Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jawabu la Swali: Eneo Muhimu (Vital Sphere) Katika Siasa za Kimataifa

August 26, 2019
3569

Mfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Mkubwa Ata bin Khalil Abu al-Rashtah, Ameer wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook "Siyasi"

Jawabu la Swali

Kwa Muhammad Ayad

Swali:

Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,

Mwenyezi Mungu akusaidieni na ajalie kheri kupitia mikono yenu na mikono yetu, na Mwenyezi Mungu atutukuze kwa Khilafah ya pili na atujalie kuwa miongoni mwa mashahidi wake na wanajeshi wake.

Mada: Eneo Muhimu (Vital Sphere) katika Siasa za Kimataifa.

Dola zinazofanya kazi na dola kubwa huainisha upeo wa utendaji kazi ambao huupa kipaumbele katika kufikia maslahi yake, ukiitwa "Vital Sphere". Vivyo hivyo, Chama huweka eneo la utendaji kazi katika nchi moja au nchi kadhaa mpaka kistawi hapo na kusimamisha Dola ya Kiislamu.

Swali: Je, ni lazima kwa Khalifa ajaye, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kuainisha eneo muhimu kwa Dola ya Kiislamu ambalo atalipa kipaumbele kwa ajili ya kueneza Uislamu ulimwenguni kwa Da'wah na Jihad? Mwenyezi Mungu akulipe kheri kwa niaba yetu.

Jibu:

Wa Alaikum Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh,

Mwenyezi Mungu akubarikie kwa dua yako njema kwetu, na sisi tunakuombea kheri...

Hakika kile ulichokiita katika swali lako kwa neno "eneo muhimu" (vital sphere) kwa maana uliyoashiria ni jambo muhimu sana kwa dola yoyote inayofanya kazi katika uwanja wa kimataifa... Na Dola ya Khilafah ni dola ya kimisingi/kiitikadi (mabda’iy), na ni dola ya ulimwengu mzima si dola ya ndani tu; kwa sababu itikadi yake ni ya ulimwengu mzima, kwani ni itikadi kwa ajili ya mwanadamu, na kwa sababu mfumo wake ni mfumo wa kimataifa, kwani ni mfumo kwa ajili ya mwanadamu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِلنَّاسِ بَشِيراً وَنَذِيراً

"Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri na mwonyaji." (QS Saba' [34]: 28)

Na amepokea Bukhari kutoka kwa Jabir bin Abdullah amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«أُعْطِيتُ خَمْساً لَمْ يُعْطَهُنَّ أَحَدٌ مِنْ الْأَنْبِيَاءِ قَبْلِي نُصِرْتُ بِالرُّعْبِ مَسِيرَةَ شَهْرٍ وَجُعِلَتْ لِي الْأَرْضُ مَسْجِداً وَطَهُوراً وَأَيُّمَا رَجُلٍ مِنْ أُمَّتِي أَدْرَكَتْهُ الصَّلَاةُ فَلْيُصَلِّ وَأُحِلَّتْ لِي الْغَنَائِمُ وَكَانَ النَّبِيُّ يُبْعَثُ إِلَى قَوْمِهِ خَاصَّةً وَبُعِثْتُ إِلَى النَّاسِ كَافَّةً وَأُعْطِيتُ الشَّفَاعَةَ»

"Nimepewa mambo matano ambayo hakupewa yeyote katika Mitume kabla yangu: Nimenusuriwa kwa kutia hofu (kwa adui) safari ya mwezi mmoja, na nimefanyiwa ardhi kuwa msikiti na yenye kutwaharisha, basi mtu yeyote katika umma wangu akifikiwa na swala basi aswali, na nimehalalishiwa ngawira, na alikuwa Nabii akitumwa kwa watu wake mahususi na mimi nmetumwa kwa watu wote, na nimepewa uombezi (shafaa)."

Pamoja na kwamba Dola ya Khilafah hutazama ulimwengu mzima na kuufanya ulimwengu mzima kuwa sehemu ya siasa na matendo yake kama inavyoonekana katika hadith iliyopokewa na Ibn Majah katika Sunan yake kutoka kwa Thawban, mtumwa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«زُوِيَتْ لِي الْأَرْضُ حَتَّى رَأَيْتُ مَشَارِقَهَا وَمَغَارِبَهَا وَأُعْطِيتُ الْكَنْزَيْنِ الْأَصْفَرَ أَوْ الْأَحْمَرَ وَالْأَبْيَضَ يَعْنِي الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَقِيلَ لِي إِنَّ مُلْكَكَ إِلَى حَيْثُ زُوِيَ لَكَ...»

"Ardhi imekunjwa (imekusanywa) kwa ajili yangu mpaka nikaona mashariki yake na magharibi yake, na nimepewa hazina mbili; ya njano au nyekundu na nyeupe, yaani dhahabu na fedha. Na nimeambiwa kuwa utawala wako utafika kule uliofanyiwa ukunjaji..."

