Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jawabu la Swali: Kuhusu Hizb ut-Tahrir na Mapinduzi ya Syria

July 10, 2013
4585

(Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni Ata bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wageni kwenye ukurasa wake wa Facebook)

Kwa Mamoun Shehadeh Mamoun Shehadeh

Swali:

Mwanachuoni Ata bin Khalil Abu al-Rashtah

Salamu, kisha:

Kutoka kwa Mamoun Shehadeh / Mwandishi wa habari na mchambuzi wa kisiasa

Ningependa kuwauliza, ni misukumo gani iliyoifanya Hizb ut-Tahrir kuelekea kujiingiza katika mapinduzi ya Syria, na kwa nini isiwe sehemu nyingine?

Jibu:

Wa Alaykumus Salaam wa Rahmatullahi wa Barakatuh

Hakika kazi yetu ewe ndugu yangu ni ile ile, haijabadilika katika kila sehemu ambayo tuna uwezo wa kufanya kazi... na kazi yetu ni kubeba Dawah (ulinganifu) kwa ajili ya kuanza tena maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashidah kulingana na mbinu aliyoichora Mtume wa Allah (saw) kwa ajili yetu tangu kupewa utume kule Makkah Al-Mukarramah mpaka aliposimamisha Dola kule Al-Madinah Al-Munawwarah. Hivyo, tunawasiliana na watu kuwaita kwenye haki, na kwamba Khilafah ni faradhi tukufu ambayo lazima waifanyie kazi... na tunaingiliana na Umma katika hilo, tukifanya kazi pamoja nao na kupitia kwao ili kufanikisha jambo hili. Vile vile, tunawasiliana na wenye nguvu (Ahlul Quwwah) tukiomba nusra yao kwa ajili ya kusimamisha Khilafah, na tunawanasihi wasipoteze juhudi zao bure kwa kutosheka na kubadilisha watu bila ya kubadilisha mfumo mzima wa kisekular wa kutungwa na mwanadamu,

bali watoe juhudi zao, nguvu zao na dhabihu zao katika kuubadilisha mfumo wa kutungwa kutoka kwenye mizizi yake pamoja na watawala wake na sheria zake, na kusimamisha Khilafah...

Na tunawabainishia jambo hili kikamilifu kama lilivyokuja katika Uislamu. Anayetuitikia, tunamuongoza kwenye muelekeo sahihi, na asiyetuitikia, basi hatuwezi kumlazimisha kuitikia bali tunamuombea uongofu...

Hili ndilo tunalolifanya kabla ya mapinduzi, wakati wake na baada yake... isipokuwa hali ya mapinduzi imetengeneza uwanja mpana zaidi wa kuwafanya watu wasikilize neno la haki bila ya hofu ya vyombo vya usalama kama ilivyokuwa hapo awali, ambapo walikuwa wakijiepusha nasi kwa kuhofia vyombo hivyo vya usalama. Na kwa sababu hii, inaonekana hivi leo watu wakiwa wametuzunguka na kutukubali, na kuwepo kwa harakati ya mwingiliano wa dhati na wenye nguvu kati yetu na wao. Hivyo, imeonekana kupanuka kwa uwanja wa Dawah tunayoibeba zaidi kuliko hapo awali kwa sababu kizingiti cha hofu kimeondolewa mbele ya watu...

Kutokea hapa, kumeingia uchunguzi wako kuhusu nguvu ya harakati yetu na kuongezeka kwake ndani ya Umma kuliko hapo awali. Na hiyo si kwa sababu hatukuwa tukifanya kazi hapo awali, bali ni kwa sababu watu kabla ya mapinduzi walikuwa wakiogopa kuelekea kwetu kwa hofu ya vyombo vya usalama ambavyo vilikuwa vikitufuata na kumfuata kila anayewasiliana nasi. Jambo hili lilikuwa likisababisha vikwazo kwa kazi zetu na kuweka kizuizi mbele ya watu ikiwa wanataka kutukaribia...

Na kwa ufahamu, hakika kazi yetu haionekani kwa nguvu katika maeneo ya mapinduzi pekee, bali iko vivyo hivyo katika maeneo mengine, na wakati mwingine inakuwa na kasi zaidi kuliko maeneo ya mapinduzi... na huenda unaona na kusikia kwamba shughuli zetu nchini Pakistan kwa mfano, ni dhahiri na zenye nguvu kama unavyoziona nchini Syria au mfano wa hayo, pamoja na kwamba Pakistan kwa sasa haina mapinduzi...

Muhtasari ni kwamba kazi yetu ilikuwepo kabla ya mapinduzi, lakini ilipanuka kwa namna inayovutia macho wakati wa mapinduzi, na haswa nchini Syria, kwa sababu kizingiti cha hofu kimeporomoka mbele ya uamsho wa watu dhidi ya dhulma na udikteta...

Hili ndilo jambo jipya katika suala hili, lakini sisi tulikuwa tukifanya kazi kabla ya mapinduzi, wakati wake na baada yake.

Ama ikiwa unamaanisha kwa neno "kujiingiza katika mapinduzi" kwamba tumekuwa na mrengo wa kijeshi, basi hilo ni kosa na haliwezekani. Kwani hatuna mrengo wa kijeshi, si hapo awali wala hapo baadaye. Sisi ni chama cha kisiasa ambacho msingi wake ni Uislamu, hakifanyi vitendo vya kimaada katika hatua ya Dawah, bali kinaomba nusra ya wenye nguvu ili waweze kukiwezesha kusimamisha Dola kama ilivyotokea kwa Mtume wa Allah (saw) katika Baia ya pili ya Aqaba, na huenda ikawa karibu.

إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا

"Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu amekwisha kiwekea kila kitu kipimo chake." (QS. At-Talaq [65]: 3)

Ndugu yenu, Ata bin Khalil Abu al-Rashtah

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir kwenye Facebook

Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir kwenye Google Plus

Share Article

Share this article with your network