(Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni mtukufu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wake kwenye ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi")
Jibu la Swali
Kwa Muhammad Abu al-Asal
Swali:
Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh...
Amir wetu, Allah abariki muda wako, juhudi zako na elimu yako...
Nina swali: Je, dalili ambazo chama (Hizb) kimezitegemea katika njia (tariqah) ya kusimamisha Dola ya Khilafah ni qati’i (zenye kukata)?
Jibu:
Walaikum Assalam Warahmatullahi Wabarakatuh,
Hakika hatua tatu kwa ujumla wake dalili zake ni qati’i:
- Mtume ﷺ alilingania kwa siri mwanzoni mwa kulingania (da’wah) kwa takriban miaka mitatu, na alikuwa akiwafunza Waislamu utamaduni wa Kiislamu (thaqafah) katika nyumba ya Al-Arqam bin Abi al-Arqam...
- Kisha akatangaza da’wah na kuibainisha wazi kufuatia kuteremka kwa neno lake Allah (swt):
فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ
"Basi tangaza kwa dhahiri uliyopewa amri (na Mola wako), na jitenge na washirikina." (Al-Hijr [15]: 94)
Nayo ni qati’i al-thubut (yakini katika usimulizi) na qati’i al-dalalah (yakini katika maana) kwamba Mtume ﷺ kabla ya kuteremka aya hiyo alikuwa akilingania kwa siri, na baada ya kuteremka kwake akaitangaza da’wah. Na katika kipindi hicho, Mtume ﷺ alifanya mgongano wa kifikra (sira’ al-fikri) na mapambano ya kisiasa (kifah al-siyasi), kisha mwishoni mwa hatua hiyo akatafuta nusra (talab al-nusrah):
Kuhusu mgongano wa kifikra, alibainisha ubatili wa kuabudu masanamu, na kusimamisha hoja dhidi ya makafiri... na aya kuhusu hilo ni nyingi, miongoni mwake ni:
أَمْ خُلِقُوا مِنْ غَيْرِ شَيْءٍ أَمْ هُمُ الْخَالِقُونَ
"Je! Wao wameumbwa pasina kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?" (At-Tur [52]: 35)
قَالَ أَتَعْبُدُونَ مَا تَنْحِتُونَ * وَاللَّهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ
"Akasema: Je, mnaabudu mnavyochonga? Na hali Allah ndiye aliyekuumbeni na mnavyovifanya." (As-Saffat [37]: 95-96)
وَقَالَ اللَّهُ لَا تَتَّخِذُوا إِلَهَيْنِ اثْنَيْنِ إِنَّمَا هُوَ إِلَهٌ وَاحِدٌ فَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ
"Na Allah amesema: Msishike miungu wawili; hakika Yeye ni Mungu Mmoja tu. Basi nicheni Mimi peke yangu." (An-Nahl [16]: 51)
مَا اتَّخَذَ اللَّهُ مِنْ وَلَدٍ وَمَا كَانَ مَعَهُ مِنْ إِلَهٍ إِذًا لَذَهَبَ كُلُّ إِلَهٍ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلَا بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْضٍ سُبْحَانَ اللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ
"Allah hakujifanyia mwana yeyote, wala hakuwa pamoja naye mungu mwingine; (ingelikuwa hivyo) basi kila mungu angelyepea na viumbe vyake alivyoviumba, na baadhi yao wangeliwashinda wengineo. Ametakasika Allah na yale wanayomsifu nayo." (Al-Mu’minun [23]: 91)
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ * اللَّهُ الصَّمَدُ * لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ * وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أَحَدٌ
"Sema: Yeye Allah ni Mmoja. Allah ndiye Anayestahiki kukusudiwa (kwa mahitaji yote). Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anayefanana naye hata mmoja." (Al-Ikhlas [112]: 1-4)
قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ * لَا أَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَ * وَلَا أَنْتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ * وَلَا أَنَا عَابِدٌ مَا عَبَدْتُمْ * وَلَا أَنْتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ * لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ
"Sema: Enyi makafiri! Siabudu mnavyovijabudu. Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. Wala mimi sitaabudu mnavyovijabudu. Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. Nyinyi mna dini yenu, nami nina dini yangu." (Al-Kafirun [109]: 1-6)
na aya nyinginezo.
