Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni mtukufu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wageni kwenye ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi"
Jibu la Swali
Uislamu na Dini za Mitume
Kwa: Abu Sarah
Swali:
Assalamu alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuhu
Sheikh wetu ambaye anatukuzwa na Allah, tungependa kukuuliza.
Katika kitabu an-Nizham al-Islam imeandikwa kuwa Uislamu ni dini iliyofunuliwa kwa Mtume Muhammad ili kuratibu mahusiano ya kibinadamu na Allah, mahusiano ya kibinadamu na wao wenyewe, na mahusiano ya kibinadamu na wanadamu wenzao.
Ninachouliza: Je, Uislamu ulifunuliwa tu kwa Mtume Muhammad, na si kwa mitume waliopita? Hivyo, dini ya mitume waliopita ilikuwa nini?
Ninakushukuru kwa jibu lako, na Mwenyezi Mungu akulipe malipo makubwa.
wassalamu alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuhu.
الجواب:
وعليكم السلام ورحمة الله وبركاته،
Unaashiria katika swali lako kile kilichokuja mwanzoni mwa mjadala wa "Mfumo wa Uislamu" katika kitabu cha (Nizham al-Islam) kuhusu ufafanuzi wa Uislamu kama ifuatavyo:
"[Uislamu ni dini ambayo Mwenyezi Mungu aliiteremsha kwa Bwana wetu Muhammad ﷺ ili kupanga uhusiano wa mwanadamu na Muumba wake, na nafsi yake, na binadamu wenzake. Na uhusiano wa mwanadamu na Muumba wake unajumuisha itikadi na ibada; na uhusiano wake na nafsi yake unajumuisha maadili, vyakula na mavazi; na uhusiano wake na binadamu wenzake unajumuisha miamala na adhabu.] Mwisho."
Hakika neno Uislamu na mnyambuliko wake kutoka katika asili yake hutumika katika maandiko ya kisheria (Nusus) kwa maana ya kilugha, yaani ukweli wa kilugha (haqiqah lughawiyyah), na hutumika kwa maana ya kiistilahi, yaani ukweli wa kisheria (haqiqah shar’iyyah). Ama maana ya kilugha ya neno Uislamu ni kujisalimisha, kutii na ikhlasi. Na ama maana ya kiistilahi, ni kuitumia lafudhi ya Uislamu kama jina la dini aliyoiteremsha Allah (swt) kwa Bwana wetu Muhammad ﷺ hasa, kama ilivyo katika ufafanuzi uliotajwa hapo juu kutoka kitabu cha Nizham al-Islam. Na huu hapa ni ufafanuzi:
Kwanza: Maana ya Kilugha (Ukweli wa Kilugha) wa lafudhi ya Uislamu:
Maana ya kilugha ya neno Uislamu imekuja katika kamusi za lugha kama ifuatavyo:
a- [Lisan al-Arab (12/289):
"Al-Islam na al-istislam maana yake ni unyenyekevu/utii. Al-Islam katika Sharia ni kudhihirisha unyenyekevu na kudhihirisha Sharia na kushikamana na yale aliyokuja nayo Mtume... Ama al-Islam, Abu Bakr Muhammad bin Bashar amesema: Inasemekana fulani ni Muslim (Muislamu), na kuna kauli mbili juu ya hilo: Moja ni kuwa yeye ni mwenye kujisalimisha kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na ya pili ni kuwa yeye ni mwenye kumtakasia (ikhlasi) Mwenyezi Mungu ibada, kutokana na usemi wao: 'Alikikabidhi (sallama) kitu kwa fulani' yaani alikifanya kuwa chake pekee... Na katika Hadith: Hakuna binadamu yeyote ila anaye shetani naye. Ikasemwa: Na wewe pia? Akasema: Ndiyo, lakini Mwenyezi Mungu amenisaidia dhidi yake, naye akasilimu (fa-aslama), na katika riwaya nyingine: Mpaka akatii (aslama), yaani alinyenyekea na akaacha kunifanyia wasiwasi..."].
b- [Al-Muhit fi al-Lughah (2/265):
"Na al-Islam: Kujisalimisha kwa amri ya Allah na unyenyekevu katika kumtii Yeye. Na wanasema: Tulijisalimisha (sallamna) kwa Allah Mola wetu: Yaani tulijisalimisha Kwake na tukasilimu (aslamna). Na as-Salamu pia ni al-Islam. Na al-Muslim ni mwenye kujisalimisha..."].
