** (Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni Ata bin Khalil Abu Al-Rashta, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya watazamaji wa ukurasa wake wa Facebook)**
Kwa Hatem M. Faour
Swali:
Sheikh wetu mpendwa Ata Abu Al-Rashta,
Assalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh.
Mtume wa Allah (saw) amesema: «Mwenye kufa hali ya kuwa hakupigana (ghazw), na wala hakuizungumzisha nafsi yake kwa ajili hiyo, amekufa juu ya tawi miongoni mwa matawi ya unafiki.» Ni vipi inakuwa kuzungumza na nafsi kuhusu kupigana (ghazw)? Mwenyezi Mungu akubarikini na akuwafikishieni katika kila kheri.
Jibu:
Wa Alaikum Assalam Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh.
Muslim ametoa katika Sahih yake kutoka kwa Abu Hurairah, amesema: Mtume wa Allah (saw) amesema:
مَنْ مَاتَ وَلَمْ يَغْزُ، وَلَمْ يُحَدِّثْ بِهِ نَفْسَهُ، مَاتَ عَلَى شُعْبَةٍ مِنْ نِفَاقٍ
"Mwenye kufa hali ya kuwa hakupigana vita vya jihadi, na wala hakuizungumzisha nafsi yake kuhusu hilo, amekufa juu ya tawi miongoni mwa matawi ya unafiki." (HR. Muslim)
Pia hadithi hii imetolewa na Ahmad katika Musnad yake, Abu Dawood katika Sunan yake, An-Nasa'i katika Sunan, na Al-Hakim katika Al-Mustadrak.
Ama maana yake ni: Muislamu awe na azma ya kuwa atatoka kupigana ikiwa Khalifah atamtaka atoke kuanzisha mapigano kwa ajili ya ukombozi (al-fath) na kueneza Uislamu, ikiwa hana udhuru. Vile vile, awe na azma ya kushiriki katika jihadi ya kujihami (qital ad-daf') ikiwa makafiri watashambulia nchi za Waislamu, ikiwa ana uwezo na hana udhuru. Na lazima awe mkweli katika nia na azma yake hiyo; na yote haya ni kwa sababu ya umuhimu wa Jihadi katika Uislamu. At-Tabarani ametoa katika Al-Mu’jam al-Kabir kutoka kwa Abu Umamah, kutoka kwa Mtume (saw) amesema:
ذُرْوَةُ سَنَامِ الْإِسْلَامِ: الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ لَا يَنَالُهُ إِلَّا أَفْضَلُهُمْ
"Kilele cha utukufu wa Uislamu ni jihadi katika njia ya Allah; haifikiliwi (jihadi hiyo) isipokuwa na walio bora miongoni mwao." (HR. At-Tabarani)
Na Ibn Abi Asim ametoa kutoka kwa Abu Dharr, kutoka kwa Mtume (saw) amesema:
ذِرْوَةُ سَنَامِ الْإِسْلَامِ الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، لَا يَنَالُهُ إِلَّا أَفْضَلُهُمْ
"Kilele cha utukufu wa Uislamu ni jihadi katika njia ya Allah; haifikiliwi isipokuwa na walio bora miongoni mwao." (HR. Ibn Abi Asim)
Ndugu yenu, Ata bin Khalil Abu Al-Rashta
Link ya jibu kutoka kwa ukurasa wa Amir kwenye Facebook
Link ya jibu kutoka kwa tovuti ya Amir
Link ya jibu kutoka kwa ukurasa wa Amir kwenye Google Plus