Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jawabu la Swali: Fi'il al-Amr

June 17, 2019
6625

Mfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Mtukufu Ata bin Khalil Abu al-Rashta, Ameir wa Hizb ut-Tahrir, kwa Maswali ya Wafuasi wa Ukurasa Wake wa Facebook "Fiqhi"

Jawabu la Swali

Fi'il al-Amr (Kitenzi cha Amri) Kwa: Abdul Rahman Al-Zayoud

Swali:

Ndugu mpendwa Ameir wetu, Mwenyezi Mungu akuhifadhi na kukulinda, na akusaidie kupitia kwa waumini wanyofu na wenye nguvu, na Mwenyezi Mungu akusaidie katika kubeba mzigo wako mzito, na atuunganishe nawe hivi karibuni tukishikana mikono nawe tukikubai kwa kusikia na kutii katika hali ya wepesi na uzito. Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh, na baada ya hayo:

Wakati nikiwa naandaa somo la Ash-Shakhsiyyah Juzuu ya Tatu kuhusu mada ya Fi'il (Kitenzi), ukurasa wa 168 toleo la kielektroniki, nilisimama kwenye maandiko yafuatayo (Ama fi'il al-amr ni kile ambacho harufi ya mudhara'ah imeondolewa kwake na si vinginevyo). Swali ni: Fi'il al-mudhari' yaf'alu inapoondolewa harufi ya mudhara'ah, je, si inakuwa ni kitenzi cha wakati uliopita (madhi)? Yaani, siyo kitenzi cha amri (amr).

Je, kuna maneno yaliyoanguka (yaliyosahaulika) wakati wa uchapishaji katika ibara yetu hii? Mwenyezi Mungu awabarikie, na muendelee kuwa katika ulinzi wa Mwenyezi Mungu.

Jibu:

Walaikum Assalam Warahmatullahi Wabarakatuh,

Mwenyezi Mungu akubarikie kwa dua yako nzuri, na namuomba Mwenyezi Mungu (swt) atujalie sisi na wewe mafanikio na usahihi.

Hakika kauli iliyomo katika kitabu cha Ash-Shakhsiyyah al-Islamiyyah Juzuu ya Tatu kuhusu fi'il al-amr: (Ama fi'il al-amr ni kile ambacho harufi ya mudhara'ah imeondolewa kwake na si vinginevyo) inapatikana katika vitabu vya Usul. Kwa mfano, imekuja katika Al-Ihkam fi Usul al-Ahkam cha Al-Amidi (1/58):

(Na kitenzi (fi'il) ni kile kinachoashiria tukio lililoambatana na wakati maalum... na wakati huo umegawanyika kulingana na mgawanyiko wa muda: wakati uliopita (madhi) kama qama na qa'ada.

Na wakati uliopo na ujao katika tamshi ni kitu kimoja na huitwa mudhari', nacho ni kile ambacho mwanzoni mwake mna moja ya harufi nne za ziada nazo ni: Hamza, Ta, Nun na Ya, kama kusema kwako: aqumu, taqumu, naqumu na yaqumu. Na kupambanua wakati ujao na wakati uliopo ni kwa kuingiliwa na "Sin" au "Sawfa" kama kusema kwako: sayaqumu na sawfa yaqumu. Ama fi'il al-amr ni kile ambacho harufi ya mudhara'ah imeondolewa kwake na si vinginevyo kama kusema kwako katika yaqumu: qum na mfano wake.) Mwisho.

Na kwa mfano, imekuja katika Sharh Alfiyyah Ibn Malik cha Al-Uthaymeen (3/11, kwa kufuata nambari za Ash-Shamila kiotomatiki):

[Mwandishi (r.h) amesema: (Kitenzi cha amri na wakati uliopita vimejengwa - buniya - na wakakifanya mudhari' kuwa na mabadiliko ya mwisho - mu'rab... ) kisha akasema: (Na kitenzi cha amri na wakati uliopita vimejengwa) yaani: kitenzi cha amri ni mabni, na wakati uliopita ni mabni...