Hivyo, Uislamu kilugha ni kujisalimisha, unyenyekevu na ikhlasi. Na kwa upande wa Mwenyezi Mungu (swt), ni unyenyekevu, kunyenyekea na kujisalimisha kwa Allah, na pia ni kuwa na ikhlasi kwa Ajili Yake (swt).
Matumizi ya maandiko ya kisheria (Nusus) ya neno Uislamu kwa maana ya kilugha:
Maandiko ya kisheria yametumia neno Uislamu na mnyambuliko wake katika sehemu mbalimbali kwa maana hiyo ya kilugha iliyotajwa hapo juu. Tutataja sehemu mbili za maandiko hayo kama mifano:
a- Kauli yake Allah Taala:
وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا إِنَّكَ أَنْتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ * رَبَّنَا وَاجْععلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِنْ ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُسْلِمَةً لَكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَا إِنَّكَ أَنْتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ * رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولاً مِنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ إِنَّكَ أَنْتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ * وَمَنْ يَرْغَبُ عَنْ مِلَّةِ إِبْرَاهِيمَ إِلَّا مَنْ سَفِهَ نَفْسَهُ وَلَقَدِ اصْطَفَيْنَاهُ فِي الدُّنْيَا وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ * إِذْ قَالَ لَهُ رَبُّهُ أَسْلِمْ قَالَ أَسْلَمْتُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ * وَوَصَّى بِهَا إِبْرَاهِيمُ بَنِيهِ وَيَعْقُوبُ يَابَنِيَّ إِنَّ اللَّهَ اصْطَفَى لَكُمُ الدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنْتُمْ مُسْلِمُونَ * أَمْ كُنْتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِنْ بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَهَكَ وَإِلَهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَهاً وَاحِداً وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ * تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُمْ مَا كَسَبْتُمْ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ
"Na pale Ibrahim na Ismail walipoinua kuta za Nyumba (wakajenga Kaaba, huku wakiomba): Mola wetu! Tutakalie (kitendo hiki), hakika Wewe ndiye Msikiaji, Mjuzi. Mola wetu! Tujaalie tuwe Waislamu (wenye kujisalimisha) Kwako, na katika kizazi chetu (pia) kuwe na umma wa Waislamu (wenye kujisalimisha) Kwako, na utuonyeshe ibada zetu na utusamehe. Hakika Wewe ndiye Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu. Mola wetu! Waletee Mtume anayetokana na wao, awasomee Aya Zako, na awafundishe Kitabu na hikima, na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. Na nani atakayejitenga na mila ya Ibrahim isipokuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa hakika Sisi tulimteua yeye duniani, na hakika yeye Akhera ni miongoni mwa watu wema. Mola wake alipomwambia: 'Silimu (jisalimishe)', akasema: 'Nimesalimu (nimejisalimisha) kwa Mola wa walimwengu'. Na Ibrahim aliwausia haya wanawe, na pia Ya’qub (akawausia wanawe akisema): 'Enyi wanangu! Hakika Allah amekuchagulieni dini hii; basi msife isipokuwa nanyi ni Waislamu (wenye kujisalimisha)'. Je, mlikuwa mashahidi wakati mauti yalipomfika Ya’qub, alipowaambia wanawe: 'Mtaabudu nini baada yangu?' Wakasema: 'Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Ishaq, Mungu Mmoja tu, na sisi Kwake ni Waislamu (tumejisalimisha)'. Huo ni umma uliokwisha pita. Utapata yale uliyoyachuma, nanyi mtapata yale mliyoyachuma. Wala hamtaulizwa juu ya yale waliyokuwa wakiyatenda." (QS. Al-Baqarah [2]: 127-134)
Lafudhi zote katika aya hizi zenye uhusiano na neno la Uislamu: (muslimayn, muslimah, aslim, aslamtu, muslimun, muslimun), ni kwa maana ya kilugha ya lafudhi ya Uislamu, yaani kujisalimisha, unyenyekevu na ikhlasi kwa Allah (swt). Na inafafanua ukweli wa jambo hili yale yaliyokuja katika vitabu vya tafsir kuhusu maana za aya hizi, na nanukuu tafsir fupi kutoka Tafsir al-Nasafi:
[Tafsir al-Nasafi (1/76):
"﴿رَبَّنَا واجعلنا مُسْلِمَيْنِ لَكَ﴾ yaani wenye ikhlasi Kwako kwa nyuso zetu, kutokana na kauli Yake: ﴿أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّهِ﴾ au wenye kujisalimisha, inasemekana alijisalimisha kwake ikiwa alinyenyekea na kufuata, na maana yake ni: Tuzidishie ikhlasi na utii Kwako. ﴿وَمِن ذُرّيَّتِنَا﴾ na fanya kutokana na kizazi chetu ﴿أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ﴾... na ikasemwa: Alikusudia kwa umma huo, umma wa Muhammad (saw)... ﴿إِذْ قَالَ لَهُ رَبُّهُ أَسْلِمْ﴾ yaani nyenyekea au tii au itakase dini yako kwa ajili ya Allah ﴿قَالَ أَسْلَمْتُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ﴾ yaani nimefanya ikhlasi au nimenyenyekea...
﴿فَلاَ تَمُوتُنَّ إَلاَّ وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ﴾ basi kifo chenu kisiwe isipokuwa mkiwa katika hali ya kudumu juu ya Uislamu... ﴿وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ﴾ kwa Allah ni wenye ikhlasi..."] Mwisho.
b- Kauli yake Allah Taala:
وَإِذْ أَوْحَيْتُ إِلَى الْحَوَارِيِّينَ أَنْ آمِنُوا بِي وَبِرَسُولِي قَالُوا آمَنَّا وَاشْهَدْ بِأَنَّنَا مُسْلِمُونَ
"Na pale nilipowafunulia Wanafunzi (wa Nabii Isa): 'Niaminini Mimi na Mtume Wangu', wakasema: 'Tumeamini, na shuhudia kuwa sisi ni Waislamu (tumejisalimisha)'." (QS. Al-Ma'idah [5]: 111)
Na ni wazi kutokana na aya hiyo kuwa mazungumzo ni kuhusu Hawariyyun (wanafunzi) wafuasi wa Isa (as) na kwamba walisema wao ni Waislamu, yaani wenye kujisalimisha na kutii amri ya Mwenyezi Mungu na wenye ikhlasi Kwake... Na imekuja katika Tafsir al-Nasafi ya aya hii yafuatayo:
[Tafsir al-Nasafi (1/314):
"﴿وَإِذْ أَوْحَيْتُ﴾ nilivuvia ﴿إِلَى الْحَوَارِيِّينَ﴾ watu maalumu au wateule ﴿أَنْ آمِنُوا﴾ yaani aminini ﴿بِي وَبِرَسُولِي قَالُوا آمَنَّا وَاشْهَدْ بِأَنَّنَا مُسْلِمُونَ﴾ yaani shuhudia kuwa sisi ni wenye ikhlasi miongoni mwa waliojisalimisha nyuso zao"].
