Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

JIBU LA SWALI: HUKUMU YA SWALA YA IJUMAA BILA KUWEPO KWA KHALIFAH

April 22, 2013
6604

Swali:

Katika mjadala na mtu mmoja, yeye anaswali swala za nyakati zote... lakini haswali Ijumaa pamoja na watu, bali anaswali adhuhuri. Nilipomkosoa kwa hilo, alisema kuwa kuwepo kwa Khalifa ni sharti la kusihi kwa Swala ya Ijumaa. Je, kuna yeyote kati ya mafaqihi anayesema hivi? Na nini maoni ya Hizb katika hilo? Jazakumullah Khayran.

Jibu:

Hakika Swala ya Ijumaa ni faradhi, iwe Khalifa yupo au hayupo, na dalili za hilo ni maarufu, miongoni mwazo ni:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِنْ يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَى ذِكْرِ اللَّهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ

"Enyi mlioamini! Ikitoewa adhana kwa ajili ya Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye kumdhukuru Mwenyezi Mungu na acheni biashara. Hivyo ni bora kwenu ikiwa nyinyi mwanajua." (QS. Al-Jumu'ah [62]: 9)

Na Al-Hakim ametoa katika Mustadrak yake kutoka kwa Abu Musa, kutoka kwa Mtume (saw) amesema:

الْجُمُعَةُ حَقٌّ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ فِي جَمَاعَةٍ إِلَّا أَرْبَعَةً: عَبْدٌ مَمْلُوكٌ، أَوِ امْرَأَةٌ، أَوْ صَبِيٌّ، أَوْ مَرِيضٌ

"Ijumaa ni haki ya lazima (faradhi) kwa kila Mwislamu katika jamaa isipokuwa watu wanne: mtumwa anayemilikiwa, mwanamke, mtoto, au mgonjwa."

Al-Hakim amesema: "Hii ni hadithi sahihi kwa sharti ya Masheikh wawili na hawakuitoa." Vilevile, An-Nasa'i ametoa kutoka kwa Ibn Umar, kutoka kwa Hafsa mke wa Mtume (saw) kwamba Mtume (saw) amesema:

رَوَاحُ الْجُمُعَةِ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُحْتَلِمٍ

"Kwenda kwenye Ijumaa ni wajibu kwa kila aliyebalehe."

Ni wazi kutokana na dalili hizi kwamba hazikufungwa na kuwepo kwa Imamu (Khalifa).

Na hivi ndivyo wanavyosema pia wenye madhehebu matatu (Malik, Shafi'i, na Ibn Hanbal). Ama upande wa Wa-Hanafi, wametaja miongoni mwa masharti ya Ijumaa:

(Idhini ya Sultani kwa hilo, au kuwepo kwake, au kuwepo kwa naibu wake rasmi, kwani hivi ndivyo ilivyokuwa katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na katika zama za Makhalifa Waongofu. Hii ni ikiwa kuna Imamu au naibu wake katika mji unaofanyika Ijumaa, lakini ikiwa hakuna mmoja wapo, kutokana na kifo au fitna au mfano wa hayo, na wakati wa Ijumaa ukafika, basi ni juu ya watu wakati huo kukusanyika kwa ajili ya mtu mmoja miongoni mwao ili awatangulie na kuwaswalisha Ijumaa.) Na sharti la idhini ya Sultani ni maoni marjuh kwetu kulingana na dalili zilizotajwa hapo awali.

Kwa ufupi, Swala ya Ijumaa ni faradhi, iwe Khalifa yupo au hakuwepo Khalifa.

Share Article

Share this article with your network