Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali Kuhusu Yai Lililorutubishwa

January 03, 2012
3533

Jibu la Swali

Kuhusu Yai Lililorutubishwa

Swali:

Kwanza: Ikiwa manii ya mume yataunganishwa na yai la mke katika maabara, kisha yai hilo lililorutubishwa likawekwa katika mji wa uzazi wa mwanamke mwingine ambaye amekubali kubeba mimba ya mtoto kwa sababu mke hawezi kubeba mimba kimatibabu au kwa sababu nyingine yoyote... Je, jambo hilo linaruhusiwa? Tafadhali zingatia kuwa mwanamume na mwanamke wenye yai lililorutubishwa ni wanandoa.

Pili: Itakuwaje ikiwa mwanamke mwingine huyo alikuwa ni mke wa pili wa mwanamume huyo? Je, kuna mazingira yoyote yanayoruhusu hili, kama vile mume kumtishia mke wake mwingine kwa talaka ikiwa hatokubali kuhamishiwa yai lililorutubishwa la mke mwenza wake?

Jibu:

Haijuzu kuchukua manii ya mume pamoja na yai la mke kisha kuyarutubisha kwa pamoja katika maabara, na baada ya hapo kulihamisha yai lililorutubishwa kwenda kwa mwanamke mwingine... Jambo hili halijuzu na ni haramu. Badala yake, ni lazima yai lililorutubishwa lirudishwe kwa mke ambaye ndiye mama mwenye yai hilo. Hii ni kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):

وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ

"Na akina mama watawanyonyesha watoto wao." (Al-Baqarah [2]: 233)

Na upande wa utoaji dalili ni kuunganishwa kwa neno al-walidat (waliozaa) na neno awladahunna (watoto wao), yaani mwanamke anayezaa mtoto ndiye anakuwa mama wa mtoto huyo. Kwa hivyo, haijuzu kwa mwanamke kumzaa mtoto ambaye si wake.

Kadhalika kauli ya Mwenyezi Mungu (swt) katika aya tukufu:

إِنْ أُمَّهَاتُهُمْ إِلَّا اللَّائِي وَلَدْنَهُمْ

"Mama zao si wengine ila ni wale waliowazaa." (Al-Mujadilah [58]: 2)

Na aya tukufu:

وَاللَّهُ أَخْرَجَكُمْ مِنْ بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ

"Na Mwenyezi Mungu amekutoeni matumboni mwa mama zenu." (An-Nahl [16]: 78)

Basi yule anayezaa ndiye mama. Kwa hiyo, si halali kwa mwanamke kuzaa isipokuwa yule ambaye yeye ndiye mama yake.

Na hakuna mazingira yoyote yanayورuhusu kufanya haramu hii, sawa mwanamke huyo akitishiwa talaka asipofanya hivyo au tishio lolote lile. Kwani haki ndiyo inayostahiki kufuatwa, na anayebeba dhambi ni yule anayemtishia mwanamke katika hali hii.

Kwa muhtasari: Ikiwa matibabu yatahitaji kurutubisha yai la mke kwa manii ya mumewe katika maabara, basi ni lazima yai lililorutubishwa lirudishwe katika mji wa uzazi wa mke mwenye yai hilo na si kwa mwanamke mwingine yeyote, hata kama ni mke wa pili wa mume huyo, kinyume na hivyo itakuwa ni haramu.

Share Article

Share this article with your network