Pili: Matumizi ya Kiistilahi ya neno Uislamu (Ukweli wa Kisheria):
Kama tulivyotaja hapo awali, maandiko ya kisheria yametumia neno Uislamu kwa maana yake ya kiistilahi, yaani kama jina la dini aliyoteremshiwa Muhammad ﷺ. Tunatoa mifano miwili ya hilo:
a- Kauli yake Allah Taala:
الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِيناً
"Leo waliofuta wamekata tamaa na dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamilishieni dini yenu, na nimekutimizieni neema Yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu." (QS. Al-Ma'idah [5]: 3)
Na imekuja katika Tafsir Ibn Kathir yafuatayo kuhusu aya hii:
[Tafsir Ibn Kathir (3/26):
"Na kauli Yake: ﴿الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإسْلامَ دِيناً﴾ hii ni neema kubwa zaidi ya Allah (swt) juu ya umma huu, ambapo Allah (taala) amewakamilishia dini yao, hivyo hawahitaji dini nyingine isipokuwa yake, wala mtume mwingine isipokuwa Mtume wao ﷺ; na kwa sababu hiyo Allah amemfanya kuwa khatam (mwisho) wa Mitume, na akamtuma kwa wanadamu na majini. Hivyo hakuna halali isipokuwa alichokihalalisha, wala haramu isipokuwa alichokiharamisha, wala dini isipokuwa aliyoishiria, na kila kitu alichokieleza ni ukweli na haki hakina uongo ndani yake wala kinyume chake, kama Alivyosema Allah Taala: ﴿وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقاً وَعَدْلا﴾ yaani: ukweli katika habari, na uadilifu katika amri na makatazo. Dini ilipokamilika kwao, neema ilitimizwa juu yao; na kwa ajili hiyo Allah Taala akasema ﴿الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإسْلامَ دِيناً﴾ yaani: basi ipendezeni kwa ajili yenu wenyewe, kwani hiyo ndiyo dini aliyoipenda Allah na akaipenda na akamtuma kwayo bora ya mitume Wake watukufu, na akateremsha kwayo kitabu Chake kitukufu zaidi. Ali bin Abi Talha amepokea kutoka kwa Ibn Abbas kauli yake: ﴿الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ﴾ nayo ni Uislamu, Allah amemueleza Mtume Wake ﷺ na waumini kuwa Amewakamilishia imani, hivyo hawahitaji nyongeza kamwe, na Allah ameitimiza hivyo haitaungua kamwe, na Allah ameipenda hivyo hataichukia kamwe."] Mwisho.
Na ni wazi kutokana na mtiririko wa aya kuwa mazungumzo ni kuhusu dini aliyoiteremsha Allah (tbwt) kwa Mtume Wake Muhammad, akaikamilisha, akaitimiza na akaipendelea kwa Waislamu.
b- Alipokea Bukhari katika Sahih yake kutoka kwa Ibn Umar (ra) amesema: Amesema Mtume wa Allah ﷺ:
«بُنِيَ الْإِسْلَامُ عَلَى خَمْسٍ شَهَادَةِ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللَّهِ وَإِقَامِ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ وَالْحَجِّ وَصَوْمِ رَمَضَانَ»
"Uislamu umejengwa juu ya mambo matano: Kushuhudia kuwa hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah, na kusimamisha Sala, na kutoa Zaka, na Hijja, na kufunga Ramadhani."
Na ni wazi kutokana na hadith hii tukufu kuwa maneno ni kuhusu dini ya Uislamu ambayo Allah aliiteremsha kwa Mtume Wake Muhammad ﷺ na kwamba hayo matano yaliyotajwa ni nguzo zake, kama ilivyokuja katika hadith nyingine.
Hakika yale yaliyokuja katika kitabu Nizham al-Islam katika nukuu iliyo hapo juu ni kuhusu Uislamu kwa maana ya kiistilahi (Ukweli wa Kisheria), na amehakikisha kufafanua Uislamu kwa namna inayodhihirisha ukamilifu wa Sharia ya Kiislamu katika nyanja zote za maisha. Amewasilisha katika ufafanuzi kuwa Uislamu ni dini aliyoteremshiwa Bwana wetu Muhammad ﷺ ili kupanga uhusiano wa mwanadamu na Muumba wake, na nafsi yake na binadamu wengine, na hivyo haikuacha uhusiano wowote unaowezekana wa mwanadamu isipokuwa iliupanga na kuuwekea hukumu.