Na kuhusu mapambano ya kisiasa, zilitelemka aya zikiziponda akili zao, uongozi wao na upotevu wao, na aya kuhusu hilo pia ni nyingi, miongoni mwake ni:
تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ * مَا أَغْنَى عَنْهُ مَالُهُ وَمَا كَسَبَ * سَيَصْلَى نَارًا ذَاتَ لَهَبٍ * وَامْرَأَتُهُ حَمَّالَةَ الْحَطَبِ * فِي جِيدِهَا حَبْلٌ مِنْ مَسَدٍ
"Imeangamia mikono miwili ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia. Mali yake hayakumfaa, wala vile alivyovichuma. Atauingia Moto wenye miale. Na mkewe, mchukuzi wa kuni. Shingoni mwake mna kamba ya kamba (ya kuitwa masadi)." (Al-Masad [111]: 1-5)
ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا * وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَمْدُودًا * وَبَنِينَ شُهُودًا * وَمَهَّدْتُ لَهُ تَمْهيدًا * ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ * كَلَّا إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا * سَأُرْهِقُهُ صَعُودًا * إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ * فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ * ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ * ثُمَّ نَظَرَ * ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ * ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ * فَقَالَ إِنْ هَذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ * إِنْ هَذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ * سَأُصْلِيهِ سَقَرَ * وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ * لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ * لَوَّاحَةٌ لِلْبَشَرِ * عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ
"Niache mimi na niliyemuumba peke yake. Na nikampa mali nyingi. Na wana wa kishuhuda. Na nikamtengenezea kila aina ya urahisi. Kisha anatumai nimzidishie. Hasha! Hakika yeye alikuwa mpinzani wa aya Zetu. Nitamtesa kwa kumuandamia mashaka makubwa. Hakika yeye alifikiri na akapanga. Basi akaangamia, namna gani alivyopanga! Kisha akaangamia, namna gani alivyopanga! Kisha akatazama. Kisha akakunja uso na akakasirika. Kisha akapa mgongo na akatakabari. Akasema: Haya si lolote ila ni uchawi uliozoeleka. Haya si lolote ila ni kauli ya binadamu. Nitamuingiza kwenye Moto wa Saqar. Na nini kitakujulisha ni nini huo Moto wa Saqar? Haubakishi wala hauachi. Unababua ngozi ya binadamu. Juu yake wapo (malaika) kumi na tisa." (Al-Muddathir [74]: 11-30)
وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَهِينٍ * هَمَّازٍ مَشَّاءٍ بِنَمِيمٍ * مَنَّاعٍ لِلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ * عُتُلٍّ بَعْدَ ذَلِكَ زَنِيمٍ * أَنْ كَانَ ذَا مَالٍ وَبَنِينَ * إِذَا تُتْلَى عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ * سَنَسِمُهُ عَلَى الْخُرْطُومِ
"Wala usimtii kila mwingi wa kuapa, duni. Msema hovyo, anayetembea akifanya masengenyo. Mwenye kuzuia kheri, dhalimu, mwenye madhambi mengi. Mkatili, na kando na hayo, ni mtoto wa haramu. Kwa kuwa ana mali na wana. Anaposomewa aya Zetu husema: Hizi ni hadithi za watu wa kale. Tutamtia alama kwenye pua yake." (Al-Qalam [68]: 10-16)
na aya nyinginezo.
Na kuhusu kutafuta nusra kwa Mtume ﷺ kutoka kwa wenye nguvu na kinga, basi alitafuta kwa makabila yenye nguvu... na akamtuma Mus’ab (ra) kwenda Madinah, ambapo Maansari walimuitikia, na kukawa na Baia ya pili ya Aqabah...
- Kisha kufuatia hayo, Mtume ﷺ akasimamisha Dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Madinah Al-Munawwarah.
Hivyo basi, hatua hizi tatu dalili zake ni qati’i, lakini kuna baadhi ya maelezo madogo ndani yake yaliyosimuliwa kupitia riwaya dhanni, kama vile maelezo ya kulingania kwa siri... na maelezo ya kutangaza da’wah na baadhi ya maelezo katika mgongano wa kifikra na mapambano ya kisiasa... na maelezo ya Hijra na kusimamisha Dola baada ya Baia ya pili ya Aqabah... baadhi ya maelezo haya dalili zake ni dhanni sahihi. Na yeyote anayetafakari vitabu vyetu na dalili zetu, ataona wazi kuwa hatua hizo tatu dalili zake ni qati’i, na baadhi ya maelezo ambayo dalili zake ni dhanni yamekamilika kwa njia ya istinbati.
Namuomba Allah (swt) kuwa picha hii imekuwa wazi kwako.
Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah
17 Shawwal 1439 H Inayoafikiana na 01/07/2018 M
Kiungo cha jibu kutoka ukurasa wa Amir (Allah amuhifadhi) kwenye Facebook
Kiungo cha jibu kutoka ukurasa wa Amir (Allah amuhifadhi) kwenye Google Plus