(Silsila ya Majibu ya Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut Tahrir, kwa Maswali ya Wageni wa Ukurasa Wake wa Facebook)
Kwa Samer Abu Omar
Swali:
As-Salaamu Alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuhu.
Je, yanayotokea nchini Iraq ni mipango ya Amerika ili kukamilisha mpango wake wa kuigawanya nchi hiyo, au ni mchezo wa Ulaya kwa ajili ya kuidhoofisha Amerika, au ni harakati ya ndani yenyewe? Tafadhali tufahamishe, Mwenyezi Mungu akulipe kheri.
Jibu:
Wa Alaykumus Salaam wa Rahmatullahi wa Barakatuhu,
Hakika sera ya Amerika nchini Iraq tangu ilipoweka zuio la anga kaskazini mwa Iraq "Kanda ya Kurdistan" mwaka 1991, imekuwa ikilenga kusambaratisha umoja wa Iraq. Tangu wakati huo, Kurdistan ya Iraq ikawa kama nusu dola. Na wakati Amerika ilipoivamia Iraq mwaka 2003, ilileta vibaraka wake juu ya vifaru vyake wakiwa wamejaa chuki za kisekta na kimadhehebu... Kisha mtawala wa Kimarekani, Bremer, akaweka mbegu ya muhasasah (ugawaji wa madaraka kulingana na madhehebu) katika utawala, na kanda (mikoa)... Kisha ikatungwa katiba iliyobeba ndani yake kusambaratika kwa dola; ambapo Rais wa nchi akawa Mkurd, Spika wa Bunge akawa wa Sunni, na Waziri Mkuu akawa wa Shia... Kwa hiyo, mazingira nchini Iraq yakawa tayari kwa mgawanyiko kwa kisingizio cha mikoa au kanda.
Kwa msingi huo, inaweza kusemwa kuwa yanayotokea nchini Iraq kwa sasa ya kusambaratika, yanatokana na mbegu za muhasasah katika utawala na kanda ambazo Amerika ilizipanda wakati wa uvamizi wake nchini Iraq. Baadaye, zana za Amerika nchini Iraq zikazishughulikia mbegu hizo, miti yake, na matunda yake kwa kuyapalilia kwa mbolea na maji...!
Ni wajibu kwa Umma kutambua kuwa umoja wake ni faradhi, na kwamba ni Umma mmoja, na ni lazima uwe na dola moja na mtawala mmoja. Hili si nchini Iraq pekee, bali katika nchi zote za Waislamu, zikijivika chini ya Bendera ya Al-Uqab, bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), bendera ya Khilafah Rashidah ambayo tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu irudi karibuni, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu na Mwenye Kushinda.
Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Facebook
Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir
Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Google Plus