa kuwa, kisha utakuja ushindi wa Mwenyezi Mungu bila shaka, kwa idhini Yake Subhaanahu. Nasi tunatarajia kheri kwa watu wa Pakistan, kwani ni nchi yenye nguvu ya Kiislamu na mizizi ya Uislamu ndani yake ni ya kina na hisia za Kiislamu ndani yake ni zenye nguvu, na jeshi lake linapenda jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na matarajio ya Waislamu ndani yake kusimamisha Khilafah yanazidi kuongezeka. Haitachukua muda mrefu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kabla ya kupatikana nusura kwa kiongozi ambaye hawadanganyi watu wake, ..., kisha itatimia kauli yake ﷺ kwa kusimamisha Khilafah Rashidah baada ya huu utawala wa kidikteta (Mulkan Jabriyya) tunamoishi; Ahmad ametoa katika Musnad yake kutoka kwa Hudhayfah amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema:

..ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ. ثُمَّ سَكَتَ

"...kisha utakuwepo utawala wa kidikteta, utakuwepo kwa muda anaopenda Mwenyezi Mungu uwepo, kisha Atauondoa pale Atakapotaka Auondoe, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume. Kisha akanyamaza."

Na siku hiyo waumini watafurahi:

وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ

"Na siku hiyo waumini watafurahi * kwa nusura ya Mwenyezi Mungu, humunusuru Amtakaye, Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu." (QS. Ar-Rum [30]: 4-5)

Mnamo tarehe 17 Dhul-Qa'dah 1446 H 15/05/2025 M

Share Article

Share this article with your network