Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: Kuhusu Mfumo wa Utawala katika Uislamu

November 02, 2011
1326

Swali: Imekuja katika kitabu cha "Al-Ajhiza" ukurasa wa 16, ibara inayosema "Mfumo wa utawala katika Uislamu si wa kidemokrasia kwa maana halisi ya demokrasia", kana kwamba katika ibara hiyo kuna utata... ni nini faida ya kutaja "maana halisi"? Tunatarajia ufafanuzi, na Allah awalipe heri.

Jibu: Kilichokuja katika kitabu cha Al-Ajhiza ukurasa wa 16 ni kama ifuatavyo:

"Na mfumo wa utawala katika Uislamu si wa kidemokrasia kwa maana halisi ya demokrasia, kwa upande wa kwamba utungaji sheria ni wa watu; wanahalalisha na kuharamisha, wanaona kizuri na kuona kibaya. Na kwa upande wa kutofungamana na hukumu za kisheria kwa kisingizio cha uhuru. Na makafiri wanatambua kuwa Waislamu hawatakubali demokrasia kwa maana yake halisi hii; ndiyo maana mataifa ya kikafiri ya kikoloni (na hasa Marekani leo) yanajaribu kuipigia debe katika nchi za Waislamu kwa kuiingiza kwao kupitia mlango wa upotoshaji, kwamba demokrasia ni mbinu ya kumchagua mtawala... Nao wakazunguka na kuichenga sehemu ya msingi ndani yake, nayo ni kuwa utungaji sheria, uhalalishaji na uharamishaji unakuwa ni wa binadamu na si wa Mola wa binadamu... wakijiepusha na maana halisi iliyowekwa na wenyewe (waanzilishi wake) ya kwamba inamaanisha enzi (sovereignty) ni ya watu, ambapo wanatunga sheria wanazotaka kwa maoni ya wengi, wanahalalisha na kuharamisha, wanaona kizuri na kuona kibaya. Na kwamba mtu yuko (huru) katika vitendo vyake, hufanya atakalo; hunywa pombe, huzini, huritadi, hutukana matukufu na kuyakebehi, chini ya jina la demokrasia na uhuru wake. Hii ndiyo demokrasia, na huu ndio uhalisia wake, maana yake na ukweli wake. Basi vipi kwa Muislamu anayemwamini Allah athubutu kusema kuwa demokrasia inajuzu, au kwamba inatokana na Uislamu?!

Ama suala la Umma kumchagua mtawala, yaani kumchagua Khalifah, hilo ni jambo lililowekwa na maandiko (nass)..." Mwisho.

Na ni wazi kutokana na hayo kwamba kutajwa kwa 'maana halisi' kulikuwa ni kwa ajili ya kupambanua demokrasia katika maana yake halisi ya kiistilahi na ile maana wanayoipigia debe kuwa ni uchaguzi... na hiyo ni kwa sababu baadhi ya watu wanadhani kuwa ni mchakato wa uchaguzi pekee, na hii siyo maana halisi ya demokrasia.

Ama kumchagua mtawala na kumpa bay’ah, hilo lipo katika Uislamu karne nyingi kabla ya Magharibi kulijua...

5 Dhul-Hijjah 1432 AH 02/11/2011 AD

Share Article

Share this article with your network