Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: Ijmaa ya Masahaba - Ufafanuzi wa Mujmal

September 09, 2014
4043

(Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni mtukufu Ata bin Khalil Abu al-Rashta, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi")

Kwa: Abu al-Walid ash-Shami

Swali:

As-salaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh, Mwenyezi Mungu akunusuru na akufanikishe katika yale anayoyapenda.. Nina swali ambalo ni: Imekuja katika kitabu cha Al-Shakhsiyyah al-Islamiyyah Juzuu ya 3, ukurasa wa 269 katika mlango wa Al-Bayan (Ufafanuzi) yafuatayo: (Na ufafanuzi unakuwa ni kauli kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, na unakuwa ni kitendo kutoka kwa Mtume). Swali langu ni kuwa, Ijmaa ya Masahaba haikutajwa katika ufafanuzi, je, Ijmaa ya Masahaba inachukuliwa kuwa ni ufafanuzi wa mujmal (kauli fupi/ya jumla inayohitaji ufafanuzi)? Na je, Khilafah na hukumu zake ambazo Masahaba walizitekeleza na kuzibainisha zinachukuliwa kuwa ni ufafanuzi wa mujmal wa aya:

وَأَنِ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ

"Na wahukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu." (QS Al-Ma'idah [5]: 49)

Naomba ufafanuzi? Was-salaamu Alaykum. (Mwisho).

Jibu:

Wa Alaykumus Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh,

Kile kilichoelezwa katika kitabu cha Al-Shakhsiyyah Juzuu ya 3: "Na ufafanuzi unakuwa ni kauli kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, na unakuwa ni kitendo kutoka kwa Mtume...", andiko hili linajumuisha Ijmaa (Makubaliano). Hii ni kwa sababu Ijmaa inafichua dalili kutoka katika Sunnah ambayo Masahaba walikuwa wakiijua. Hivyo, suala lilipowasilishwa kwao, walitoa hukumu yake bila kusimulia hadith kwa sababu ilikuwa inajulikana kwao.

Kwa mfano: Waliletewa suala la mirathi ya babu pamoja na mtoto, yaani pindi mtu anapofariki na kuacha mtoto na babu, ni kiasi gani babu anarithi? Masahaba walikubaliana (Ijmaa) kuwa anarithi sudusi (moja ya sita). Hii inamaanisha kuwa walisikia hadith kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kuhusu jambo hilo, na kwa sababu walikuwa wanaijua, walitaja hukumu bila kutaja dalili. Na kwa ajili hiyo inasemwa kuwa Ijmaa ya Masahaba inafichua dalili (kashf an ad-dalil), yaani inafichua hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ambayo Masahaba hawakuisimulia bali walitaja hukumu moja kwa moja.

Hivyo basi, andiko lililotajwa katika Al-Shakhsiyyah linajumuisha Ijmaa ndani yake kwa sababu Ijmaa inafichua hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Imekuja katika kitabu cha Al-Shakhsiyyah Juzuu ya 3 katika mlango wa Ijmaa, ukurasa wa 295 yafuatayo:

(Nne: Ijmaa ya Masahaba inarudi kwenye lile andiko la kisheria lenyewe (an-nass ash-shar'i). Kwani wao hawakubaliani juu ya hukumu isipokuwa wawe na dalili ya kisheria kutokana na kauli ya Mtume, kitendo chake, au kunyamaza kwake (taqrir), ambayo wameitegemea. Hivyo basi, Ijmaa yao inakuwa imefichua dalili... kwani Masahaba hawakukubaliana juu ya jambo lolote isipokuwa wawe na dalili ya kisheria juu ya hilo ambayo hawakuisimulia. Kwa hiyo, Ijmaa ya Masahaba inakuwa ni dalili ya kisheria kwa sifa yake ya kufichua dalili...) Mwisho.

Kutokana na hapa, jibu la swali lako la mwisho linakuwa wazi... Ndiyo, yale yaliyokuja katika Ijmaa ya Masahaba (rd) katika maudhui ya Khilafah ni ufafanuzi wa yale yaliyokuja katika Qur'an Tukufu miongoni mwa aya za utawala.

Ndugu yenu, Ata bin Khalil Abu al-Rashta

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir kwenye Facebook

Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir kwenye Google Plus

Share Article

Share this article with your network