Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: An-Nasikh wal-Mansukh

November 27, 2018
7016

(Silsila ya Majibu ya Mwanachuoni Mtukufu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa Maswali ya Wageni kwenye Ukurasa Wake wa Facebook "Fikhi")

Kwa Al-Mawaridi

Swali:

Question is,

Tulijadiliana kuhusu mbinu yetu ya kusimamisha tena Khilafah na ndugu mmoja. Nilipewa jibu na ndugu huyo kwamba kufanya vitendo vya kisiasa non-violent (bila kutumia nguvu) na kutafuta Nusrah mjini Makka kabla ya Hijra kulifutwa (abrogated) na aya ya Qur’an ambayo ni:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ قِيلَ لَهُمْ كُفُّوا أَيْدِيَكُمْ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَخْشَوْنَ النَّاسَ كَخَشْيَةِ اللَّهِ أَوْ أَشَدَّ خَشْيَةً وَقَالُوا رَبَّنَا لِمَ كَتَبْتَ عَلَيْنَا الْقِتَالَ لَوْلَا أَخَّرْتَنَا إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ قُلْ مَتَاعُ الدُّنْيَا قَلِيلٌ وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّمَنِ اتَّقَىٰ وَلَا تُظْلَمُونَ فَتِيلًا

"Je! Huwaoni wale walio ambiwa: Zuieni mikono yenu, na shikeni Sala, na toeni Zaka. Na walipo faradhiwa kupigana, mara kundi moja miongoni mwao likawaogopa watu kama kumwogopa Mwenyezi Mungu, au kwa khofu kubwa zaidi. Na wakasema: Mola wetu Mlezi! Kwa nini umetufaradhia kupigana? Mbona hukuatupa muhula mpaka muda ukaribu? Sema: Starehe ya dunia ni kidogo, na Akhera ni bora zaidi kwa mwenye kumcha Mungu. Wala hamtadhulumiwa hata kadiri ya uzi wa kokwa ya tende." (QS. An-Nisa [4]: 77)

Katika aya hii, Mwenyezi Mungu aliamrisha kufanya Jihad ambayo ilifuta (abrogated) Hukmu ya awali (kuzuia mikono yao). Hivyo basi, ni jibu gani nitakalotoa kwa ndugu huyo. Jazakallahu Khair ndugu yangu.

Kutoka kwa Ndugu yako, Asif Sulaiman

Jibu:

Wa Alaikum Salaam wa Rahmatullahi wa Barakatuh,

Kwanza: Inaonekana kwamba huyo aliyekuuliza ana mkanganyiko katika maudhui ya An-Nasikh (kufuta hukmu), na ndiyo maana alidhani kuwa kufaradhishwa kwa Jihad mjini Madina ni kufutwa kwa kutokuruhusiwa kwa Mtume (saw) kufanya Jihad mjini Makka. Ukweli wa mambo ni kwamba hakuna kufutwa kwa hukmu (Nasikh), na hiyo ni kwa sababu An-Nasikh hutokea pale inapokuja khitabu ya jumla kutoka kwa Mwenye Sheria (Ash-Shari') inayotulazimisha kufanya kitendo fulani, kisha inakuja baada yake khitabu nyingine ya jumla kutoka kwa Mwenye Sheria inayozuia kuendelea kwa hukmu iliyothibiti katika khitabu ya kisheria ya awali, na kuwe na mgongano (ta’arudhu) kwa kila upande, bila uwezekano wa kuchanganya (jam’u) kati ya khitabu hizo mbili, na mazingira ya khitabu ya awali au hali iliyoshughulikiwa na khitabu ya awali isiwe tofauti na mazingira na hali ya khitabu ya baadaye. Vinginevyo, kila khitabu itakuwa maalum kwa mazingira na hali yake... Na ili kufafanua hilo, nitakutajia mifano:

1- Mifano ya Nasikh (Kufutwa kwa Hukmu):

a- Kufutwa kwa wajibu wa kuelekea Jerusalem (Al-Quds) na kuelekea Al-Kaaba:

قَدْ نَرَى تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاءِ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَحَيْثُ مَا كُنْتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ

"Hakika tunaona unavyo geuza geuza uso wako mbinguni. Basi tutakuelekeza kwenye Kibla ukipendacho. Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo, elekezeni nyuso zenu upande huo." (QS. Al-Baqarah [2]: 144)

Hapa mazingira na hali ya kuelekea Kibla cha kwanza na Kibla cha pili ni moja kwa ajili ya anayeswali...

b- Kufutwa kwa katazo la kuzuru makaburi na kuruhusiwa kwake:

كُنْتُ نَهَيْتُكُمْ عَنْ زِيَارَةِ الْقُبُورِ أَلا فَزُورُوهَا

"Nilikuwa nimewakataza kuzuru makaburi, basi sasa yazuruni."