Tatu: Uislamu na Dini za Mitume:
Hakika Uislamu kwa maana yake ya kilugha kwa upande wa Mwenyezi Mungu (swt), yaani kujisalimisha na unyenyekevu kwa Allah, na ikhlasi Kwake, ni sifa ya dini ya mitume wote tangu Adam mpaka kwa Mtume wetu Muhammad ﷺ. Hivyo mitume wote walikuwa katika Uislamu:
a- Imekuja kwa upande wa Ibrahim (as) katika Qur'ani Tukufu:
﴿إِذْ قَالَ لَهُ رَبُّهُ أَسْلِمْ قَالَ أَسْلَمْتُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ﴾.
b- Na imekuja kwa upande wa Ya’qub (as) na wanawe:
﴿وَوَصَّى بِهَا إِبْرَاهِيمُ بَنِيهِ وَيَعْقُوبُ يَا بَنِيَّ إِنَّ اللَّهَ اصْطَفَى لَكُمُ الدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنْتُمْ مُسْلِمُونَ * أَمْ كُنْتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِنْ بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَهَكَ وَإِلَهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَهاً وَاحِداً وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ﴾.
c- Na kwa upande wa Yusuf (as):
﴿تَوَفَّنِي مُسْلِماً وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ﴾.
d- Na kwa upande wa Musa (as) na wafuasi wake, na pia kwa upande wa wachawi walioamini:
﴿وَقَالَ مُوسَى يَا قَوْمِ إِنْ كُنْتُمْ آمَنْتُمْ بِاللَّهِ فَعَلَيْهِ تَوَكَّلُوا إِنْ كُنْتُمْ مُسْلِمِينَ﴾, ﴿وَمَا تَنْقِمُ مِنَّا إِلَّا أَنْ آمَنَّا بِآيَاتِ رَبِّنَا لَمَّا جَاءَتْنَا رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْراً وَتَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ﴾.
e- Na kwa upande wa Suleiman (as):
﴿فَلَمَّا جَاءَتْ قِيلَ أَهَكَذَا عَرْشُكِ قَالَتْ كَأَنَّهُ هُوَ وَأُوتِينَا الْعِلْمَ مِنْ قَبْلِهَا وَكُنَّا مُسْلِمِينَ﴾.
f- Na kwa upande wa Isa (as) na wasaidizi wake:
﴿فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَى مِنْهُمُ الْكُفْرَ قَالَ مَنْ أَنْصَارِي إِلَى اللَّهِ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنْصَارُ اللَّهِ آمَنَّا بِاللَّهِ وَاشْهَدْ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ﴾.
g- Na kwa upande wa Watu wa Kitabu:
﴿الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِهِ هُمْ بِهِ يُؤْمِنُونَ * وَإِذَا يُتْلَى عَلَيْهِمْ قَالُوا آمَنَّا بِهِ إِنَّهُ الْحَقُّ مِنْ رَبِّنَا إِنَّا كُنَّا مِنْ قَبْلِهِ مُسْلِمِينَ﴾.
Hivyo basi, Uislamu kwa maana ya kujisalimisha na unyenyekevu kwa Allah (swt) na ikhlasi Kwake, ni sifa ya dini ya mitume wote.
Na ama kwa maana ya kiistilahi ya kisheria, ni kama ilivyokuja katika Nizham al-Islam:
"[Uislamu ni dini ambayo Mwenyezi Mungu aliiteremsha kwa Bwana wetu Muhammad ﷺ ili kupanga uhusiano wa mwanadamu na Muumba wake, na nafsi yake, na binadamu wenzake. Na uhusiano wa mwanadamu na Muumba wake unajumuisha itikadi na ibada; na uhusiano wake na nafsi yake unajumuisha maadili, vyakula na mavazi; na uhusiano wake na binadamu wenzake unajumuisha miamala na adhabu.] Mwisho", na dalili za hilo ni nyingi na zenye kukata, na tumebainisha baadhi yake hapo juu...
Natumai katika jibu hili kuna utoshelevu, na Allah ni Mjuzi zaidi na Mwenye hikima zaidi.
Ndugu yenu, Ata bin Khalil Abu al-Rashtah
08 Jumada al-Akhirah 1444 H Inayoambatana na 01/01/2023 M
Link ya jibu kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Amir (Allah amhifadhi): Facebook