Basi fi'il al-amr ni mabni, na inasemwa: ni mu'rab, lakini usahihi ni kwamba ni mabni, na hujengwa juu ya kile ambacho fi'il al-mudhari' yake hufanyiwa jazma (jazm). Ikiwa mudhari' yake inafanyiwa jazma kwa sukun, basi hujengwa juu ya sukun, na ikiwa mudhari' yake hujengwa kwa kuondolewa harufi ya ziada (harf al-'illah) au kuondolewa Nun, basi vivyo hivyo hujengwa juu ya kuondolewa harufi ya ziada au kuondolewa Nun. Na kwa sababu hii husema: Ikiwa unataka kuunda fi'il al-amr, basi leta fi'il al-mudhari' iliyofanyiwa jazma kisha ondoa harufi ya mudhara'ah na harufi ya jazma.] (Mwisho)

Ili kufafanua hilo kwa kutegemea utafiti wa kanuni za lugha katika vyanzo vyake, tunasema na kwa Mwenyezi Mungu ndio kuna mafanikio:

1- Fi'il al-amr huchukuliwa kiumbo kutoka kwa fi'il al-mudhari' baada ya kuondolewa kwa harufi ya mudhara'ah. Lakini kwa sababu fi'il al-amr ni majzum (yenye jazma), basi umbo lake huchukuliwa kutoka kwa fi'il al-mudhari' iliyofanyiwa jazma baada ya kuondolewa kwa harufi ya mudhara'ah, na bila shaka baada ya kuangusha chombo cha jazma (adat al-jazm) kwa sababu hiyo si sehemu ya kitenzi. Hivyo, ukitaka kufikia fi'il al-amr kutoka kwa fi'il al-mudhari', kwanza ingiza harufi ya jazma kama "lam" kwenye fi'il al-mudhari' ili iwe kitenzi kilichofanyiwa jazma (majzum), kisha angusha harufi ya jazma "lam" yaani bakisha umbo la jazma la fi'il al-mudhari' bila kile chombo cha jazma, kisha ondoa harufi ya mudhara'ah kutoka kwenye hiyo fi'il al-mudhari' iliyofanyiwa jazma, hapo kitachujika kwako kitenzi cha amri (fi'il al-amr)...

2- Kwa mfano, kitenzi "يخاف" (yakhafu) kinakuwa kwa kuingiza lam juu yake "لم يخَفْ" (lam yakhaf), na kwa kuangusha lam kinakuwa "يخَفْ" (yakhaf), na kwa kufuta harufi ya mudhara'ah "Ya" iliyoko mwanzo wa kitenzi kinakuwa "خَفْ" (khaf), nacho ni fi'il al-amr cha "خاف" (khafa). Na mfano wake ni vitenzi (yanamu, yaqumu, yaqulu, yazuru...).

3- Na kwa mfano, kitenzi "يفي" (yafi) kinakuwa kwa kuingiza lam juu yake "لم يفِ" (lam yafi), na kwa kuangusha lam kinakuwa "يفِ" (yafi), na kwa kufuta harufi ya mudhara'ah "Ya" iliyoko mwanzo wa kitenzi kinakuwa "فِ" (fi), nacho ni fi'il al-amr cha "وفى" (wafa). Na mfano wake ni vitenzi: (wa'a, waqa, ra'a...).

4- Na kwa mfano, kitenzi "يضرب" (yadribu) kinakuwa kwa kuingiza lam juu yake "لم يضْرِبْ" (lam yadrib), na kwa kuangusha lam kinakuwa "يضْرِبْ" (yadrib), na kwa kufuta harufi ya mudhara'ah "Ya" iliyoko mwanzo wa kitenzi kinakuwa "ضْرِبْ" (drib), lakini harufi ya kwanza ambayo ni Dhad ni harufi yenye sukun, na harufi yenye sukun haiwezekani kuanza kutamkwa isipokuwa kwa hamzatul wasl, hivyo inakuwa "اضْرِبْ" (idrib) nacho ni fi'il al-amr cha "ضرب" (daraba). Na mfano wake ni vitenzi: (amila, da'a, bana...).

5- Muhtasari ni kwamba ikiwa harufi ya mudhara'ah itaondolewa kutoka kwenye fi'il al-mudhari' iliyofanyiwa jazma, matokeo yake ni fi'il al-amr na wala si fi'il al-madhi. Na kwa hiyo, yale yaliyokuja katika kitabu cha Ash-Shakhsiyyah al-Islamiyyah Juzuu ya Tatu ni maneno sahihi kulingana na yaliyofafanuliwa hapo juu na hakuna "maneno yaliyoanguka wakati wa uchapishaji".

Natumai jambo hili sasa limekuwa wazi.

Ndugu yenu, Ata bin Khalil Abu al-Rashta

14 Shawwal 1440 H Sawa na 17/06/2019 M

Link ya jawabu kutoka kwenye ukurasa wa Ameir (Mungu amhifadhi) kwenye Facebook Link ya jawabu kutoka kwenye ukurasa wa Ameir (Mungu amhifadhi) kwenye Tovuti

Share Article

Share this article with your network