Pia hapa, mazingira na hali ya kuzuru makaburi na kutokuzuru ni moja...

Mifano hii yote imetokea An-Nasikh kwa sababu ni khitabu ya jumla iliyoelekezwa kwa Waislamu, na mazingira ya khitabu ya awali na ya baadaye ni mamoja, na mgongano kati yake ni kwa kila upande, yaani haiwezekani kuvichanganya pamoja, na hivyo basi khitabu ya baadaye inakuwa ni yenye kufuta (nasikh) khitabu ya awali.

2- Mifano ya kutokuwepo kwa Nasikh:

  • Saumu ni faradhi kwa mwenye uwezo:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ أَيَّامًا مَعْدُودَاتٍ

"Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu kama walivyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kucha Mungu. Siku zilizo hisabiwa." (QS. Al-Baqarah [2]: 183-184)

  • Na kwa mgonjwa au aliye safarini, anaruhusiwa kula:

فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ

"Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yuko safarini, basi (atimize) hisabu katika siku nyingine. Na wale wasio weza, watoe fidia kwa kumlisha masikini." (QS. Al-Baqarah [2]: 184)

Hapa haisemwi kuwa aya ya pili imefuta aya ya kwanza, bali inasemwa kuwa kila hukmu inatumika kulingana na mazingira na hali yake; hivyo kufunga ni faradhi kwa mwenye mwili mzima aliyeko nyumbani, lakini kula kunaruhusiwa kwa mgonjwa au aliyeko safarini. Au inasemwa khitabu ya aya ya kwanza ni ya jumla kwa Waislamu na khitabu ya aya ya pili ni mahususi kwa mgonjwa au msafiri...

Pili: Kuhusu aya tukufu iliyozungumziwa katika swali, hakuna kufutwa kwa hukmu (Nasikh) ndani yake. Mazingira ya Waislamu mjini Makka yalikuwa ni kuwa wao ni wanyonge... wakiteswa na kuishi chini ya mamlaka ya makafiri. Hivyo kwa hekima anayoijua Mwenyezi Mungu, hakuwafungia Jihad... Na ndiyo maana Mtume (saw) hakuwaruhusu kikundi kile cha Waislamu kupigana walipomuhimiza mjini Makka... Al-Hakim ametoa katika Al-Mustadrak na akasema hii ni hadithi sahihi kwa sharti ya Al-Bukhari: kutoka kwa Ikrimah, kutoka kwa Ibn Abbas (ra), kwamba Abdurrahman bin Awf na masahaba zake walimjia Mtume (saw) na kusema: "Ewe Nabii wa Allah, tulikuwa katika utukufu tulipokuwa washirikina, na tulipomini tumekuwa wanyonge." Akasema: "Hakika mimi nimeamrishwa kusamehe, basi msipigane na watu." Lakini alipohamia Madina, alimwamrisha kupigana, lakini wakajizuia, ndipo Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ قِيلَ لَهُمْ كُفُّوا أَيْدِيَكُمْ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ إِذَا فَرِيقٌ مِنْهُمْ يَخْشَوْنَ النَّاسَ...

"Je! Huwaoni wale walio ambiwa: Zuieni mikono yenu, na shikeni Sala, na toeni Zaka. Na walipo faradhiwa kupigana, mara kundi moja miongoni mwao likawaogopa watu..." (QS. An-Nisa [4]: 77)

Na mafuhumu ya aya hiyo ni kwamba tusifanye kama walivyofanya wao, yaani tusiwe na haraka ya kufaradhishwa kwa amri fulani kisha inapofaradhishwa tunasita kuitekeleza na tukawa miongoni mwa wenye kulaumiwa...

Hivyo basi, kwa sababu mazingira ni tofauti, tumesema hakuna Nasikh. Badala yake, hukmu ya Makka ilikuwa ni hali maalum ambapo Mwenyezi Mungu hakufaradhisha kupigana na makafiri katika siku zile kwa hekima anayoijua Mjuzi Mwenye Hekima... Ama mjini Madina, Mwenyezi Mungu amefaradhisha Jihad humo, na kuanzia tarehe hiyo, Jihad inaendelea hadi Siku ya Kiyama. Na ushahidi wa hilo ni:

  • Al-Bukhari ametenga mlango katika Sahih yake akauita: (MLANGO WA JIHAD INAENDELEA PAMOJA NA KIONGOZI MWEMA NA MUOVU KWA SABABU YA KAULI YA MTUME (SAW): FARASI WAMEFUNGWA KHERI KATIKA NYUSO ZAO HADI SIKU YA KIYAMA).