Hata hivyo, hiyo haimaanishi kuwa mipango inayowekwa na Dola ya Khilafah katika siasa za kigeni iwe sawa kwa nchi zote, wala haimaanishi kuwa nchi na maeneo yote duniani yapate kiasi kile kile cha umuhimu kutoka kwa Dola ya Khilafah. Bali, Dola ya Khilafah huweka eneo muhimu (vital sphere) kwake kulingana na maslahi ya Da'wah na hali halisi ya kisiasa, kiuchumi na kijeshi iliyopo, na hujitahidi kutekeleza siasa zake kwa kiasi kikubwa zaidi na kwa umakini zaidi katika eneo muhimu ililojiainishia yenyewe... Na eneo hili muhimu hubadilika kulingana na kufikiwa kwa malengo, mabadiliko ya uhalisia na maslahi ya Da'wah... n.k.

Kwa kufuatilia wasifu wa Mtume (saw) na maswahaba zake watukufu (ra), inabainika kuwa Mtume (saw) alifanya Bara la Arabuni kuwa eneo muhimu la dola baada ya kuisimamisha Madina Munawwarah. Kisha, haikupita muda baada ya kupata ushindi mwingi katika Bara la Arabuni, akapanua eneo muhimu la dola ili kujumuisha kingo za nchi za Sham na Iraq... Kisha wakaja Makhalifa Waongofu baada yake, na eneo muhimu la dola likapanuka baada ya kupatikana kwa mwanzo wa ufunguzi (futuhat) ili kujumuisha Sham, Iraq, Uajemi, kisha Misri, kaskazini mwa Afrika na maeneo mengine... Hivyo ndivyo eneo muhimu la Dola ya Khilafah lilivyokuwa likibadilika na kupanuka kulingana na ushindi uliokuwa ukipatikana na Dola na kulingana na mabadiliko ya hali na mazingira...

Kwa mujibu wa hayo, Dola ya Khilafah ya pili iliyoongoka itakaposimama kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, itarejesha wasifu wa Dola ya kwanza ya Kiislamu inshaAllah. Itaweka mipango na kuchora mikakati mwafaka na itachukua eneo muhimu linaloendana na maslahi ya Da'wah, uhalisia na mazingira... Na itachukua njia (* وسائل*) na mbinu (أساليب) zinazohitajika kwa ajili ya kubeba Uislamu na kuueneza duniani ikizingatia eneo muhimu ililojiainishia, na itatazama upya eneo hili muhimu kulingana na maslahi ya Da'wah na mabadiliko yatakayojitokeza, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Imeelezwa katika kitabu The Islamic State (Dola ya Kiislamu) katika mlango wa "Siasa za Kigeni za Dola ya Kiislamu" kile kinachoashiria kuzingatia kwa dola mazingira yaliyopo katika kuweka mipango na mbinu za kutekeleza siasa zake:

[Kwa msingi huo, fikra ya kisiasa ambayo inajenga uhusiano wa Dola ya Kiislamu na dola nyingine, mataifa na umma ni kueneza Uislamu miongoni mwao na kuwabeba Da'wah, na njia ya kufanya hivyo ni Jihad. Hata hivyo, kuna mipango na mbinu zinazowekwa na dola na kuwekewa njia na nyenzo za utekelezaji. Kwa mfano, hufanya mikataba ya ujirani mwema kwa muda maalumu na baadhi ya maadui na kupigana na wengine, kama alivyofanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipowasili Madina mara ya kwanza. Au kutangaza vita dhidi ya maadui zake wote, kama alivyofanya Abu Bakr alipoelekeza majeshi Iraq na Sham kwa wakati mmoja. Au kufanya mikataba ya muda ili kuweza kutengeneza maoni ya umma kwa ajili ya Da'wah, kama alivyofanya Mtume (saw) katika mkataba wa Hudaybiyah... Na dola inaweza kufanya mikataba ya kibiashara na baadhi ya nchi na kutoifanya na nchi nyingine kwa msingi wa maslahi ya Da'wah. Inaweza kuanzisha uhusiano na baadhi ya nchi na kutoanzisha na nyingine kulingana na mpango uliochorwa wa Da'wah. Inaweza kufuata mbinu za Da'wah na propaganda na baadhi ya nchi, wakati ikifuata mbinu za kufichua mipango na vita baridi na nchi nyingine. Hivyo ndivyo dola inavyoweka mipango na kutekeleza mbinu kulingana na kile kinachoamuliwa na aina ya kazi na kinachohitajika na maslahi ya Da'wah... Lakini yote hayo ni kwa ajili ya kueneza Uislamu kupitia njia yake ya kuuenea ambayo ni Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu.] Mwisho wa nukuu. Na kuchukua eneo muhimu kwa dola si jambo geni na maneno haya yaliyonukuliwa kutoka kitabu The Islamic State.

Pokea salamu zangu.

Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah

25 Dhul-Hijjah 1440 H Inalingana na 26/08/2019 M

Link ya jibu kutoka kwa ukurasa wa Ameer (Mungu amuhifadhi) kwenye Facebook

Link ya jibu kutoka ukurasa wa Ameer (Mungu amuhifadhi) kwenye Web

Share Article

Share this article with your network