Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: Kuhusu Kuvaa Wigi (Baruka) Kwa Ibrahim Khabbash

June 28, 2013
4935

(Mfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut Tahrir, kwa Maswali ya Wageni wa Ukurasa Wake wa Facebook)

Jibu la Swali:

Kuhusu Kuvaa Wigi

Kwa Ibrahim Khabbash

Swali:

Allah awalipe kila la kheri na atunufaishe kupitia elimu yenu. Hata hivyo, kuna upande mmoja wa swali ambao haukujibiwa, tungependa kama mgeugusia - Sheikh wetu - nao ni (ni upi hukumu yake kwa ujumla/katika chuo?) kwa maana kama mwanamke yuko nyumbani kwake, je, inaruhusiwa kwake kuvaa wigi au inachukua hukumu ya al-wasilah (anayewaunga nywele) na al-mustawsilah (anayeungwa nywele)?

Jibu:

Wa Alaikum Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh.

Tulikwisha jibu swali hili hapo awali na kulichapisha kwenye ukurasa:

Kwamba haijuzu kuvaa wigi na kutoka nalo nje kwa sababu ni tabarruj (kujirembesha kuliko haramu). Na tulisema kuwa vazi la maisha ya hadharani (al-hayat al-ammah) linashartiwa kuwa na mambo haya matatu kwa pamoja: (kusitiri uchi/awrah, kutokuwa na tabarruj, na kuvaa jilbab). Na kuvaa wigi ni tabarruj, hivyo basi haijuzu kutoka nalo nje isipokuwa ikiwa kilemba (khimar) kitakifunika kabisa.

Kwa hivyo, ikiwa ulimaanisha kwa neno "al-kulliyah" (chuo) kwamba mwanamke aende chuoni akiwa amevaa wigi, basi haijuzu. Ama akiwa ndani ya nyumba yake, inajuzu kuivaa mradi asionekane ndani ya nyumba hiyo isipokewa na maharimu wake na mumewe. Ama kaka wa mumewe, haijuzu kwake kuliona wigi kichwani mwake.

Ama kuhusu iwapo wigi ina maana sawa na al-wasilah na al-mustawsilah, basi jambo si hivyo. Kwa sababu al-wasilah ni yule anayeunga nywele zake na nywele nyingine ili kuzirefusha, na si kwamba anavaa wigi juu ya nywele zake, bali anafunga nywele nyingine kwenye nywele zake ili zionekane ndefu. Na hili ni haramu popote alipo mwanamke, hata ndani ya nyumba yake, kwa mujibu wa hadith iliyopokelewa na Al-Bukhari kutoka kwa Abu Hurayrah (ra), kutoka kwa Mtume (saw) aliyesema:

لَعَنَ اللَّهُ الوَاصِلَةَ وَالمُسْتَوْصِلَةَ

"Mwenyezi Mungu amemlaani mwenye kuunga nywele na mwenye kuungwa nywele..." (Imepokelewa na Al-Bukhari)

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir kwenye Facebook

Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir kwenye Google Plus

Share Article

Share this article with your network