  • Na Al-Bukhari ametoa katika Sahih yake akisema, Abu Nu'aim ametuhadithia, Zakaria ametuhadithia, kutoka kwa Amir, Urwah al-Bariqi ametuhadithia kwamba Mtume (saw) amesema:

الْخَيْلُ مَعْقُودٌ فِي نَوَاصِيهَا الْخَيْرُ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ الْأَجْرُ وَالْمَغْنَمُ

"Farasi wamefungwa kheri katika nyuso zao hadi Siku ya Kiyama: malipo (ajira) na ghanima." Na Muslim pia ametoa hadithi hii.

Na maneno (Farasi wamefungwa katika nyuso zao) ni sitiari ya Jihad.

  • Na Al-Bayhaqi ametoa katika As-Sunan al-Kubra kutoka kwa Anas bin Malik (ra) amesema: Mtume wa Allah (saw) amesema:

ثَلاثٌ مِنْ أَصْلِ الإِيمَانِ، الْكَفُّ عَمَّنْ قَالَ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ، لا يُكَفِّرُهُ بِذَنْبٍ، وَلا يُخْرِجُهُ مِنَ الإِسْلامِ بِعَمَلٍ، وَالْجِهَادُ مَاضٍ مُنْذُ بَعَثَنِي اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ إِلَى أَنْ يُقَاتِلَ آخِرُ أُمَّتِي الدَّجَّالَ لا يُبْطِلُهُ جَوْرُ جَائِرٍ وَلا عَدْلُ عَادِلٍ، وَالإِيمَانُ بِالأَقْدَارِ

"Mambo matatu ni katika msingi wa imani: Kujizuia na aliyesema La ilaha illa Allah, usimkufurishe kwa dhambi yoyote, na usimtoe katika Uislamu kwa kitendo chochote; na Jihad inaendelea tangu Allah Aliponituma mpaka wa mwisho wa umma wangu watakapopigana na Dajjal, haibatilishwi na dhuluma ya dhalimu wala uadilifu wa mwadilifu; na kuamini Qadar."

Hivyo, Jihad inaendelea hadi Siku ya Kiyama, haifutwi (nasikh) wala haisitishwi. Kila kiongozi Mwislamu, awe Khalifah au la, akitangaza Jihad dhidi ya makafiri, basi anapiganwa naye dhidi ya makafiri hao, na wapiganaji watajaziwa thawabu mbele ya Allah kulingana na nia zao...

Tatu: Inaonekana aliyekuuliza au kujadiliana nawe kuhusu aya hii alitaka kukuambia: (Kwa nini Hizb ut-Tahrir haitumii Jihad katika kazi yake ya kusimamisha Khilafah, hali ya kuwa kutokupigana mjini Makka kulifutwa mjini Madina?) Ni kana kwamba amechanganya kati ya Jihad na kazi ya kusimamisha Khilafah akadhani kuwa ni suala moja, na huku ni kudhania kimakosa. Tayari tulishajibu mnamo tarehe 22/09/2013 swali lililotufikia kuhusu mada hii, na ninakunukulia baadhi ya yaliyokuja katika jibu hilo, kwani yana ufafanuzi zaidi kwa yule aliyekujadili katika suala hili, huenda akaongoka kwenye jambo la sawasawa akipenda Mwenyezi Mungu:

(Jibu: Katika swali hili kuna mambo kadhaa yanayohitaji ufafanuzi: 1- Ushahidi (Adillah) uliokuja, uwe ni kutoka katika Kitabu au Sunnah, ni wajibu kufuatwa jinsi ulivyo, na hakuna tofauti kati ya ushahidi uliokuja mjini Makka na uliokuja mjini Madina.

