Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni mtukufu Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir,
kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi"
Kwa Ahmed Benfetita
Swali:
Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh
Sheikh wetu mbora, Ata al-Khair, Allah akulinde na ayaongoze hatua zako,
Ni nini maana ya kuwa "viwanda vya aina zote viwe juu ya msingi wa siasa ya kivita"? Kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Ajhizat ad-Dawlah al-Khilafah (Katika Utawala na Usimamizi) "...na viwanda vya aina zote lazima vijengwe juu ya msingi wa siasa ya kivita."
Na je, kuna mifano ya jambo hilo?
Barakallahu fikum Amir wetu, na Allah akupe nguvu kwa jeshi Lake na msaada Wake, na ainusuru Umma wetu wa Kiislamu kupitia kwako.
Jibu:
Walaikum Assalam Warahmatullahi Wabarakatuh,
Hakika jibu la swali lako linapatikana katika kitabu cha Ajhizat ukurasa wa 107 (faili la Word) na pia katika kitabu cha Muqaddimat ad-Dustur Sehemu ya Kwanza ukurasa wa 232 (faili la Word), na ninakunukulia yale yaliyokuja kuhusiana na jambo hili:
[Na kwa kuwa Dola ya Kiislamu ni dola inayobeba Da'wah ya Kiislamu, kwa njia ya Da'wah na Jihad, basi itakuwa ni dola yenye utayari wa kudumu wa kutekeleza Jihad, na hili linapelekea kuwa sekta ya viwanda ndani yake, viwe vizito au vyepesi, ijengwe juu ya msingi wa siasa ya kivita, ili pindi itakapohitajika kuvibadilisha kuwa viwanda vinavyozalisha zana za kivita za kila aina iwe rahisi kwake kufanya hivyo wakati wowote itakapotaka; na kwa ajili hiyo ni lazima sekta yote ya viwanda katika Dola ya Khilafah ijengwe juu ya msingi wa siasa ya kivita, na viwanda vyote vijengwe, iwe ni vile vinavyozalisha bidhaa za viwanda vizito, au vile vinavyozalisha bidhaa za viwanda vyepesi, juu ya msingi wa siasa hii, ili iwe rahisi kubadilisha uzalishaji wake kuwa uzalishaji wa kivita wakati wowote dola inapohitaji kufanya hivyo.] Mwisho.
Hii ina maana kwamba viwanda vyote katika Dola ya Khilafah vinapaswa kuwekwa katika namna ambayo mzunguko wa uzalishaji unaweza kubadilishwa kwa urahisi ili kuzalisha bidhaa zinazohusiana na nyanja ya kivita tofauti na zile zinazozalishwa kwa kawaida. Kwa mfano, ikiwa kuna kiwanda cha magari ya kiraia, basi kinapaswa kujengwa kwa namna ambayo inawezekana kitaalamu na kivitendo kubadilisha mzunguko wa uzalishaji wake kwa ajili ya kutengeneza magari ya kijeshi yanayotumiwa na dola katika vita dhidi ya makafiri... Na kwa mfano, ikiwa kuna kiwanda cha nguo, basi kinapaswa kuwekwa kwa namna ambayo uzalishaji unaweza kubadilishwa kwa urahisi kuwa uzalishaji wa sare za kijeshi... Na hivyo ndivyo siasa ya ujenzi wa viwanda inavyokuwa imejengwa juu ya siasa ya kivita katika mzunguko wa uzalishaji, katika majengo ya viwanda, katika uwezekano wa kujilinda dhidi ya mashambulizi, na uwezekano wa kufanya kazi ndani yake katika majengo yaliyo chini ya ardhi... n.k., miongoni mwa mambo yanayopangwa na wataalamu na kusimamiwa na dola.
Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah
15 Muharram al-Haram 1445 AH Sawa na 02/08/2023 CE
Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir (Allah amuhifadhi) kwenye Facebook