2- Ushahidi unaohitajika ni ule unaohusu suala lenyewe na si ushahidi wa suala jingine:

a- Kwa mfano, nikitaka kujua jinsi ya kutawadha, nitatafuta ushahidi wa udhu popote ulipo, uwe ulishuka Makka au Madina, na hukmu ya kisheria itatolewa kutoka humo kulingana na misingi (Usul) inayofuatwa... Lakini sitatafuta ushahidi wa Saumu ili kuchukua hukmu ya udhu na jinsi yake!

b- Na kwa mfano, nikitaka kujua hukmu za Hijja, kadhalika nitatafuta ushahidi wa Hijja popote ulipo, uwe ulishuka Makka au Madina, na hukmu ya kisheria itatolewa kutoka humo kulingana na misingi inayofuatwa, lakini sitatafuta ushahidi wa Sala ili kuchukua hukmu ya Hijja na jinsi yake!

c- Na kwa mfano, nikitaka kujua hukmu za Jihad: iwe ni Faradhi ya Kujitosheleza (Kifayah) au Faradhi ya Kila Mtu (Ayn), katika kujihami au kuanza, na yale yanayotokana na Jihad kama vile hukmu za ufunguzi (fath) na kueneza Uislamu, kufungua kwa nguvu au kwa suluhu... basi nitatafuta ushahidi wa Jihad popote ulipo, uwe ulishuka Makka au Madina, na hukmu ya kisheria itatolewa kutoka humo kulingana na misingi inayofuatwa, lakini sitatafuta ushahidi wa Zaka ili kuchukua hukmu ya Jihad na maelezo yake!

d- Na kadhalika katika kila suala, hutafutwa ushahidi wake popote ulipokuja, mjini Makka au Madina, na hukmu ya kisheria ya suala hilo huchukuliwa kutoka katika ushahidi huo kulingana na misingi inayofuatwa.

3- Na sasa tunakuja kwenye suala la kusimamisha Dola ya Kiislamu, na tunatafuta ushahidi wake, uwe ulishuka Makka au Madina, na tunatoa hukmu ya kisheria kutoka humo kulingana na misingi inayofuatwa.

Hakika hatupati ushahidi wowote wa kusimamisha Dola ya Kiislamu isipokuwa ule alioubayanisha Mtume wa Allah (saw) katika Sira yake mjini Makka.

Aliita watu kwenye Uislamu kwa siri, akatengeneza kundi (kutlah) la waumini wenye subira... kisha akaitangaza mbele ya watu mjini Makka na katika msimu wa Hijja... kisha akatafuta Nusrah kutoka kwa wenye nguvu na mamlaka, na Allah (swt) Akamkirimu kwa Maansari, akahamia kwao na kusimamisha Dola.

Huu ndio ushahidi wa kusimamisha Dola, na hakuna ushahidi mwingine. Mtume (saw) alitubainishia katika Sira yake ubainifu uliotosheleza, na ni wajibu kwetu kuushikilia. Hivyo basi, mada hii siyo kipindi cha Makka kabla ya kufaradhishwa Jihad na kipindi cha Madina baada ya kufaradhishwa Jihad, bali ni kutafuta ushahidi wa kusimamisha Dola, na huo haupo isipokuwa Makka hadi alipohamia Mtume (saw) Madina na kusimamisha Dola.

Hili (kusimamisha dola) ni jambo moja na Jihad ni jambo jingine. Na kama tulivyosema, ushahidi wa kusimamisha Dola unachukuliwa kutoka sehemu yake, na ushahidi wa Jihad unachukuliwa kutoka sehemu yake, na hiki ni tofauti na kile na moja haitegemei nyingine. Na ndiyo maana Jihad haisitishwi kwa kukosekana kwa Dola ya Khilafah...

Kadhalika, kazi ya kusimamisha Khilafah haisitishwi kwa sababu ya watawala kusitisha Jihad...

Kwa mujibu wa hayo, Jihad inaendelea, na kazi ya Khilafah inaendelea hadi itakaposimama, na moja haitegemei nyingine. Hayo ni masuala mawili, na kila suala hutafutiwa ushahidi wake wa kisheria, na hutolewa hukmu ya kisheria mahususi kwa suala hilo kulingana na misingi inayofuatwa...). Mwisho.

Natumai kuwa katika hayo kuna yale yanayotosha kumshawishi yule aliyekujadili ili aongoke kwenye jambo la sawasawa, In Shaa Allah.

Ndugu yenu, Ata bin Khalil Abu al-Rashtah

18 Rabi’ al-Awwal 1440 H Inayoambatana na 26/11/2018 M

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir (Allah amuhifadhi) kwenye Facebook

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir (Allah amuhifadhi) kwenye Google Plus

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir (Allah amuhifadhi) Web

Share Article

Share this article with your network